Mwabukusi, Dkt Slaa, Mdude, Sauti ya Watanzania waongezewe Ulinzi

Mwabukusi, Dkt Slaa, Mdude, Sauti ya Watanzania waongezewe Ulinzi

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Huu ni wito wa tahadhali kabla ya hatari. Beberu akiuita "security alert."



Hali ya hewa imebadika, matumaini ya watanzania yaliyokuwa yamefifia mno, hatimaye ghafla yamefufuka.

Mungu atupe nini Ya-Rabi sisi?

Zama zile zilizokuwa zimepotea, ghafla zimerejea. Tena si kitoto, bali kwa mwelekeo ulio mwema zaidi. Tabasamu na hata morali ya washirika, ni zile zenye kumtetemesha
adui akatambua wazi kuwa kujifanya kiziwi, siyo dili tena!

"Kwamba kwa mara nyingine, zile enzi zetu za M*ndonga mtu kazi, kumdunda mtu kama ngoma zimerejea?" Enzi zile za kheri za kuukataa utwana. Enzi za kina Kinjekitile, Mkwawa, Mtikila na kina Nyerere!

Nani alisema mtanzania ni mwoga (coward)?

"Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi"

Ya nini kuandikia mate? Waoga wako hapa:

"Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu"

"Utukufu na sifa vyote vimrejee yeye aliyejuu. Mwenye kutupenda mno sisi kama waja wake. Aliyetukumbuka hatimaye na kutotoa katika lindi la kiza"

Hata hivyo si ajabu jambo jema kutopokelewa vyema na wote. Hutokea wakati yakazuka makundi na hali ikawa hata siyo.

Hala hala mti na macho:

"Dkt. Slaa, Mwabukusi, Mdude na vigogo Sauti ya Watanzania lulu ya leo ya watanzania, ulinzi uimarishwe."

Posts #2, 3, 4 zinakazia hitaji hili la dharura mno kwa watu lulu kama hawa.

Mungu uwalinde majemedali wetu Mwabukusi, DKt. Slaa na Mdude. Ukawapatie afya njema na maisha marefu. Ukawawezeshe kuiona Tanzania njema ya ndoto zetu sasa.

Mungu ibariki "Sauti ya Watanzania."
 
Ipo tofauti ya kimawazo na mtizamo:

Natambua umakini wake
Natambua uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, kuchambua na kushawishi ili ukubaliane naye
Natambua uthubutu wake linapikuja suala la haki na kuipigania Tanganyika ...

1. HIzi ni sifa zake ambazo kwa hakika itakuwa ni wivu uliopitiliza kwa awaye yote kutotaka kuzitambua au kukiri hadharani.

"Mnyonge, mnyongeni, haki yake mpeni."

Yaani kuna wakati anaongea yeye wanatetemeka wengine

2. Kauli hii siyo sahihi. Labda kama una maana wanaotetemeka ni CCM na vibaraka zao.

Kwa hakika wale madalali wa DP World na vibaraka zao wanatetemeka mno wakisikia jina lake likitajwa. Hali wanafurahi mno wakisikia hata dalili tu, za kutaka kujaribu kumbagaza kwa namma yoyote. Kwa hakika hapo hata maokoto yanaweza yakahusika.

Nia yake ni thabiti na uhalisia wake unauona kabisa kwenye matamshi yake na body language yake!

3. Hili ni sahihi ni la muhimu mno kwetu (sote) bila kujali vyama tunapokabiliana na CCM na vibaraka zao. Adui zetu wanapaswa kuliona hilo kwa uthabiti wake na bila ya kuwapo tashwishi yoyote.

Kwamba CCM wakisikia tunataka katiba mpya sasa, wajue tuna maanisha hivyo na si vinginevyo!

"Mtu akisema anachukia rushwa, tukimwangalia usoni, tulione hilo!" -- JKN.

QUOTE="Mshana Jr, post: 48065520, member: 98741"]

Lakini amakinike mno na mfumo maana hauishiwi mbinu za kukwamisha ama kufelisha mambo! [/quote]

4. Haya ni mawazo yako ambapo kila mtu anaweza kuwa na yake. Kwamba ni ushauri wako wa nia njema kwa mtazamo wako, kwa Mwabukusi?

Hiyo kwa hakika ni haki yako kama ilivyo kwa mtu yeyote. Miye naweza kuwa nao wangu pia hata kwako, Retired au kwa mwingine awaye yote.

"Kumbuka kuna watu wengi tu (hata humu JF) wanaamini wanazo shauri bora zaidi kwa kina Natenyahu, HAMAS, Museveni, PK, Obama na hata kina Biden huko."

Yote ya kheri tu.

Ni nature ya binadamu kudhani anaweza kuwa na mawazo mazuri zaidi kuliko wengine. Lakini haina maana kuwa ndiyo ulio usahihi au hata ulio pekee. Hii ikizingatiwa kwa ukamili wake kuwa hakuna ambaye ni "supernatural" baina yetu.

1664543999224~2.jpg


Kibonzo hapo juu kinajielekeza zaidi.

Nia yake ni thabiti na uhalisia wake unauona kabisa kwenye matamshi yake na body language yake!

5. Hili halina ubishi kwa maana hata misahafu inasema, tutawatambua manabii (wakiwamo wa uongo) kwa matendo yao.

Lakini amakinike mno na mfumo maana hauishiwi mbinu za kukwamisha ama kufelisha mambo!

6. Hili angalizo lako hapa lina ukakasi. Linakuwa je kutoka kwetu kwenda kwa wapambanaji waliodhamiria wenye kuhitaji mkubwa wa kupewa moyo na kutiwa shime zaidi?

Maangalizo ya hivi kama mlengwa hajakuomba, huwa ni ya kutulia shaka sana. Haya huwa ni ya adui mwenye lengo la kuwajengea hofu wale wenye nia ya kumkabili.

pessimism-is-an-excuse-for-not-102548-1.jpg


Tutaogopa kuthubutu hadi lini, kwa sababu ya maangalizo tu kama yale uchwara ya vipigo vya mbwa koko?

Juzi OCD wa Mbeya alimuingiza mtegoni kizembe sana..

Kulikoni kumsemea Hivi OCD? Tangu lini watu hao wamekuwa wema au hata kuwa fair kwa nani?

Unajuaje ulikuwa ni mtego au hata kuwa wa kizembe kama unavyosema?

"Si kila mtu anapambana na hali yake?"

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

Wa hivyo watakuwapo wengi tu. Hao si hukanwa hadharani na bila kuchelewa?

Hudhani kuchelewa kuwakana huku ni chanzo cha mitafaruku isiyokuwa na tija wala sababu?

Alimwambia mkutano wake umezuiwa kwakuwa CHADEMA wameenda KULALAMIKA polisi kwamba nyimbo zao CHADEMA zinapigwa kwenye mkutano wa wakili msomi Mwabukusi.. Mwabukusi bila hata kutafakari hiyo kauli akasitisha mkutano wake na kwa namna fulani akailaumu CHADEMA

Kwenye ukombozi potoshaji zitakuwepo nyingi. Watakuja huyu na yule. Hata misahafu inasema kutakuwa na manabii wa uongo.

Wapo watajinasibu hata kwa majina yetu kupotosha hili na lile:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Kweli tugombane kwa sababu OCD kapotosha nini?
 
QUOTE="Mshana Jr, post: 48065520, member: 98741"]

Alimwambia mkutano wake umezuiwa kwakuwa CHADEMA wameenda KULALAMIKA polisi kwamba nyimbo zao CHADEMA zinapigwa kwenye mkutano wa wakili msomi Mwabukusi.. Mwabukusi bila hata kutafakari hiyo kauli akasitisha mkutano wake na kwa namna fulani akailaumu CHADEMA[/quote]

1. Mkuu, huku ni kumkosea sana wakili wa mahakama ya rufaa, wakili msomi, bwana Mwabukusi.

"Kulikoni kudhani hakutafakari?"

Hizi namna "fulani za kuilaumu Chadema" ni zipi?

Hivi kweli wakili msomi Mwabukusi alishindwa kuuona mtego hapo? Ni lini polisi wamekuwa wema kiasi hicho cha kuchukua hatua za haraka walipopata malalamiko ya CHADEMA?

2. Kutaka kumzungumzia Mwabukusi wakili msomi na polisi haiwezi kuwa kwenye udadavuzi wako huu na eti huku tuache hata kukustua "offside" hiyo ya wazi, ndugu.

"Mwabukusi anapambana nao hao watu kila siku na pia mahakamani. Huyo ana kitanzi cha kifo shingoni kama mafwedhuli hao wakiweza kukithibitisha ambacho walishapenda kumtuhumu nacho

Itoshe kukufahamisha huyo siyo level yetu: yaani mimi ay wewe!

Zingatia:

"Mwabukusi alisema alichoambiwa na polisi.
Kosa lake ni kusema alichokuwa ameambiwa na polisi?"

Kuna kesi ngapi polisi za uonevu, za kubambikwa za kusingiziwa za viongozi na wanachama wa CHADEMA kila mahali Tanganyika ambazo zinasuasua mpaka kesho?

3. Maonezi ya polisi kwa vyama, watu, nk, nani asiye yajua? Zingatia hata kuna tume ya haki jinai kazini.

"Hilo hata CCM, mama Abduli, polisi nk na wote kabisa wenye akili zao kichwani wanalijua?

Wapi umeona kuwa Mwabukusi ana mkono au kuufurahia, kushangilia, au hata kuushadadia udhwalimu wa aina hizo, popote?

Hekima ya CHADEMA iliepusha mfarakano mkubwa sana!


4. Wewe hujui kuwa tuko vitani na mbinu zote overt na covert, madui huzitumia?

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Nini kisichoeleweka hapo ndugu? Haya tumekuwa tukisema sana tu;

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

CHADEMA kabla ya kujibu kwa haraka tuhuma hizo walichukua muda kujiridhisha kwamba hizo taarifa zilikuwa za uzushi, uongo na upotoshaji mkubwa..

5. Kutokujibu kwa haraka lilikuwa ni kosa kubwa na itaendelea kuwa hivyo kama inawalea wasio na dhamana ya kukisemea chama.

Lissu rudini ubaoni, Majukwaani hakutamng'oa CCM

Kumkana hadharani na bila kuchelewa huyo OCD mzushi, ulikuwa wajibu wao sahihi nambari one!
hawa wa mitandaoni[/URL]

alimtafuta Mwabukusi na kumwambia hali halisi kwamba hakuna mahali popote CHADEMA ilifanya hivyo

6. Ingependeza zaidi kama wangesonga mbele na agenda ya mapatano kabisa.

Kwetu wananchi la muhimu zaidi
lilikuwa ni la mapatano wala si huyo mzushi. Wazushi watakuwapo wengi tu.

Wakili msomi Mwabukusi ni mnyenyekevu na mkweli sana baada ya taarifa hiyo aliita waandishi wa habari na kuwapa mrejesho huo huku akiapa kumburuza kortini OCD

7. Wanyenyekevu ni watu wenye kutaka mapatano. Si watu wa visasi. Si wenye kujihesabia haki. Si wajanja wajanja. Si watu wa hila. Nk. nk.

Kwa kiswahili wakiitwa waungwana.

Kwamba kumbe hata mnajua yeye alikuwa ni kama transmitter tu? Akizichukua na kuzifanyia kazi hadharani na bila kuchelewa taarifa zote kama alivyozipata?

Zingatia alipopata ya polisi alifanyia kazi mara moja kama ilivyokuja. Akawaambia watu lililojiri na kuahirisha mkutano. Hekima nyingine kubwa tu.

Sasa hadi hapo Ya-Rabi, iko shida gani na nani, na Mwabukusi wapi?
 
