ROJA MIRO
Member
- Jul 19, 2021
- 52
- 56
Bei za baadhi ya sigara nchini Tanzania kutokana na majibu ya wauzaji wa Sigara mnamo mwezi July 2021 wilayani Pangani Mkoani Tanga.
| BAADHI YA SIGARA | BEI ZA SIGARA HIZO KWA SASA | |
| BEI YA PAKTI MOJA | BEI YA SIGARA MOJA | |
| Winston & Master Club | Tsh1600/= | Tsh 100/= |
| Sports Club & Sm Club | Tsh 3000/= | Tsh 150/= |
| Portsman (Sports Kawaida) | Tsh 3400/= | Tsh 200/= |
| Embasy | Tsh 4500/= | Tsh 250/= |
NB: Kwa mujibu wa maoni ya wauzaji wasigara kwenye maduka ni kwamba kiwango cha chini cha mvutaji wa sigara ni wastani wa sigara 10 kwa siku na pia wanunuaji wengi hununua kwa bei ya reja reja.
Matumizi kwa Siku,Mwezi na Mwaka.
Mchanganuo wa kiasi cha Pesa anchotumia mtu mtu kununua sigara kwa siku,mwezi hadi mwaka kutokana na bei zilizooneshwa kwenye jedwali hapo juu.
1.Winston & Master Club.
Sigara 10 X 100 hivyo ni sawa na Tsh 1000/= kwa siku.
Tsh 1000 X 30 hivyo ni swan a Tsh 30,000/= kwa mwezi.
Tsh 30,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 360,000 kwa mwaka.
2.Sports Club & Sm Club.
Sigara 10 X 15O hivyo kwa siku sawa na Tsh 1500.
Tsh 1500 X 30 hivyo ni sawa na Tsh 45,000/- kwa mwezi.
Tsh 45,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 540,000 kwa mwaka.
3.Portsman (Sports Kawaida).
Sigara 10 X 200 hivyo kwa siku ni sawa na Tsh 2000/=
Tsh 2000 X 30 hivyo kwa mwezi ni sawa na Tsh 60,000/=
Tsh 60,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 720,000/=
4.Embassy.
Sigara 10 X 250 hivyo ni sawa na Tsh 2500 kwa siku.
Tsh 2500 X 30 hivyo ni sawa na Tsh 75,000 kwa mwezi.
Tsh 75,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 900,000/= kwa mwaka.
Madhara ya Sigara kiuchumi.
NB:- Kwa takwimu za hapo juu mvuta sigara hutumia kiasi cha Tsh 360,000/= hadi Tsh 900,000/= kwa mwaka kununua sigara.
Ripoti ya Makadirio ya Idadi ya Watu kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2035, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa, amesema Umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kutoka miaka 37 mwaka 1978 na kufikia miaka 65 mwaka 2018.
Kijana nchini Tanzania huanza kuwa na maamuzi akifikia miaka 18 na kama akianza shule na miaka 7 hadi anafikisha miaka 18 tayari atakuwa amemaliza kidato cha nne hivyo hapo atakuwa mtu mzima na mimi kama muandaaji wa makala hii nachukulia kama mtu ataanza kuvuta sigara akiwa na miaka 18.
Ukokotozi.
Makadirio ya maisha ya mtanzania kwa sasa ni miaka 65
Kama mtu akianza kuvuta sigara na miaka 18(Hapa tunamuhesabu kama mtu mzima)
Soln 65-18=maana yake maisha yake yote atakuwa na wastani wa miaka 47 ya kuvuta sigara.
Fanya, Kwa takwimu za jedwali hapo juu mvuta sigara hupoteza kiasi cha chini cha Tsh 360,000/= na cha juu hadi Tsh 900,000/= kwa mwaka kununua sigara.
Tafuta kiasi maisha yake yote.
Sawa na 1. Tsh 360,000 X 47=Tsh 16,920,000/=
2. Tsh 900,000 X 47=Tsh 42,300,000/=
HIVYO:- Mvuta sigara Tanzania hutumia kiasi cha Tsh 16,920,000/= hadi Tsh 42,300,000/= kununua sigara kipindi chote cha maisha yake
Uvutaji wa Sigara hupingwa?
NDIO:-Tarehe 31 Mei ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku.
Mnamo tarehe 8 Disemba 2020 Shirika la Afya Duniani,WHO lilizindua kampeni ya mwaka mzima kwa jina "Jitolee kuacha kuvuta." Walipokuwa wanaelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutovuta tumbaku kwa mwaka 2021.
picha kwa hisani ya mtandao
Madhara ya kiafya ya Uvutaji wa Sigara.
