Huu ni wito wa tahadhali kabla ya hatari. Beberu akiuita "security alert."
Your browser is not able to display this video.
Hali ya hewa imebadika, matumaini ya watanzania yaliyokuwa yamefifia mno, hatimaye ghafla yamefufuka.
Mungu atupe nini Ya-Rabi sisi?
Zama zile zilizokuwa zimepotea, ghafla zimerejea. Tena si kitoto, bali kwa mwelekeo ulio mwema zaidi. Tabasamu na hata morali ya washirika, ni zile zenye kumtetemesha
adui akatambua wazi kuwa kujifanya kiziwi, siyo dili tena!
"Kwamba kwa mara nyingine, zile enzi zetu za M*ndonga mtu kazi, kumdunda mtu kama ngoma zimerejea?" Enzi zile za kheri za kuukataa utwana. Enzi za kina Kinjekitile, Mkwawa, Mtikila na kina Nyerere!
"Utukufu na sifa vyote vimrejee yeye aliyejuu. Mwenye kutupenda mno sisi kama waja wake. Aliyetukumbuka hatimaye na kutotoa katika lindi la kiza"
Hata hivyo si ajabu jambo jema kutopokelewa vyema na wote. Hutokea wakati yakazuka makundi na hali ikawa hata siyo.
Hala hala mti na macho:
"Dkt. Slaa, Mwabukusi, Mdude na vigogo Sauti ya Watanzania lulu ya leo ya watanzania, ulinzi uimarishwe."
Posts #2, 3, 4 zinakazia hitaji hili la dharura mno kwa watu lulu kama hawa.
Mungu uwalinde majemedali wetu Mwabukusi, DKt. Slaa na Mdude. Ukawapatie afya njema na maisha marefu. Ukawawezeshe kuiona Tanzania njema ya ndoto zetu sasa.
Natambua umakini wake
Natambua uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, kuchambua na kushawishi ili ukubaliane naye
Natambua uthubutu wake linapikuja suala la haki na kuipigania Tanganyika ...
2. Kauli hii siyo sahihi. Labda kama una maana wanaotetemeka ni CCM na vibaraka zao.
Kwa hakika wale madalali wa DP World na vibaraka zao wanatetemeka mno wakisikia jina lake likitajwa. Hali wanafurahi mno wakisikia hata dalili tu, za kutaka kujaribu kumbagaza kwa namma yoyote. Kwa hakika hapo hata maokoto yanaweza yakahusika.
3. Hili ni sahihi ni la muhimu mno kwetu (sote) bila kujali vyama tunapokabiliana na CCM na vibaraka zao. Adui zetu wanapaswa kuliona hilo kwa uthabiti wake na bila ya kuwapo tashwishi yoyote.
Kwamba CCM wakisikia tunataka katiba mpya sasa, wajue tuna maanisha hivyo na si vinginevyo!
Lakini amakinike mno na mfumo maana hauishiwi mbinu za kukwamisha ama kufelisha mambo! [/quote]
4. Haya ni mawazo yako ambapo kila mtu anaweza kuwa na yake. Kwamba ni ushauri wako wa nia njema kwa mtazamo wako, kwa Mwabukusi?
Hiyo kwa hakika ni haki yako kama ilivyo kwa mtu yeyote. Miye naweza kuwa nao wangu pia hata kwako, Retired au kwa mwingine awaye yote.
"Kumbuka kuna watu wengi tu (hata humu JF) wanaamini wanazo shauri bora zaidi kwa kina Natenyahu, HAMAS, Museveni, PK, Obama na hata kina Biden huko."
Yote ya kheri tu.
Ni nature ya binadamu kudhani anaweza kuwa na mawazo mazuri zaidi kuliko wengine. Lakini haina maana kuwa ndiyo ulio usahihi au hata ulio pekee. Hii ikizingatiwa kwa ukamili wake kuwa hakuna ambaye ni "supernatural" baina yetu.
6. Hili angalizo lako hapa lina ukakasi. Linakuwa je kutoka kwetu kwenda kwa wapambanaji waliodhamiria wenye kuhitaji mkubwa wa kupewa moyo na kutiwa shime zaidi?