Mwabukusi amakinike na timu aliyonayo!

1. Kulikoni kutokumakinika wewe ili ufanye vizuri zaidi? Hudhani ushauri wako huu kufanana na Tanzania kujaribu kuishauri Japan namna ya njema zaidi ya kutengeneza magari vizuri?

Au ni Ile kujidanganya kuwa kwenye miti hakuna wajenzi?

Hivi umejiuliza kama Mwabukusi anahitaji hata ushauri lakini? Achilia mbali wa kwako?

"Kwa mtaji huu huoni unakaribia kuanza kujipa kazi ya kumshauri hata Mungu?"

Hiiiiiii bagosha!

Ama kweli mmevurugwa siyo kwa kiwango hiki. Tafuteni suluhu. Ujanja ujanja haulipi!

Kina Mwabukusi hawana ugomvi na mtu. Kina Mwabukusi wana agenda za wananchi mkononi.

"Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono"

Sina mashaka na Mdude..

2. Kwani wewe nani mkuu? Hata Yesu kumbuka watu walimshangaa. Huyu mtoto wa seremala vipi? Sembuse wewe ndugu?

Hata kama huna mashaka naye au hata kama ungekuwa nayo, so what ndugu? Hayo si ni yako mkuu?

Kwani Mwabukusi kakwambia anatafuta wachumba na hivyo anahitaji mawazo ya watu kuhusu watu? Ya kuwa angependezwa mno na usiokuwa na mashaka nao ndugu?

Tunaelekea wapi huku ndugu zangu? Kuna katiba mpya huku kweli? Au ni usanii tu?

Kama tuko pro people fitna zote hizi zisizokuwa na msingi ni za nini?

Lakini kwa Dr. Slaa kuna ukungu.. Ukimsikiliza kwa makini katikati ya matamshi yake kuna vitu haviko sawa sana!

3. Huku ni kujihesabia haki ambako hata misahafu inakataza ndugu yangu.

Kumwona mtu, kumhisu au kumfikiria mtu alivyo na kwenda kumwanika hadharani ati kwamba ni maoni yako binafsi tu si haki hata kidogo.

Hata kama aliwahi kujikwaa au hata kutukwaza, misahafu si inasema kusamehe ni 7 x 70? Au wenzetu 7 x 71 yenu imeshafika?

Looh! Hata Yesu alikuja kwa wakosaji si kwa malaika labda kama nyie.

F7iw4TwXAAAZ6NP.jpeg


Kwamba kumbe na chuki zenu mnataka kumgawia na nani mwingine? Si mkae nazo wenyewe huko muone kama ni mali?

Kwa mfano alipopata wasaa wa kuwasalimia Wanambeya waliokusanyika nyumbani kwa Mwabukusi alitoa mfano wa kushangaza kwamba bunge lisiwe la chama kimoja tu bali kuwe walau na uwiano! Akatoa mfano CCM ikiwa na wabunge 200 basi wengine wawe na wabunge 100

4. Mkuu haya ni mawazo yako. Wengine tunaona Slaa aliongea vizuri mno. Labda kuliko hata siku zingine zote. Sasa hii yenu tuiite husuda?

"Wana Mbeya wako pale hawajaondoka. Walimfurahia Dk. Slaa na wakamshangilia."

Tunajua CCM, polisi na vibaraka wao walichukia mno. Wewe kama unaona ungeweza kuongea wakafurahi zaidi? Tatizo liko wapi ndugu?

Si uende pale upeleke huo ujumbe halafu ukipenda utuletee mrejesho?

What a grave mistake! Hapo alijidhihiri anasimamia nini na anaamini nini... Kwamba bado ana imani kubwa na CCM kuliko vyama vingine! Katika nyakati hizi za harakati kubwa za kuiondoa CCM madarakani, mpiganaji mpambanaji kamwe hawezi kuongea kitu kama hicho! Sitaki kumuita Dr. Slaa pandikizi.. Lakini nyayo zake zimechafuka!

