Mwabukusi afungua shauri la kikatiba, akata rufaa dhidi ya uamuzi wa kamati ya maadili ya mawakili

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Rais wa chama cha mawakili Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi, amefungua shauri la kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dodoma, kupinga uhalali wa shauri la kinidhamu linaloendelea dhidi yake mbele ya Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa niaba yake, jopo la mawakili wanaojitolea kumwakilisha Mwabukusi limefungua shauri hilo likitaka kuhoji uhalali wa kumfungulia shauri yeye binafsi, huku likieleza kuwa azimio linalohusika linatokana na masuala ya kitaasisi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa shauri hilo linatarajiwa kutajwa Oktoba 16, 2026.Aidha, jopo hilo limekata rufaa kupinga uamuzi wa Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili uliomnyima Mwabukusi fursa ya kuwasilisha rejoinder pamoja na muda wa kutosha wa kujiandaa na kutoa ufafanuzi baada ya wakili wake kujitoa katika shauri hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyoiliyochapishwa kwenye mtndaonwa facebook , hatua hizo zinakusudia kuhakikisha haki ya kusikilizwa inazingatiwa, huku rufaa hiyo ikisubiri kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine, Mwabukusi anatarajiwa kufika katika ofisi za ZCO, Dar es Salaam, Oktoba 15, 2026, baada ya kupokea wito kupitia simu. Jopo la mawakili wanaojitolea kumwakilisha limesema litamsindikiza kufika katika ofisi hizo kwa ajili ya kuitikia wito huo.

Kamati ya Maadili ya Mawakili yatofautishwa na TLS

Katika taarifa hiyo, jopo la mawakili limefafanua kuwa Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili ni chombo cha kisheria kilicho tofauti na Tanganyika Law Society (TLS), na kwamba haiko chini ya TLS wala haiendeshwi na chama hicho.

Jopo hilo limeongeza kuwa muundo wa kamati hiyo unahusisha watumishi wa Serikali na Mahakama, huku likieleza kuwa mawakili hawana ushiriki wa moja kwa moja katika uendeshaji wake kama ambavyo baadhi ya watu wanaweza kudhani.

Taarifa hiyo imehitimisha kwa kueleza kuwa jopo hilo litaendelea kutumia njia za kisheria zinazopatikana katika kutafuta haki na kuhakikisha taratibu za kisheria pamoja na haki ya kusikilizwa vinazingatiwa.
Chanzo :Boniface Mwabukusi
 
ok. sawa.

ila ni lazima aachie ngazi kwakua hana sifa tena kua rais wa TLS :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom