Hali ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), bado si shwari baada ya kuibuka mvutano wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa ambayo kwa sasa inashikiliwa na FREEMAN MBOWE.
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, mvutano uliopo hivi sasa ni wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mwezi Machi mwaka 2009. Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mwezi Desemba 2008, kabla ya kuahirishwa kwa kile kinachoelezwa na wafuatiliaji wa siasa ndani ya chama hicho kuwa ni kutokana na mvutano wa uongozi unaofukuta.
Kimsingi, mvutano wa uongozi ndani ya CHADEMA ni mkubwa kiasi cha kusababisha kuibuka kwa makundi matatu yanayogombea kushika wadhifa wa Mwenyekiti. Makundi hayo yana nguvu na kila moja limejiandaa kupigana kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa linatwaa Uenyekiti wa chama hicho.
Makundi hayo ni lile linalomuunga mkono Mwenyekiti wa sasa, FREEMAN MBOWE na ambalo kwa sehemu kubwa linaundwa na viongozi na wanachama wenye nyadhifa na uhusiano mzuri na Makao Makuu ya CHADEMA. Kundi hili limeanza kujiandaa kuhakikisha kuwa MBOWE anarejea tena katika uongozi wa chama hicho, na ndiye atakuwa mgombea wa Urais wa chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Taarifa inaeleza kuwa, wafuasi wa kundi hili, wanajua MBOWE amepoteza umaarufu ndani na nje ya chama lakini wanajua kuwepo kwake katika uongozi ni jambo la kheri kwao. Kundi hili, bado linamuona MBOWE kuwa ni kiongozi mwenye mvuto na anaweza kuendelea na uongozi wa chama hicho pamoja na kuwepo kwa tuhuma na migogoro iliyochafua wasifu wake katika siku za hivi karibuni.
Hata hivyo, wafuatiliaji wa mambo ndani ya CHADEMA wanaamini kuwa, MBOWE amepoteza umaarufu hasa kutokana na kutajwa kuwa ndiye chanzo cha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza ndani ya chama hicho.
Kundi la pili na lililoibuka na ambalo linaelezwa kuwa na nguvu zaidi, ni lile linalomuunga mkono katibu wa chama hicho, DR. WILBROAD SLAA. Kundi hili linaloaminika kuwa na ngome yake katika Kanda ya Ziwa, linajenga hoja kuwa DR. SLAA ndiye mtu pekee ndani ya chama hicho ambaye anaonyesha sifa ya kukiongoza chama hicho na kukiletea tija kisiasa.
Kundi la DR. SLAA linaonekana kuwa na nguvu zaidi kwa sababu linaungwa mkono na wanachama wengi ambao wanataka kuona chama kikipata mafanikio zaidi na kurejesha imani yake kwa wananchi. Wafuasi wa DR. SLAA wanamuona kuwa hana kashifa kama alivyo Mwenyekiti wa chama, MBOWE na ndiyo maana wanataka ashike usukani ili kuokoa chama kisisambaratike.
Kambi hii, inadai kuwa CHADEMA inahitaji kupata mtu msafi (ambaye hajachafuka) anayeungwa mkono na wanachama wa kawaida na ndiye atakisadia chama hicho kuimarika katika ngazi za chini badala ya kuwa cha Makao Makuu.
Mbali na makundi hayo mawili ambayo kwa sehemu kubwa ndiyo yanaonekana kuwa na mchuano mkali, lipo kundi la tatu ambalo linaelezwa kuungwa mkono na watu wenye pesa ndani na nje ya chama hicho. Kundi hili ambalo limepachikwa jina la kundi la wenye fedha kutokana na kujumuisha wafanyabiashara matajiri, linaamini kuwa chama kinapaswa kuongozwa na watu wenye umri mkubwa kama MZEE PHILEMON NDESAMBURO.
Habari zinadai kuwa, kundi linalomuunga mkono NDESAMBURO ni lile ambalo limekuwa likinufaika na chama katika kufanya biashara zao. Hata hivyo, wanachama wasiolitaka kundi la NDESAMBURO wanadai kuwa katika kikundi chochote watu hawawi na malengo ya kufanana, wengine wanataka kutumia kikundi kujinufaisha binafsi na wengine wanataka kuona kikundi kikifanikiwa. Hivyo, hata ndani ya CHADEMA kuna wachache ambao wapo humo lakini wanataka kuhakikisha mambo yao yakifanikiwa kupitia chama na hawa ndio wanaounga mkono watu wenye pesa na walio na mawazo ya kibiashara ndani ya chama hicho.
Kuna madai kuwa kuibuka kwa kundi la tatu ni ishara ya kuwa waasisi wa chama hicho hawako tayari kuona chama kikiondoka mikononi mwao na kuwaachia wageni kutoka CCM kama ilivyo kwa DR SLAA. Hata hivyo, watu wanaojenga dhana kuwa kundi hili halina madhara kwa makundi mengine, kwa maana kwamba watu wenye umri mkubwa kama NDESAMBURO hawana jipya linaloweza kuwashawishi na kuwavutia wapiga kura ambao wengi wao ni vijana.
