Mwabukusi: Watanzania waambie waandamane kwa ajili ya Simba au Yanga, wataandamana hata uchi

Mwabukusi: Watanzania waambie waandamane kwa ajili ya Simba au Yanga, wataandamana hata uchi

Kwa Tanzania hii ukitaka maandamano yafae na watu waitikie kuna mikoa ifuatayo ambayo watu wake hawana cha kupoteza.
1. Mbeya
2. Mara
3. Arusha
4. Singida
5. Shinyanga.
Japo kwa Singida na Shinyanga mpaka jambo liwaguse sana wahusika.
 
Atalaumiwa sana dobi kaniki rangi yake:

"Maandamano yalikuwa yaanzie Tanga kwenye mazishi, yakazimwa blindly."

Kwa maneno ya mkenya

"Mwizi huwa hapeani miadi!"
Cc: imhotep, binti kiziwi
Kama lengo likikuwa ni kupinga utekaji, mateso, na mauaji.
Wangefanya siku hiyohiyo huko Tanga.

hii ingekuwa na impacts zaidi, kuliko kusubiri wiki mbili baadae.
n tabia ya watanzania washasahau.
Kama ambavyo tumewasahau waliopotea wengine
 
Watanzania waambie njooni muandamane Simba ameleta kombe, wataandamana hata uchi kwenda uwanja wa Taifa. Wanazingatia sana mamboa ambayo si ya msingi.

Kwenye culture yetu tuliamini kuwa mambo yote magumu magumu ni ya viongozi. Hali hii itaendele na itakuwepo kwa muda mrefu kwasababu kwanza hatujabadili mfumo wetu wa elimu na sasa hivi tumeubemenda, tumeutikisa zaidi.

Ile free thinking huipati sawasawa ndiyo maana utakuta watoto wa siku hizi Ukimona anapiga kelele ni boom, yaani kama ndege.

Soma:
Niandamane hela ya luzuku ya chama chenu mtanigaia..
 
Jamaa kaongea point sana.

Hiki kizazi cha kipuuzi kabisa
Yeye mbona hakuenda kuandamana maandamano ya Chadema? Yeye sie wa kizazi hiki na ana free thinking kubwa mbona hakwenda maandamano?

Mwandishi unayehoji na wewe huko vizuri ulitakiwa umuhoji kuwa wewe kama wa kizazi kinachojielewa na chenye free thinking na elimu ya kueleweka uliandamana wapi labda maandamano ya Chadema yaliyoitishwa?

Waandishi wa habari jiongezeni jamani
 
Watanzania waambie njooni muandamane Simba ameleta kombe, wataandamana hata uchi kwenda uwanja wa Taifa. Wanazingatia sana mamboa ambayo si ya msingi.

Kwenye culture yetu tuliamini kuwa mambo yote magumu magumu ni ya viongozi. Hali hii itaendele na itakuwepo kwa muda mrefu kwasababu kwanza hatujabadili mfumo wetu wa elimu na sasa hivi tumeubemenda, tumeutikisa zaidi.

Ile free thinking huipati sawasawa ndiyo maana utakuta watoto wa siku hizi Ukimona anapiga kelele ni boom, yaani kama ndege.

Soma:
Kwa kifupi Watanzania tulio wengi hatuna 'critical thinking' (hatuwezi kuhoji kwa nini mambo yafanyike kama yanavyofanyika na si tofauti). Kwa vile hatuna utamaduni wa kujihoji, tupo tupo tu bora liende, Kila mtu na shughuli zake.
 
Back
Top Bottom