Mwabukusi: CCM ishauri Serikali ifute kesi zote zenye viashiria vya kisiasa kama hatua ya kwanza ya maridhiano

Mwabukusi: CCM ishauri Serikali ifute kesi zote zenye viashiria vya kisiasa kama hatua ya kwanza ya maridhiano

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniphace Mwabukusi, akizungumza leo Septemba 8, 2026, kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa nchini ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ameeleza kuwa kutoridhishwa kwa wananchi na hali ya kidemokrasia na kisiasa ndiko kulikosababisha changamoto za hivi karibuni, na si masuala ya uchaguzi pekee.

Wakili Mwabukusi amebainisha kuwa nchi inakabiliwa na kulegalega kwa vyombo vyenye dhamana, ikiwemo Bunge kushindwa kuisimamia na kuishauri Serikali ipasavyo kwa kuonekana kuwakilisha matakwa ya vyama vya siasa badala ya wananchi, huku matukio ya migogoro ya ardhi, utekaji na kupotea kwa wakosoaji yakizidi kushusha matumaini ya jamii.

Akitolea mfano mataifa kama Sierra Leone, Kenya, Ghana na Zanzibar, amependekeza kuanzishwa kwa Tume ya Ukweli (Truth Commission) ili kuponya taifa na kuweka mazingira ya uwajibikaji badala ya kulenga adhabu za kisasi, huku akiitaka Serikali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua hatua za kiutashi kwa kufuta kesi zote zenye viashiria vya kisiasa ili kufungua fursa ya mashauriano ya kitaifa.

"Kwa hiyo lazima tuangalie, na anayeweza kuongoza hili, anayetakiwa kuchukua hatua stahiki ni Chama Cha Mapinduzi kielekeze serikali hatua ya kwanza ifute kesi zote zenye viashiria vya kisiasa, hiyo ndio iwe hatua ya kwanza. CCM ili wanaliweza, liko ndani ya uwezo wao, watoe maelekezo sio kwa kuingilia mahakama, kwa utaratibu wa kisheria upo, kwa sababu CCM ndio ina serikali iseme tunataka kulileta taifa pamoja"

 
Back
Top Bottom