Maangalizo ya hivi kama mlengwa hajakuomba, huwa ni ya kutulia shaka sana. Haya huwa ni ya adui mwenye lengo la kuwajengea hofu wale wenye nia ya kumkabili.
Tutaogopa kuthubutu hadi lini, kwa sababu ya maangalizo tu kama yale uchwara ya vipigo vya mbwa koko?
Alimwambia mkutano wake umezuiwa kwakuwa CHADEMA wameenda KULALAMIKA polisi kwamba nyimbo zao CHADEMA zinapigwa kwenye mkutano wa wakili msomi Mwabukusi.. Mwabukusi bila hata kutafakari hiyo kauli akasitisha mkutano wake na kwa namna fulani akailaumu CHADEMA
Alimwambia mkutano wake umezuiwa kwakuwa CHADEMA wameenda KULALAMIKA polisi kwamba nyimbo zao CHADEMA zinapigwa kwenye mkutano wa wakili msomi Mwabukusi.. Mwabukusi bila hata kutafakari hiyo kauli akasitisha mkutano wake na kwa namna fulani akailaumu CHADEMA[/quote]
1. Mkuu, huku ni kumkosea sana wakili wa mahakama ya rufaa, wakili msomi, bwana Mwabukusi.
Hivi kweli wakili msomi Mwabukusi alishindwa kuuona mtego hapo? Ni lini polisi wamekuwa wema kiasi hicho cha kuchukua hatua za haraka walipopata malalamiko ya CHADEMA?
2. Kutaka kumzungumzia Mwabukusi wakili msomi na polisi haiwezi kuwa kwenye udadavuzi wako huu na eti huku tuache hata kukustua "offside" hiyo ya wazi, ndugu.
"Mwabukusi anapambana nao hao watu kila siku na pia mahakamani. Huyo ana kitanzi cha kifo shingoni kama mafwedhuli hao wakiweza kukithibitisha ambacho walishapenda kumtuhumu nacho
Itoshe kukufahamisha huyo siyo level yetu: yaani mimi ay wewe!
Zingatia:
"Mwabukusi alisema alichoambiwa na polisi.
Kosa lake ni kusema alichokuwa ameambiwa na polisi?"
Kuna kesi ngapi polisi za uonevu, za kubambikwa za kusingiziwa za viongozi na wanachama wa CHADEMA kila mahali Tanganyika ambazo zinasuasua mpaka kesho?
Wakili msomi Mwabukusi ni mnyenyekevu na mkweli sana baada ya taarifa hiyo aliita waandishi wa habari na kuwapa mrejesho huo huku akiapa kumburuza kortini OCD
7. Wanyenyekevu ni watu wenye kutaka mapatano. Si watu wa visasi. Si wenye kujihesabia haki. Si wajanja wajanja. Si watu wa hila. Nk. nk.
Kwa kiswahili wakiitwa waungwana.
Kwamba kumbe hata mnajua yeye alikuwa ni kama transmitter tu? Akizichukua na kuzifanyia kazi hadharani na bila kuchelewa taarifa zote kama alivyozipata?
Zingatia alipopata ya polisi alifanyia kazi mara moja kama ilivyokuja. Akawaambia watu lililojiri na kuahirisha mkutano. Hekima nyingine kubwa tu.
Sasa hadi hapo Ya-Rabi, iko shida gani na nani, na Mwabukusi wapi?
1. Kulikoni kutokumakinika wewe ili ufanye vizuri zaidi? Hudhani ushauri wako huu kufanana na Tanzania kujaribu kuishauri Japan namna ya njema zaidi ya kutengeneza magari vizuri?
Au ni Ile kujidanganya kuwa kwenye miti hakuna wajenzi?
Hivi umejiuliza kama Mwabukusi anahitaji hata ushauri lakini? Achilia mbali wa kwako?
"Kwa mtaji huu huoni unakaribia kuanza kujipa kazi ya kumshauri hata Mungu?"
Hiiiiiii bagosha!
Ama kweli mmevurugwa siyo kwa kiwango hiki. Tafuteni suluhu. Ujanja ujanja haulipi!
