Mvutano wa kimaslahi wa zanzibar na Tanganyika ni wa kitoto sana.

Mvutano wa kimaslahi wa zanzibar na Tanganyika ni wa kitoto sana.

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Hivi majuzi tulishuhudia wabunge na baraza la wawakilishi Zanzibar likikosoa kauli ya Waziri wa sheria jamuhuri ya muungano wa Tanzania Prof Palamagamba Kibudi kuhusu tamko la raisi wa Jamuhuri dhidi ya usajili wa meli yakuwa rasisi wa JMT ana manlaka hiyo huku wabunge wa SMZ wakifikia hatua ya kumwita waziri wa sheria mpumbavu.

Leo nashangaa baada ya mbunge wa bunge la Wawakilishi kuuliza swali "je ni lini SMZ italipa deni la nje la dola elfu sabini "?
Ukatolewa ufafanuzi kwamba Zanzibar haipaswi kudaiwa madeni ya nje bali serikali ya JMT ndio yenye jukumu la kulipa deni hilo la nje ambalo Zanzbar ilikopa.
Wote wakashangilia swali hilo.

Swali ni je "Kumbe SMZ inaangalia mambo yanayoinufaisha Zanzibar tu kutoka SJMT na kuyapa kipaumbele na kuyapuuza mengine ambayo wanaona hayawanufaishi?

Huu ni utoto unaochezwa na watu wazima tena wasomi.
 
Na bado wanataka pasipoti ziwe na sura ya muungano yaani Mzee Karume aka Baba wa Taifa la Zanzibar awepo
 
Back
Top Bottom