Mwabukusi: Kama tunataka kupona kitaifa tutibu kwanza majeraha

Mwabukusi: Kama tunataka kupona kitaifa tutibu kwanza majeraha

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakilj Boniface Mwabukusi, amesema Tanzania inahitaji umakini, kusikilizana na kukubali makosa ili kujenga maridhiano na kuanza mchakato wa uponyaji wa taifa.

Mwabukusi amesema hayo Agosti 28, 2026, katika Jukwaa la Demokrasia, akisisitiza kuwa taifa halihitaji vitisho wala kutukanana katika kipindi hiki, bali linahitaji kukabiliana na changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho la pamoja.

“Hatuhitaji vitisho. Hatuhitaji kutukanana. Lazima tukubali tumekosea. Na wote tuwe tayari kusikilizana. Sisi wanaharakati tuwe tayari kusikilizana, Serikali iwe tayari kutusikiliza na vyama viwe tayari kusikilizwa.”

Mwabukusi amesema haki ya mpito haipaswi kuangalia tu upande wa makosa ya jinai, bali pia kuangalia waathirika waliopoteza mali na ndugu zao, akisisitiza umuhimu wa marejesho ya haki (reparations).

Aidha, Mwabukusi amesema Tanzania inahitaji kwanza kujenga mazingira ya uponyaji na utulivu wa fikra kabla ya kuingia katika mjadala mpana wa Katiba.

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom