Gogomoka,
Thanks and most welcome to JF. Nadhani tuna matatizo kadhaa. Tunaweka picha kuwa sisi tulioko humu ndio kipimo sahihi cha matakwa ya Watanzania zaidi ya 40 Million. Kwa maoni yangu baada ya kuzunguka Tanzania nzima, Wilaya zote isipokuwa za Mkoa wa Kagera, hali halisi si hii inayoelekea kupigiwa debe na wachache hawa wanaoandika humu JF. Ni hatari sana kufanya generalization ya aina hii.
Watanzania niliowaona kwenye mikutano ya hadhara na kwenye makundi na mikutano ya ndani wanakuwa "electrified" kila wanapokutana na Mbowe. Ushahidi documented upo wazi, Mbowe has been and still is a crowd puller todate. Kwa tafsiri ya kawaida, kabla mtu hajafanya conclusions, crowds hizo maana yake nini. Swali hili linahitaji kujibiwa kabla ya generalizations kama hizi, ambazo kwa kigezo chochote kile ziko biased and for obvious reasons. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kuweka kumbukumbu sahihi kama Kiongozi wa Chadema mwenye kujua facts on the ground.
Pamoja na yote hayo, muhimu sana ni kuwa ugombea Urais, kwa msingi wowote ule, hauendi kwa ushabiki, mapenzi ya mtu binafsi bila Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria husika za nchi, Katiba na Taratibu ndani ya Chama husika. Hivyo, suala la Mbowe kugombea au kutogombea ni suala la Katiba ya Chadema, Taratibu za Ndani ya Chadema. Ikumbukwe kuwa Mbowe, au mtu yeyote ndani ya Chadema si mwamuzi peke yake bali ni vikao halali ndivyo vyenye kumteua Mgombea wa nafasi yeyote Udiwani, Ubunge na Urais. Dhana ya inayojengwa hapa ni ya udikteta wa Mbowe ambaye anajengwa kuwa "hakubaliki" lakini anajilazimisha. Nadhani dhana hii si sahihi na ikiachiwa itawapotosha watanzania bila sababu yeyote ya Msingi.