5. Ha haa ha 🤣🤣 Kwamba wewe sasa umekuwa Jaji. Mwanzo ulikuwa prosecutor na Shahidi? Kwamba hukumu yako sasa ni ya haki. Hii siyo janja ya nyani kula mahindi mabichi tu ndugu?

Hamna kitu hapa ndugu yangu.

Kujaribu kumbagaza Dk. Slaa wewe, ni sawa na Mwaipopo na Shivji tu.

Hapa nikurejeshe kule kwenye matunguli yetu na uganga wa kienyeji dongobeshi ikungu lya bashashi ndugu yangu. Haya mengine ni level nyingine!

Kuhusu Buberwa kila nikimuangalia yuko moderate sana! Na mara nyingi sauti yake haiakisi uhai na uhalisia..!
Huu ni mtazamo wangu binafsi

6. Haha ha ha. 🤣🤣 Kwani macho yako yana upako ndugu? Au wewe ni supernatural yaani Mungu, malaika, jini au shweitani?

Ustaarabu si ni kukaa na mtazamo wako ndugu? Kila mtu ana wake.

Kila mtu akianza kutupa mitazamo yake kukuhusu wewe na wengine wakakubatiza na ushoga humo, kwani utasema je hapo ndugu?

HITIMISHO

Inasikitisha kuwa bandiko lako refu linajadili watu (Mwabukusi na Dk. Slaa) badala ya kujadili hoja zao.

Cha kusikitisha zaidi Kwa maoni yangu ni kuwa umeshindwa kujielekeza kwenye kutafuta mapatano ukajikita kwenye chokochoko za kitoto. Yaani kuleta mafarakano kati ya chama na hawa ndugu au hawa ndugu baina yao.

Jitihada hizo ni dua la kuku kwa sababu agenda za hawa ni agenda za watu si zao. Agenda za watu ni agenda za Mungu.

Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono

Hazipo agenda za ruzuku Wala ubunge hapa.

Katika katiba mpya ni nia ya wananchi kufuta ruzuku na pia kuweka stahiki za wabunge kuwa sawa na za watanzania wengine.

Tuziacheni siasa za maji taka kuwachafua hawa ndugu. Tunajua udhwalimu wote dhidi yao utashindwa na wabaya wao wataishia kuvuna mafurushi ya miba.

Mungu mbariki Mwabukusi. Mungu mbariki Dk. Slaa. Mungu mbariki Mdude.

Mungu ibariki Sauti ya Watanzania.

Aluta continua!
 
Nawàheshimu sana hawa watu.
Na wakiunda chama cha upinzani watashinda.
Nitawatafuta niongee nao mambo ya msingi.
Ambayo siwezi kuyaongelea hadharani.
Wenye hamu ya lile, wanifuate inbo,

Ni Bora tuwaachie watu wa mjini waongee.

Hakuna haja ya vyama vingine mkuu. Upako unapatikana kote hata ukisali kwa Kakobe kesho Kwa Mwamposa, TEC su Kwa Rashid.

Utitiri wa vyama si tija. Tungesukuma mapatano badala ya mafarakano.

Bila kudhamiria ni sawa na kucheza "Gombe Sugu" tu.
 
Kama wanataka kufanikiwa katika upinzani wao ni lazima wawe tofauti kidogo kwanza wakubali kukosolewa. Pili wakubali kuwa hata ccm kuna mazuri wanafanya hivyo basi wanapaswa kuwapongeza pale wanaopoana jambo zuri limefanywa na serikali ya ccm.

Tatu wasiwe wanapinga kila kitu ambacho serikali ya ccm inafanya hasa issue za kimaendeleo mfano ujezi wa reli, ununuzi wa ndege nk. badala yake wawe wanatoa ushauri nini kifanyike ili kuboresha.

