Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa mwito mzito kwa Baraza la Vyama vya Siasa pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuchukua hatua za kufuta vyama vyote vya siasa ambavyo havina utendaji unaoonekana kwa wananchi kule nyanjani (field).
Akizungumza, Oktoba 7, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa, Wakili Mwabukusi amesisitiza kuwa imefika wakati wa kuwa na vyama vyenye matokeo mbadala ya kubaki vikiwa vimesajiliwa kwenye karatasi pekee bila kutoa mchango wowote wa kidemokrasia.
"Sisi wananchi tusiokuwa wanasiasa tumewapa mkataba kwamba nyinyi mtatutungia sera na kujiandaa kuongoza nchi. Moja ya kazi ya Baraza la Vyama iwe ni kufuta vyama ambavyo hatuvioni field. Vyama hata kama huwezi kuzunguka nchi nzima, chagua mikoa yako minne uweke kambi mpaka upate mbunge au madiwani." — Wakili Boniface Mwabukusi, Rais wa TLS.
Akiangazia misingi ya kiutawala, Mwabukusi ameeleza kuwa siasa za Tanzania zinahitaji kujengwa kwenye utamaduni wa kusema ukweli, kwani huo ndio mwanzo wa uwajibikaji unaoweza kurejesha matumaini yaliyopotea kwa wananchi.
Rais huyo wa TLS amebainisha kuwa iwapo vyama vya siasa vitajikita katika maeneo maalum na kupata uwakilishi wa kweli, itasaidia kuondoa mfumo wa chama kimoja kutawala kwa asilimia kubwa bungeni. Ametoa mfano kuwa hali hiyo ikitokea, mawaziri watalazimika kujipanga vyema kabla ya kuwasilisha mswada au hoja bungeni wakijua hawana kauli ya mwisho bila maridhiano na vyama vingine.