Prince Nadheem
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 1,259
- 1,056
Habari za jumapili ya leo? Natumai wengi mmetulia mkijitathmini namna ya kuanza mikiki mikiki ya wiki mpya mbele yetu.
Nimekuja hapa nikiwa nina shida moja, gari yangu siielewi.
Gari ilianza kupunguza oil, nikaona hapo overhaul yanihusu. Kutokana na sababu za kifedha nikaona niwe naangalia tu oil isiishe kwa kujazia pindi inapotokea imepungua hadi nipate pesa ya overhaul.nilipoipeleka service ya mwisho juzi baada ya km 3000 kutimia niliweka Oil yangu ya Siku zote (BP Premium.).
Siku ya pili kuwasha gari nikaona inatoa moshi mwingi sana wa blue. Ila gari ikitembea kidogo moshi unakata na siku nzima haitoi moshi zaidi ya asubuhi.
Sasa imekuja na ugonjwa mpya tena. Nikiiwasha inawaka vizuri tu halafu baada ya kama dakika mbili unaanza mvumo kama nimewasha mota ya kuoshea kioo cha mbele na wiper (hapo gari inakuwa na milio miwili)ila haiathiri mlio wa gari.
Nimechunguza ila sijapata hata sehemu ya kuihisi kuhusika.
Naombeni mawazo yenu kama hii shida inahusiana na oil pump au chujio limejaa uchafu au ni kitu gani.
Gari kwa sasa nimeipaki hadi ijumaa ijayo ndio nafikiria kuipeleka garage maana nataka pia nisimamie kila hatua, najua nikianza nayo ijumaa basi j2 ijayo narudi na gari.
Please usichangie mzaha wala utani. Kama huna mchango pita kimya kimya tu.
NB: gari ni Toyota Corolla 5A ya 1998, imetembea km 127,000 hadi sasa