Jamaa mroho wa madaraka, maisha yamemchenga anakomaa akaibe hela za TLS. Kamati ya Rufaa ikaliona hilo, ikamkata
Ni aibu kwa Taasisi ya kisheria kuonyesha mfano mbaya sana wa kidemokrasia.
Hili ndilo tatizo la kuwa na mawakili wa Mwendokasi ambao hawakusoma masomo ya dini kule mashuleni.
Mandela alifungwa miaka 27 lakini ni kati ya karaisi bora kabisa Duniani.
Kwa sasa tulitegemea TLS ijivunie kuwa na Wakili wa aina ya Mwabukusi anayesimama na kuwaonyesha wanasiasa uovu na mapungufu yao kisheria na sio kuwasifia na kuwaogopa wezi.
Wanasiasa wa Afrika wanajiona kuwa Rasilimali zote ni mali zao na watoto wao. Wanatumia rasilimali za umma kufifisha uzalendo na haki za watu kwa manufaa yao na mawakala wao toka nje.
Kenya wanasiasa wamejificha baada ya vijana kuchachamaa kudai nchi yao iwe na haki sawa kwa wote katika mgawanyo wa Keki ya Taifa.
Kama nchi inauzwa halafu chama cha mawakili kipo ,kina maana gani kwa wananchi ?
Miswada ya kuwalinda wezi kama akina Bashe inapelekwa bungeni TLS imekaa kimya sasa hicho ni chama gani? Kimekuwa kama CWT na vyama mfu vya wafanyakazi.
Wanasiasa wanaogelea kwenye pesa za wizi huku kodi zikipandishwa.
Badala ya Mkuu wa nchi kusafiri na watumishi wa umma kama walimu madaktari , manesi, Mapolisi wa chini na magereza ili wakajifunze jinsi wenzao wanavyotoa huduma bora kwa watu wao badala yake anasafiri na kundi la kumpigia kampeni kwenye uchaguzi . Anajali cheo chake na sio taifa. TLS wapo kimya hawana hata ushauri kama taasisi ya kisheria.
Mpaka karne hii tunachaguliwa kiongozi mkubwa kama Naibu Waziri mkuu ambaye hayupo kikatiba na hakuna hata mwongozo na sifa za kumpata . Mtu anachaguliwa kama shukrani ya kuwezesha uuzwaji wa ardhi yenye madini kwa wageni. TLS imelala doro.
Waziri mkuu anapitishwa na Bunge kama msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali lakini cha ajabu analetwa Waziri mkuu kivuli na wa mchongo na kufanya kazi zisizo zake kisheria na Kikatiba. Waziri mkuu kivuli wa chama tawala anapewa jina lisilokiwepo katika katiba yetu la Naibu waziri mkuu. TLS wapo kimya hawakujitokeza hata kushauri.
Vyedha za umma zinatumika kuendesha ofisi za mchongo na vyeo vya madili na michongo huku kodi zikopanda juu na wafanyabiashara na Wafanyakazi na wakulima wakiumizwa na bei na tozo . TLS kimya.
TLS haina maana yoyote zaidi ya kuwa ni kichaka cha Watu kupata ofisi na posho za kujipendekeza kwa watawala na kupata teuzi na sifa binafsi.
TLS mmeonyesha mfano mbaya sana wa kulijenga Taifa lenye kuheshimu Demokrasia, Haki,usawa,uwajibikaji,utu,nidhamu kwa watumishi kwa umma na utawala unaozingatia sheria.
Tunapinga kwa nguvu zote kuona taasisi ya sheria inageuka kuwa Taasisi " Chawa."
Kama Mwabukusi hafai basi tuone kwenye sanduku la wapiga kura na sio kuengua jina lake. Hizo ni mbinu za kishetani za CCM zinazoligharimu taifa hili takatifu lisilofungamana na upande wa madhalimu .
Huyo mgombea anayedhani kuwa anakubalika na ana sifa njema zaidi ya Mwabukusi basi ni nafasi yake kuwaambia wajumbe sifa zake kwenye kampeni. Na hayo mapungufu ya Mshindani wake ndiyo faida na ushindi kwake.
TLS kitakua ni chombo cha mwisho kabisa kuzika Demokrasia na kuua kabisa ndoto ya watanzania kuwapata viongozi wazalendo.
Rushwa na matumizi mabaya ya fedha kimewafanya watumishi wengi wa Taasisi huru kuwa walamba viatu wa watwala wanaotumia fedha kuwap9 umma kamale fedha za mifukoni mwao kuwainamisha na kuwapigisha magoti na kuwafanya ombaomba.
Hata taasisi za dini nazo ni hivyo hivyo mabilioni ya Sadaka yanatoka lakini hazina tija kwa waumini badala yake wanalialia kuhusu misamaha ya Kodi wakati sadaka hawazitumii kufanya miradi na kuunda taasisi kubwa za kifedha zenye kuwezesha waimini wao kujitoa kwenye taasisi za kinyonyaji.
Yote ni sababu ya kuwa na viongozi machawa wa Wanasiasa hasa wa Chama Tawala kwa lengo la kupaka rangi nzuri uovu wao na kumtukuza shetani na fahari zake .