Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Anyisile Mwabukusi, ametangaza kupokea wito wa Jeshi la Polisi na kwamba kesho, tarehe 15 Oktoba 2026 asubuhi, ataripoti katika Ofisi za Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO), akisindikizwa na Jopo Zito la Mawakili Waliojitolea Kumuwakilisha.
Taarifa hiyo rasmi kwa umma na mawakili nchini inakuja katikati ya vuguvugu zito la kisheria, ambapo Jopo la Mawakili wa Mwabukusi limefungua Shauri la Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kuhoji uhalali wa kugeuza Maazimio ya Kitaasisi ya TLS kuwa mashitaka ya nidhamu na kimaadili ya mtu binafsi dhidi ya Rais huyo wa TLS.
Pamoja na hatua hiyo ya Dodoma, Jopo hilo limekata rufaa kupinga uamuzi wa Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili uliomnyima Mwabukusi fursa na muda wa kutosha wa kujiandaa na kutoa maelezo ya ufafanuzi (rejoinder) baada ya wakili wake kujitoa, likisisitiza kuwa hatua hiyo inakiuka haki ya msingi ya kusikilizwa.
"Nilipokea Wito kufika kwa ZCO, Dar es Salaam. Hivyo Jopo la Mawakili wanaojitolea kuniwakilisha kesho, tarehe 15 Oktoba 2026 asubuhi, litanisindikiza kufika katika ofisi hizo... Jopo limefungua shauri la kikatiba Mahakama Kuu Dodoma kuhoji uhalali wa shauri dhidi yangu kama wakili binafsi ilhali Azimio linatokana na masuala ya taasisi. Umma uelewe kuwa Kamati ya Maadili si chombo cha TLS; muundo wake unahusisha watumishi wa Serikali na Mahakama," ilieleza taarifa hiyo rasmi ya Wakili Mwabukusi.
Aidha, Mwabukusi ametoa ufafanuzi wa kisheria kuwa Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili ni chombo kinachoundwa na watumishi wa Serikali na Mahakama na wala si chombo kilicho chini ya TLS, huku akiahidi kuwa jopo lake litaendelea kutumia nafuu zote za kisheria kutetea haki na misingi ya sheria.