Aidha, kuna kundi la aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Marehemu CHACHA WANGWE. Kundi hili, linajumuisha wanaCHADEMA waliokuwa wanamtaka CHACHA WANGWE kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa (CHADEMA). Baada ya kifo cha WANGWE, kambi hii haijaamua mgombea wa kumuunga mkono kati ya kundi la MBOWE, DR SLAA na NDESAMBURO. Hata hivyo, kundi hili limeweka wazi kwamba halitamuunga mkono Mwenyekiti wa sasa, FREEMAN MBOWE.
Habari zaidi zinaonyesha kuwa kuibuka kwa mvutano huu wa kuwania uongozi wa CHADEMA, kumetokana na kubaini kuwa Mwenyekiti MBOWE amechafuka kiasi cha kuwa mzigo kwa chama, viongozi wenzake na Watanzania waliokuwa wakiunga mkono sera za CHADEMA.
Wanaopinga MBOWE wanasema kuwa, baadhi ya kashifa ambazo zinamwandama ni pamoja na ya kuacha majina yaliyopendekezwa na chama kuwa wabunge wa viti maalum na kujaza ya watu aliowataka yeye.
Kashfa nyingine ni ya chama kukimbiwa na viongozi wa juu kwenda CCM au kuanzisha chama kingine kama ilivyotokea kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, DR AMANI WALID KABOUROU ambaye alihamia CCM na PAUL KYARA aliyekuwa Mweka Hazina wa CHADEMA Taifa ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa chama cha Sauti ya Umma.
Miongoni mwa kashifa hizo, ipo pia ya matumizi mabaya ya pesa za ruzuku ikiwemo kulipa madeni yaliyotokana na matumizi ya Helkopta katika kampeni za Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
Kashfa ambayo imemchafua zaidi MBOWE katika siku za karibuni ni ya kuhusishwa na Kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake CHACHA WANGWE ambaye pamoja na mambo mengine alikuwa akihoji masuala tajwa hapo juu. Kifo cha WANGWE kimesababisha MBOWE kushambuliwa kwa mawe huko Tarime wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika hivi karibuni. Ikumbukwe pia kuwa MBOWE hakwenda kumzika WANGWE kutokana na sababu hizo hizo.
Kutokana na mlolongo wa matukio haya wana-CHADEMA wanaona ni kwa nini MBOWE asikae pembeni ili kutoa nafasi kwa watu wasio na kashfa?
Wana JF, habari hii inatupa changamoto ya kuanzisha mdahalo (debate) wa kuchanganua mipaka ya kuwajibika kwa viongozi wa kisiasa nchini. Imekuwa ni kawaida na mazoea kwa vyama vya upinzani nchini kudai viongozi wa chama tawala CCM wawajibike wakati wao hawafikirii kufanya hivyo kwa wanachama wao waliowachagua. Nimekuwa sipati jibu ni kwa nini viongozi wa kisiasa wawe wa upinzani au chama tawala ni wagumu kuwajibika ili kuonyesha mfano wa kuigwa? Je, ni udikteta au ni kukosa sifa za uongozi?
Naomba kutoa hoja.
Kwanza umeseme "Habari za Uhakika" ni kwamba kuna makundi matatu.
Lakini kwenye habari hiyo hapo juu kuna makundi manne...Kwasababu ya hilo kundi la Marehemu Wangwe uliloliongezea bila taarifa..So nakusahihisha..Ni makundi manne..Na hii ni ikiwa ni kweli kwamba habari hizi ni za uhakika.
Kwa mantiki hiyo basi ni dhahiri habari hii ni ya kipropaganda.
Tukirudi kwenye mada halisi...Hapa hata chairman Mbowe ataona kuwa mambo ya mzee wa kiraracha yanamnyemelea na binadamu hawana shukrani bali tamaa, majungu na wivu.
Mbowe amefanya kazi kubwa sana kuiweka chadema kwenye ramani ya siasa..Just kama alivofanya Mrema na nccr na tlp.
Tamaa ya madaraka na urais ndiyo mgogoro ulipo na ikifika kwenye issue hiyo watu hawana hiyana na wana kudrop like a hot potatoe...Hii ilipelekea Mrema kuitwa dikteta kwasababu watu wenye nia mbaya ni wengi na wana uwezo wa kuingia kwenye nafasi nyeti kwani mapandikizi si watu wa hovyo bali wasomi na wenye ushawishi na wakishaingia ndani ya chama na kujidai ni wenzako basi hapo wanachama waliokuwa na imani na wewe ni rahisi kupotoshwa kwa propaganda za wanachama wabaya na mashabiki wa mapandikizi na mamluki wenye tamaa na chuki, wenye kujidai wana uchungu na chama mara baada ya chama chenyewe kupata umaarufu zaidi, kupewa nguvu na viongozi wengine waliofanya kazi ngumu na ya ziada ya ujenzi wa chama ikiwa ni pamoja na kuleta wanachama wapya, michango nk..Tatizo hilo ni sugu sana....Kwamba utafanya kazi kwa moyo mmoja lakini one day someone might come and ruin it in a mtter of seconds.