Ripoti ya shirika la afya Duniani,WHO ya mwaka 2018 inaonesha, “kila mwaka watu wapatao milioni 8 hufariki dunia kutokana na tumbaku. Mamilioni ya wengine wanaishi na magonjwa sugu kama vile saratani, Kifua Kikuu, pumu au magonjwa sugu ya njia ya hewa yanayosababishwa na matumizi ya tumbaku.” Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema matumizi ya tumbaku hayajaacha watoto salama kwa kuwa, “zaidi ya watoto 60,000 wenye umri wa chini ya miaka 5 hufariki dunia kutokana na kuvuta moshi watu wavutao sigara.
Picha kutoka mitandao ya afya
Namna ya kuacha kuvuta sigara
Utafiti wa karibuni zaidi umeonesha kwamba njia bora zaidi ya kuacha uraibu wa kuvuta sigara ni kuacha mara moja.
-Utafiti ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Annals of Internal Medicine unasema washiriki walioacha mara moja walikuwa na uwezekano mara 25% zaidi ya kutovuta sigara nusu mwaka baada ya kuachana na uraibu huo wakilinganishwa na walioacha uvutaji sigara taratibu taratibu.
-Idara ya Afya ya Taifa Uingereza inasema njia bora zaidi ni kutenga siku fulani kuwa ya kuacha kuvuta sigara.
Weka ahadi, tenga siku na uhakikishe umefanya hivyo siku hiyo, idara hiyo inashauri.
Utafiti huo wa karibuni uliofadhiliwa na Wakfu wa Moyo wa Uingereza ulihusisha washiriki 700 wa kujitolea.
Waliwekwa kwenye makundi mawili, moja la kuacha kuvuta sigara mara moja na jingine la kuacha asteaste.
Baada ya miezi sita, ni 15.5% ya washiriki walioacha kuvuta sigara taratibu taratibu waliokuwa bado hawavuti sigara wakilinganishwa na 22% kwenye kundi la walioacha kuvuta sigara mara moja.
Tafuta msaada
Watafute wale ambao wamefaulu kuacha mazoea hayo kwa kuwa huenda zaidi ya kuelewa hisia zako, wanaweza kukusaidia. Marafiki na washiriki wa familia mara nyingi hutoa ushirikiano kwako ili uweze kutimiza azma yako.
Tembelea kliniki za kuzuia uvutaji.
Madaktari wanaweza kukupa msaada unaouhitaji endapo unafikiri ni vigumu kuacha kuvuta tumbaku.
Dawa mbalimbali zinaweza kukusaidia.
Utafiti mmoja ulibaini kuwa asilimia 88 ya watu waliofaulu kuacha kuvuta sigara wanasema walifanya hivyo bila kutumia dawa zozote. Dawa hizo huhusisha dawa mbadala ya nikotini na huwa katika mifumo tofauti kama vidonge au bazoka. Pia kuna sigara za kieletroniki (e-cigarette) ambazo zimetengenezwa na hukufanya ujisikie kama unavuta sigara ya kawaida.
Lishe.
Tafiti zinaonesha kuwa ukila matunda mengi na mbogamboga ambayo yanakiwango cha kutosha cha vitamin, nicotine inaondoka haraka kwenye mfumo wa damu.
Utafiti ulifanywa na watafiti wa afya ya jamii kutoka chuo cha Buffalo. Wavutaji 1000 wenye umri kuanzia miaka 25 nchi nzima walihusishwa. Miezi 14 baadaye watafiti waliangalia kama wahusika wameacha kuvuta ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Matoke yalikuwa hivi, wale waliokula matunda na mbogamboga zaidi walikuwa wanaelekea kuacha mara 3 zaidi ukilinganisha na wale waliokula kidogo kwa angalau siku 30. Pia walipata alama nzuri kwenye nicotine dependency test na kuvuta kidogo zaidi kila siku.
Hitimisho.
Najua wanaosoma makala hii wapo wanaovuta sigara na wanaofanya biashara hii,lengo langu sio kuharibu biashara zenu,la hasha!!! Ila nimetaka tu kuonesha madhara ya kiuchumi ya uvutaji wa sigara na katika kutaka kulipa nguvu andiko langu nikaamua kugusia na madhara ya kiafya kidogo na hapa nataka mtu aamue mwenyewe kuhusiana na kuendelea kuvuta au kuacha lakini tayari elimu imefika na ndio maana hata sigara huandikwa,’’ONYO UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO’’ hivyo angalizo muhimu ili mwisho ubakie mwenyewe na maamuzi yako basi naomba msinichukulie vibaya.
Picha kutoka mtandaoni
Upvote
10