Kina Mwabukusi hawana ugomvi na mtu. Kina Mwabukusi wana agenda za wananchi mkononi.
Kwa mfano alipopata wasaa wa kuwasalimia Wanambeya waliokusanyika nyumbani kwa Mwabukusi alitoa mfano wa kushangaza kwamba bunge lisiwe la chama kimoja tu bali kuwe walau na uwiano! Akatoa mfano CCM ikiwa na wabunge 200 basi wengine wawe na wabunge 100
What a grave mistake! Hapo alijidhihiri anasimamia nini na anaamini nini... Kwamba bado ana imani kubwa na CCM kuliko vyama vingine! Katika nyakati hizi za harakati kubwa za kuiondoa CCM madarakani, mpiganaji mpambanaji kamwe hawezi kuongea kitu kama hicho! Sitaki kumuita Dr. Slaa pandikizi.. Lakini nyayo zake zimechafuka!
5. Ha haa ha 🤣🤣 Kwamba wewe sasa umekuwa Jaji. Mwanzo ulikuwa prosecutor na Shahidi? Kwamba hukumu yako sasa ni ya haki. Hii siyo janja ya nyani kula mahindi mabichi tu ndugu?
Hamna kitu hapa ndugu yangu.
Kujaribu kumbagaza Dk. Slaa wewe, ni sawa na Mwaipopo na Shivji tu.
Hapa nikurejeshe kule kwenye matunguli yetu na uganga wa kienyeji dongobeshi ikungu lya bashashi ndugu yangu. Haya mengine ni level nyingine!
6. Haha ha ha. 🤣🤣 Kwani macho yako yana upako ndugu? Au wewe ni supernatural yaani Mungu, malaika, jini au shweitani?
Ustaarabu si ni kukaa na mtazamo wako ndugu? Kila mtu ana wake.
Kila mtu akianza kutupa mitazamo yake kukuhusu wewe na wengine wakakubatiza na ushoga humo, kwani utasema je hapo ndugu?
HITIMISHO
Inasikitisha kuwa bandiko lako refu linajadili watu (Mwabukusi na Dk. Slaa) badala ya kujadili hoja zao.
Cha kusikitisha zaidi Kwa maoni yangu ni kuwa umeshindwa kujielekeza kwenye kutafuta mapatano ukajikita kwenye chokochoko za kitoto. Yaani kuleta mafarakano kati ya chama na hawa ndugu au hawa ndugu baina yao.
Jitihada hizo ni dua la kuku kwa sababu agenda za hawa ni agenda za watu si zao. Agenda za watu ni agenda za Mungu.
Nawàheshimu sana hawa watu.
Na wakiunda chama cha upinzani watashinda.
Nitawatafuta niongee nao mambo ya msingi.
Ambayo siwezi kuyaongelea hadharani.
Wenye hamu ya lile, wanifuate inbo,
Nawàheshimu sana hawa watu.
Na wakiunda chama cha upinzani watashinda.
Nitawatafuta niongee nao mambo ya msingi.
Ambayo siwezi kuyaongelea hadharani.
Wenye hamu ya lile, wanifuate inbo,
Kama wanataka kufanikiwa katika upinzani wao ni lazima wawe tofauti kidogo kwanza wakubali kukosolewa. Pili wakubali kuwa hata ccm kuna mazuri wanafanya hivyo basi wanapaswa kuwapongeza pale wanaopoana jambo zuri limefanywa na serikali ya ccm.
Tatu wasiwe wanapinga kila kitu ambacho serikali ya ccm inafanya hasa issue za kimaendeleo mfano ujezi wa reli, ununuzi wa ndege nk. badala yake wawe wanatoa ushauri nini kifanyike ili kuboresha.
Nne wasiwe wanaonesha kufurahia hadharani pale mali za umma zinapokamatwa mfano ndege, hii itawafanya waonekane wapinzani wastaarabu. Tano wasijikite kupambana na mtu mmoja mmoja ndani ya ccm kwani kuna siku huyo mtu anaweza asiwepo bali ccm itaendelea kuwepo na kutawala, wanapaswa kupambana na mfumo. Sita wawe wanajikita kuzungumzia maswala ya wananchi zaidi kuliko mambo yao binafsi ya chama, mfano wanapaswa kuilazimisha serikqli kukamilisha miradi kwa wakati, mfano miradi ya maji, umeme, vituo vya afya nk.
