PreGE2025 Mwabukusi afunguka mazito atoa msimamo wa TLS''hatumuogopi mtu'' agusia no reform no election

PreGE2025 Mwabukusi afunguka mazito atoa msimamo wa TLS''hatumuogopi mtu'' agusia no reform no election

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Viongozi watawala wa CCM, bunge lake la cha kimoja na vyombo vyake dola vinatakiwa kupata elimu kama hii ya kutoka kwa rais wa TLS na pia wadau wengine wajitokeze kutoa elimu kama baba askofu Bagonza alipotoa muhadhara huu mwaka 2023

TOKA MAKTABA :

31 March 2023

MJADALA WA WAZI UCHAMBUZI MIAKA 30 TANGU VYAMA VINGI VIANZISHWE TANZANIA 1992

View: https://m.youtube.com/watch?v=M2LZAy8j-Aw

Askofu Benson Kalikawe Bangoza wa dayosisi ya Karagwe ya Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT ...

Katika mada aliyotoa tarehe
31 March 2023 yaani miaka miwili iliyopita (leo 2025) kwa hadhira ikiyofika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), iliyokuwa imeandaa mjadala wa miaka 30 ya demokrasia ya Tanzania katika Ukumbi wa Kisenga LAPF Conference Center, Jijini Dar es Salaam ....

Ujumbe mzito wenye ushahidi unaonesha kuwa Watawala wanasisitiza Amani kuliko Haki.. anafafanua askofu Bagonza,...

N.B mwaka 2025
Hivi kweli waTanzania tutegemee HAKI leo 2025 tukielekea uchaguzi wa 2025 huku tuna ushahidi usio na shaka wa Uchafuzi wa chaguzi za 2020, 2024 TAMISEMI ila tunapenda kujisaulisha kuwa kuna mabadiliko bila shindikizo la NO REFORMS NO ELECTION 2025 kufanyiwa kazi?

Hii ni akili kubwa
 
09 April 2025

MWABUKUSI AFUNGUKA MAZITO ATOA MSIMAMO WA TLS ''HATUMUOGOPI MTU'' AGUSIA NO REFORM NO ELECTION

View: https://m.youtube.com/watch?v=zFB3QFtmK3w
TLS ni mshauri wa umma people's power wakati mwanasheria mkuu ni mshauri wa serikali afafanua rais wa TLS mwanasheria msomi Boniface Mwabukusi...katibu wa Bunge naye anaishauri Bunge ...

Rais wa TLS amesema hayo wakati akifafanua umuhimu wa kusoma historia kwa mtazamo chanya .... hili la kusema No Reforms No Election ni uasi, wakati tunaweza kuzungumza tukarekebisha kabla ya kufikia hatua zingine zenye madhara historia inavyoeleza kwa mifano ya watu kufa Kenya ... Tanzania tunauwezo wa kuepuka hilo maana tuna nafasi...

Katiba ya 1977 ilipitishwa na watu wachache kwa muda mfupi, na hili suala la mabadiliko ya katiba kuwa muda hautoshi ni hoja mufulisi...

Lazima watawala waje mezani muda upo na nchi siyo yenu watawala ...

Jukwaa la Katiba limeshaung mkono
 
Wananchi wamezinduka 2025, waandishi wa habari na media wanajifanya hamnazo kama vile mazinzigira kuelekea 2025 ya uchaguzi mkuu yatakuwa ya amani, haki na huru

Media kama vituo vya Redio, televisheni hawafanyi mijadala ya wazi kuelezea hali halisi ilivyo ya ugandamizaji haki mchakato mzima wa uchaguzi 2025
Hata wakikaa kimya mawe yatapiga mayowe
 
1744214497772.jpeg
 
TOKA MAKTABA :

09 January 2020
JAJI NSEKELA AJITETEA - "SISI SIO MATAPELI, WAMELETA BAADA YA RAIS KULETA"

1744214654722.jpeg

Picha maktaba : Kamishina wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini Tanzania Jaji mstaafu Harold Nsekela
 
Ni Muda wa kuwasha moto kote - ukondoo nchi hii sasa basi.

Hii hoja ni ya kitaifa- uchaguzi usio na thamani ya kura yako wa nini?
 
Sikiliza hoja mujarabu kutoka kwa Rais wa TLS Adv. Mwabukusi.
 
Back
Top Bottom