Nne wasiwe wanaonesha kufurahia hadharani pale mali za umma zinapokamatwa mfano ndege, hii itawafanya waonekane wapinzani wastaarabu. Tano wasijikite kupambana na mtu mmoja mmoja ndani ya ccm kwani kuna siku huyo mtu anaweza asiwepo bali ccm itaendelea kuwepo na kutawala, wanapaswa kupambana na mfumo. Sita wawe wanajikita kuzungumzia maswala ya wananchi zaidi kuliko mambo yao binafsi ya chama, mfano wanapaswa kuilazimisha serikqli kukamilisha miradi kwa wakati, mfano miradi ya maji, umeme, vituo vya afya nk.

Saba wawe wanaeneza sera zao kwa wananchi kwamba wao wakipata dola watafanya nini na sio kuishia kukosoa serikali halafu hawasemi wao watafanya nini endapo watapata dola.

Nane wawe tayari kufanya kazi na mtu yeyote mzalendo wasichague anatoka pande gani nchii hii ni yetu sote.

Tisa waweke uchama pembeni, Tanzania na utaifa ndio iwe kipaumbele chao.

Kumi wajiepushe na lugha za kejeli, ubaguzi na zenye ukakasi, watanzania walio wengi ni wastaarabu na wamejingewa misingi ya kuheshimiana mkubwa kwa mdogo.

Mwisho waheshimu kila binadamu aliyopo chama chochote na wasione kama wao ndio wenye akili na kuanza kudharau kila mtu aliye kwenye chama kingine, wakumbuke siasa haina adui wa kudumu hivyo basi wanapaswa wawe na chama ambacho mfuasi wa chama chochote anaweza jiunga bila kujiona mgeni na anaweza ondoka bila kusimagwa na kuitwa majina kama msaliti.
 
Kama wanataka kufanikiwa katika upinzani wao ni lazima wawe tofauti kidogo kwanza wakubali kukosolewa. Pili wakubali kuwa hata ccm kuna mazuri wanafanya hivyo basi wanapaswa kuwapongeza pale wanaopoana jambo zuri limefanywa na serikali ya ccm.

Kukosolewa. Kukosolewa. Kukosolewa. Nimemwita huyo x 3.

Huo ni mfupa mchungu mno kwa wale wengine. Ndiyo maana matumaini ya watanzania yalikuwa yamefifia mno.

Tatu wasiwe wanapinga kila kitu ambacho serikali ya ccm inafanya hasa issue za kimaendeleo mfano ujezi wa reli, ununuzi wa ndege nk. badala yake wawe wanatoa ushauri nini kifanyike ili kuboresha.

Kupinga kila kitu ni wenda wazimu.

Hata shweitani ana yake si haba.

Mwanamke mzuri hakosi kasoro.

Nne wasiwe wanaonesha kufurahia hadharani pale mali za umma zinapokamatwa mfano ndege, hii itawafanya waonekane wapinzani wastaarabu.

Ninakazia!

Hatuwezi kutupa mtoto na maji yake ya kuogea.

Taifa mbele. Wananchi kwanza. Wenye nchi wananchi.

Mtoto akiunyea mkono, haukatwi!

Hasira za mkizi kulikoni?!

Tano wasijikite kupambana na mtu mmoja mmoja ndani ya ccm kwani kuna siku huyo mtu anaweza asiwepo bali ccm itaendelea kuwepo na kutawala, wanapaswa kupambana na mfumo. Sita wawe wanajikita kuzungumzia maswala ya wananchi zaidi kuliko mambo yao binafsi ya chama, mfano wanapaswa kuilazimisha serikqli kukamilisha miradi kwa wakati, mfano miradi ya maji, umeme, vituo vya afya nk.

Uwajibikaji. Uwajibikaji. Uwajibikaji. Nimemwita x 3.

Ninakazia.

Vipaumbele. Vipaumbele. Vipaumbele. Naye nimemwita x 3

Ninakazia.

Miradi ni kwa wakati vinginevyo ni wenda wazimu.

Kutokuwepo kwa rafiki wala adui wa kudumu ndiyo msingi mzima Bali agenda.

Watu watakuja na kwenda kiroho safi.

