The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Mwabukusi akitema cheche
Baada ya wakili Boniface Mwabukusi kukatwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kwa madai ya kuwa na doa la kimaadili kinyume na kanuni za uchaguzi huo, ameibuka akisema kuwa wakati wa zoezi hilo la uchaguzi, aliwekewa mapingamizi kadhaa, lakini yalipofika kwenye kamati ya uchaguzi mapingamizi haya yaliondolewa kwakuwa yalionekana kuwa hayana hoja. Pingamizi la kwanza lilieleza kuwa Mwabukusi ni mwanasiasa.
Hata hivyo, kuhusu hilo, Mwabukusi anaeleza kuwa, "Sheria wala kanuni zetu hazikatazi mtu kuwa mwanasiasa, zinakataza mtu kuwa kiongozi wa chama cha siasa. Na mhusika alishindwa kuwasilisha ushahidi wowote mbele ya kamati kuonesha kwamba mimi ni kiongozi wa chama chochote cha siasa.
Anasema pingamizi la pili ni kuwa alipatikana na kosa la kimaadili kwahiyo kutokidhi matakwa ya Kanuni ya 13 ambayo inasema kiongozi anatakiwa kuwa na ethics na good morals. Hata hivyo, Mwabukusi anasema mashitaka yalyokuwa yakimkabili ni professional misconduct, na siyo ethical issues. Na kuwa uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ambao ulitolewa kwa nia ya kumuonea, ulimhukumu "kwakuwa eti niliwakosea viongozi wakuu wa nchi. Hata kama ninazungumza ukweli sikutakiwa kuzungumze eti nistasababisha vurugu... Nani alikwambia kuna kiongozi wa juu ya Katiba na Sheria yetu?"
"Kila mtu anakosolewa, cha muhimu ni kikukosoa nikukosoe kwa ukweli. Mimi sikuwakosoa viongozi wa juu kwa kuwakosea. Nilisema kweli na ndiyo msimamo wangu kuwa Mkataba wa ule wa IGA uliosainiwa kati ya Tanzania Bara na Dubai ni mkataba unaoiba rasilimali za taifa kinyume na sheria"
"Kuna magenge ya nje ya ndani na nje ya TLS yanayofanya kazi ku-frustrate michakato ya kidemokrasia ya ndani kwa lengo la kuwapangia Mawakili wanaowataka. Nataka kawaambia I'll never retreat, I'll never surrender mpaka nipate haki yangu!"
PIA, SOMA:
- Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi imemuengua Boniface Mwabukusi kugombea nafasi ya Rais wa TLS