Pili wengi ni maslahi binafsi na zaidi ya hapo ni wachache sana wenye nia njema na madhubuti kwa taifa na wananchi wake.
Maslahi binafsi yanachochewa na system ambayo ni vyema tukaiangalia upya..WANANCHI WAELEZWE KUWA NI PESA ZAO ZINAZOWALIPA RUZUKU HIVYO VYAMA...Hivyo basi ni muhimu kwa pesa hizo kuwa accountable in a good and mannerly ways.
Unaona huyo Kyara aliyekuwa mweka hazina na baadaye mwenyekiti wa Sauti ya Umma...Si aliona ruzuku na utamu wake hapo hazina so akaona njia pekee ya kuendeleza ufisadi kwa wananchi ni kuanzisha chama cha kuwagawa wananchi na kuendelea kula pesa zao bila HURUMA....Kuna wale ambao wana zile za "TUKOSE WOTE" Na hii inachangangiwa na perception ya uongozi ni nini hasa...Watu hawaoni umuhimu wa kuwatumikia wananchi.....Bali wanaona uongozi ni previledge ya kujinufaisha wao binafsi,makundi yao na familia zao..Kama siasa za vyama ndizo hizi..Na siasa hizi ndizo zinatupatia viongozi wa nchi..Then we need to look at this situation in a more critical and serious manners...Kuchagua rais kutoka kwenye makundi kulitupatia wanamtandao wenye interests za kundi hilo la mtandao.
Hivi wana jf tujiulize swali moja...Kama kusingekuwa na ruzuku..Then wangehama hama na kupoteza pesa za wananchi bure?
Migogoro inakuwa created ili mchezo huu mchafu wa kuwapumbaza wananchi uendelee....Kama tunataka vyama vya kweli basi na wajiendeshe kwa michango ya wanachama ili kama wakilikoroga walinywe wenyewe na si kumtegemea mtu anayeitwa Tendwa eti ili awagawawie pesa zetu wananchi kwa kigezo cha domokrasia la majungu,migogoro,fitna na chuki.
Sasa mwenye hoja unaweza kuona mfano halisi hapa....Kutokana na issue yote kuwa hivi..Sasa kuna wanaotaka tugeuze macho yetu na kuwaandama chadema....This is not a solution to our nation problems at this moment.
Ofcourse chadema bado hakijashika dola...Ila ninawataarifu wanachadema waongee na Mzee wa Kiraracha kwani yeye ni "Been there done that"
All over a sudden Mbowe hafai?!
Nakubaliana na wale wanaosema ni kawaida kuwa na kambi za uchaguzi..Hilo liko wazi..Lakini na mimi nasema...Kuna nguzo ambazo ni misingi ya uendeshaji wa chama chenye mwelekeo wa kidemokrasia..Kwa hiyo hayo makundi ama kambi hayawezi ku affect jambo la kimsingi ambalo chama kwa kupitia sera zake kina lizisimamia....Kama vile kusimamia rasilimali za wananchi vizuri.
Ndio maana unaona inapokuja kwenye kambi hizo hakuna mambo ya kitaifa ama yenye tija kwa wananchi yanazungumziwa..Sana sana utasikia ohoo kapitwa na wakati, ooh ana kashfa nyingi, ooh ana pesa...Who gives a darn?
We want a Govt for the people and not the other way round.
Hivyo nyie wanachadema muwe makini na siasa za ki republican ambapo wanaleta issue ambazo si muhimu wakati muhimu na hivyo kusababisha wananchi kuchaguwa mashetani badala ya viongozi wa watu...Watu wenye personal interests..Hata hayo makundi kama hayana nia nzuri ya kuwatumikia wananchi nayo pia hayana mpango...Watu wanataka sera...Ni kivipi tutaondokana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuutumia vyema utajiri wetu ambao mzee wa Rhuksa alidai mmeukalia.
NB:Naomba pia iwekwe wazi kama makundi hayo ndani ya chadema yana maslahi gani kwa Taifa,watawafanyia nini wananchi wao kama kundi ndani ya chadema? Nani humo chadema anaruhusu makundi? Huo si ndio mwanzo wa ufisadi kwa kuwa na interest groups within the party kama wanamtandao wa ccm?
Ni bora tu iwekwe wazi kuwa ni kambi za uchaguzi na si makundi ndani ya chadema yenye kutaka uenyekiti and possibly urahisi badala ya Urais....Ila tusisahau kuwa hata JK na yeye alikuwa na kambi..Sasa hiyo kambi nyie mliibatiza mtandao?
Ama mtandao ni kundi?