Mvutano wa Tanzania na Malawi umemalizwa, makubaliano yasainiwa Dodoma

Mvutano wa Tanzania na Malawi umemalizwa, makubaliano yasainiwa Dodoma

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Tanzania na Malawi zimeamua kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kibiashara baada ya kumaliza mvutano wa kibiashara uliodumu kwa siku kadhaa, kufuatia marufuku ya uingizaji wa bidhaa zilizowekwa na Malawi Machi 13, 2025. Hatua hiyo imefikiwa kupitia mkutano wa pamoja wa mawaziri uliofanyika Mei 2, 2025, jijini Dodoma.

Mkutano huo ulifuatia mashauriano ya awali yaliyofanyika Aprili 24, kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Nancy Gladys Tembo. Mazungumzo hayo yaliwahusisha pia mawaziri wa kilimo, biashara na habari kutoka pande zote mbili.

Katika tamko la pamoja lililotolewa baada ya kikao hicho, nchi hizo mbili zilikubaliana kuchukua hatua za haraka kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kwa kuzingatia misingi ya ujirani mwema na sheria za kikanda na kimataifa. Viongozi wa pande zote waliweka bayana dhamira ya kushirikiana kwa karibu kutatua changamoto zilizopo katika biashara ya mipakani.

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuandaa taratibu za pamoja kuhusu viwango vya usalama wa chakula na mimea (Sanitary and Phytosanitary Standards), pamoja na kusaini Mkataba wa Biashara Rahisi (Simplified Trade Regime Agreement) kufikia Mei 30, 2025. Malawi pia iliahidi kurahisisha taratibu za uingizaji na usafirishaji wa bidhaa kati ya nchi hizo.

Waziri Kombo alisisitiza kuwa Tanzania na Malawi zina uhusiano wa kihistoria na wa kindugu, ambao unapaswa kuimarishwa kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili. "Tumeazimia kuutumia msingi huu kuimarisha zaidi ushirikiano wa kibiashara kwa manufaa ya wananchi wetu," alisema.

Kwa upande wake, Waziri Tembo aliishukuru Tanzania kwa kuondoa marufuku ya kuingiza mazao ya mimea kutoka Malawi, hatua aliyoiita ni ishara ya mshikamano wa kweli kati ya mataifa hayo mawili.

Hatua hizi zinatarajiwa kuleta utulivu na ufanisi zaidi katika biashara kati ya Tanzania na Malawi, na kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa pande zote mbili.

IMG_4732.jpeg


Pia, Soma
 
Back
Top Bottom