Saba wawe wanaeneza sera zao kwa wananchi kwamba wao wakipata dola watafanya nini na sio kuishia kukosoa serikali halafu hawasemi wao watafanya nini endapo watapata dola.

Ninakazia.

Nane wawe tayari kufanya kazi na mtu yeyote mzalendo wasichague anatoka pande gani nchii hii ni yetu sote.

Ninakazia.

Tisa waweke uchama pembeni, Tanzania na utaifa ndio iwe kipaumbele chao.

Ninakazia.


Kumi wajiepushe na lugha za kejeli, ubaguzi na zenye ukakasi, watanzania walio wengi ni wastaarabu na wamejingewa misingi ya kuheshimiana mkubwa kwa mdogo.

Ninakazia.

DKt. Slaa ni mzamivu wa shule na hekima.

Hii timu inasikiliza ushauri. Inabeba agenda za wananchi.

Hawa si wahuni!

Kwa hakika wanayastahili maua yao. Ama kwa hakika wametutoa kimasomaso.

Mwisho waheshimu kila binadamu aliyopo chama chochote na wasione kama wao ndio wenye akili na kuanza kudharau kila mtu aliye kwenye chama kingine, wakumbuke siasa haina adui wa kudumu hivyo basi wanapaswa wawe na chama ambacho mfuasi wa chama chochote anaweza jiunga bila kujiona mgeni na anaweza ondoka bila kusimagwa na kuitwa majina kama msaliti.

Ninakazia.

Ndiyo maana wao ni wa mapatano si mafarakano. Agenda za wananchi zikiwa kipaimbele pekee. Agenda binafsi tupa kule.

Tuko wote mkuu.

Aluta continua!
 
BAK Mwabukusi anawindwa ashughulikiwe mwezi huu. DP WORLD wanaingia bandarini 01 Nov 2023.

Ama kweli tumevurugwa:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Wapi wenye kuililia CHADEMA machozi kuliko Lissu wakilia machozi ya mamba.

Hatudanganyiki!

Kulikoni kumpenda mwanao kuliko mama yake?

Wananchi kwanza. Taifa kwanza.

Agenda za chama Viz a viz za wananchi? Za wananchi zina tamalaki.

Tuwekezeni kwenye mapatano. Si mafarakano. Tunajenga nyumba moja.

U CCM, CHADEMA, ACT nk inakuja baada ya I Tanzania.

Habari ndiyo hiyo.
 
 

Hoja haipingwi kwa rungu ndugu.

Yamewakuta kina Biko, Mahlangu, Mandela, Tutu, Hani na wengi wengine Afrika Kusini huko. Majina yao yameandikwa kwenye wino wa dhahabu kama mashujaa.

"Ni heri kuteswa na kufa ukipigania ukombozi kuliko kufa kwa Malaria." --Lwaitama.
 
Sakata la Bandari na hifadhi za misitu na mbuga za wanyama ipo siku Watanzania watalia kama mbwa, bidii na uzalendo wa Hawa watu inaonekana ni mzaha Watanganyika watambue wazanzibar wana agenda mbaya sana kupitia huyu Bibi yao. Fitina yao ipo rohoni toka uchaguzi wa 2005
 
Sakata la Bandari na hifadhi za misitu na mbuga za wanyama ipo siku Watanzania watalia kama mbwa, bidii na uzalendo wa Hawa watu inaonekana ni mzaha Watanganyika watambue wazanzibar wana agenda mbaya sana kupitia huyu Bibi yao. Fitina yao ipo rohoni toka uchaguzi wa 2005

Muda ni mwalimu mzuri sana. Kamwe haujawahi kushindwa.

Wanaodhoofisha jitihada za wananchi wazalendo hawa na hata kuwaombea dua mbaya:

F7iw4TwXAAAZ6NP.jpeg


Kiroho safi, kuwasamehe, tutawasamehe. Lakini hatutasahau.

"Walikuwapo kina Buthelezi, Sithole, Muzorewa na wengi wengine wa namna pia."

Aluta continua!
 
Back
Top Bottom