Mwabukusi ni Pandikizi la CCM? Ndiye mvurugaji mkuu wa Demokrasia!

Huyu jamaa huwa ni mnafki,huwa mara nyingi huwa anajifanya mpinzani lakini mara nyingi kazi yake ni kuunga mkono wanaotukana CHADEMA na kujifanya wao ndiyo wapinzani wa kweli
Mtu kama huyu ni Hatari zaidi ya huyo Mwabukusi
Hajui hata kuwa tunamjua huyo Mwabukusi nje ndani na kilichomtoa CHADEMA
 

Upinzani gani hautaki Urais?. Tuache unafiki. Halafu kuhusu katiba Mpya, mbona CHADEMA wamelipigia kelele
 
Unamzungumzia nani hapa hata hueleweki.

Kama unanizungumzia mimi, ujue nilishavuka huo mstari wa siasa za kitoto mnazoimba hapa, nikiona baya popote nalisema, nyie ni madikteta msiojitambua, hamtaki kukosolewa lakini mnataka kwenda ikulu, mkifika huko ikulu mtakuwa madikteta wabaya sana msiomsikiliza yeyote.

Mko na upeo wa kifikra unaofanana, sijui mlisomea shule moja!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Utamkubalije Mwabukusi anaye ushambulia upinzani kila siku especially CHADEMA?. Siku akiunga mkono CCM utafanyaje?. Maana hawatabiliki Hawa watu.
Nani aliwaambia Chadema ni malaika wasikosolewe? akiunga mkono CCM ni juu yake, kwani wangapi wameshakwenda huko kisha Chadema ikapoteza nini?! Uoga wenu tu.

Hii mindset yenu mnaamini itawapeleka ikulu? ili mkawe madikteta mkifika huko?

Nyie watu tokeni nje ya hilo box mlilojificha, msiendelee kujidanganya kwa ujinga wenu mkajiona mko sahihi, simply because ujinga wenu uko na support kubwa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mwabukusi hajawahi kuwa the best,una mahaba na wavurugaji sana we mtu, Mwabukusi ni zao la tamaa ya Madaraka, anapiga kelele kwa tamaa hiyo hiyo,yeye na Mbatia walikaa kimya baada ya kuahidiwa ubunge Busokelo na Magufuli,baada ya kugombana huko NCCR ndiyo anajifanya kutaka kuegamia CHADEMA na CHADEMA wampe bega wakati aliondoka baada ya kukosa umakamu mwenyekiti wa kanda ya Nyasa, baki na mahaba yako lakini huna uhalali wa kutuambia Mwabukusi anafaa kuungwa mkono, huyo jamaako no opportunist
 
Kijana jenga ACT yako achana na CHADEMA
 
ata akigombea serikali za mitaa hashindi ng'oo 🐒
 
Sioni hoja yako, ni hisia tupu umejaza kichwani dhidi yake kama wenzako, mnatetemeka na siasa zenu za kioga.

Adv. Mwabukusi is the best, kama hujafika level ya kumuelewa ujue wewe bado ni mchanga sana kifikra.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

Sawa tumekusikia. Ila CHADEMA itabakia hata Mwabukusi aishambulie kiasi gani.
 
Sawa tumekusikia. Ila CHADEMA itabakia hata Mwabukusi aishambulie kiasi gani.
Mnaongoza kundi la wafuasi laini wa upinzani, linaloogopa kukosoana kisa litapoteza kura, very funny!

Hizo kura za kuhamishwa kwa kauli ya mtu mmoja ni fake, hazina mizizi, wake up na wenzako muwe na imani, sio kuishi kwa hofu za kitoto.

Akitokea mtu kuwakosoa mnamuona adui hafai, wow!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Acha ushamba bwana hakunaga kitu kama kuvuka siasa za kitoto, siasa ni itikadi kama itikadi yangu haiendani na Mwabukusi huwezi kunilazimisha nimuunge mkono eti kisa kuonesha Maturity,siasa siyo suala la maturity ni suala la unaamini nini na huamini nini,kujifanya umevuka aina hizi za siasa ni dalili za kujiuza ili uonekane na wagawa vyeo.
 
Ila Mwabukusi atachuja muda sio mrefu. Maana baadala ya kuunganisha nguvu anawaponda CHADEMA, wakati yeye juzi tu hapa alikuwa rafiki wa CCM na wakahaidiwa majimbo kabla upepo haujabadilika.
 

Mbona kukosoana kupo?. Mbona Mbowe tulimkosoa mpaka akalalamika hadharani. Lakini kitendo Cha Mwabukusi kuwashambulia wapinzani hasa CHADEMA kuliko CCM kunatia shaka Sana. Yani anayewin ni CCM.

Huyo Mwabukusi aliitisha maanadamano Mbeya yakashindikana , nani alimlaumu?. Aanzishe chama chake tuone alicholenga Kama sio uchawa kwa CCM .
 
Nimecheka namba 13.
 
Mimi ninamjua Mwabukusi, nimekuwa sehemu za kampeni yake kanda ya Nyasa kabla hajahamia NCCR, sitangulizi hisia,naongea kitu ninachokifahamu,Mwabukusi ni msaka fursa
Lakini kama wewe ni make wake siwezi kukupinga maana utakuwa unamjua vizuri zaidi yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…