Saba wawe wanaeneza sera zao kwa wananchi kwamba wao wakipata dola watafanya nini na sio kuishia kukosoa serikali halafu hawasemi wao watafanya nini endapo watapata dola.
Nane wawe tayari kufanya kazi na mtu yeyote mzalendo wasichague anatoka pande gani nchii hii ni yetu sote.
Tisa waweke uchama pembeni, Tanzania na utaifa ndio iwe kipaumbele chao.
Kumi wajiepushe na lugha za kejeli, ubaguzi na zenye ukakasi, watanzania walio wengi ni wastaarabu na wamejingewa misingi ya kuheshimiana mkubwa kwa mdogo.
Mwisho waheshimu kila binadamu aliyopo chama chochote na wasione kama wao ndio wenye akili na kuanza kudharau kila mtu aliye kwenye chama kingine, wakumbuke siasa haina adui wa kudumu hivyo basi wanapaswa wawe na chama ambacho mfuasi wa chama chochote anaweza jiunga bila kujiona mgeni na anaweza ondoka bila kusimagwa na kuitwa majina kama msaliti.
Kama wanataka kufanikiwa katika upinzani wao ni lazima wawe tofauti kidogo kwanza wakubali kukosolewa. Pili wakubali kuwa hata ccm kuna mazuri wanafanya hivyo basi wanapaswa kuwapongeza pale wanaopoana jambo zuri limefanywa na serikali ya ccm.
Tatu wasiwe wanapinga kila kitu ambacho serikali ya ccm inafanya hasa issue za kimaendeleo mfano ujezi wa reli, ununuzi wa ndege nk. badala yake wawe wanatoa ushauri nini kifanyike ili kuboresha.
Tano wasijikite kupambana na mtu mmoja mmoja ndani ya ccm kwani kuna siku huyo mtu anaweza asiwepo bali ccm itaendelea kuwepo na kutawala, wanapaswa kupambana na mfumo. Sita wawe wanajikita kuzungumzia maswala ya wananchi zaidi kuliko mambo yao binafsi ya chama, mfano wanapaswa kuilazimisha serikqli kukamilisha miradi kwa wakati, mfano miradi ya maji, umeme, vituo vya afya nk.
Saba wawe wanaeneza sera zao kwa wananchi kwamba wao wakipata dola watafanya nini na sio kuishia kukosoa serikali halafu hawasemi wao watafanya nini endapo watapata dola.
Kumi wajiepushe na lugha za kejeli, ubaguzi na zenye ukakasi, watanzania walio wengi ni wastaarabu na wamejingewa misingi ya kuheshimiana mkubwa kwa mdogo.
Mwisho waheshimu kila binadamu aliyopo chama chochote na wasione kama wao ndio wenye akili na kuanza kudharau kila mtu aliye kwenye chama kingine, wakumbuke siasa haina adui wa kudumu hivyo basi wanapaswa wawe na chama ambacho mfuasi wa chama chochote anaweza jiunga bila kujiona mgeni na anaweza ondoka bila kusimagwa na kuitwa majina kama msaliti.
Sakata la Bandari na hifadhi za misitu na mbuga za wanyama ipo siku Watanzania watalia kama mbwa, bidii na uzalendo wa Hawa watu inaonekana ni mzaha Watanganyika watambue wazanzibar wana agenda mbaya sana kupitia huyu Bibi yao. Fitina yao ipo rohoni toka uchaguzi wa 2005
Sakata la Bandari na hifadhi za misitu na mbuga za wanyama ipo siku Watanzania watalia kama mbwa, bidii na uzalendo wa Hawa watu inaonekana ni mzaha Watanganyika watambue wazanzibar wana agenda mbaya sana kupitia huyu Bibi yao. Fitina yao ipo rohoni toka uchaguzi wa 2005