Niseme tu kuwa sina kipingamizi na wewe kufikiria
"mambo makubwa zaidi" kwa sasa. After-all ni mambo ya kitaifa. Nilikualert kama mtu anayefuatilia mambo (Tulipata kujadili juu ya sanaa na Diamond was mentioned) na maybe kuna kitu ungekiona especially perception ya watu (vijana) kwa Diamond. Nadhani kipindi kile tunajadili juu ya Diamond na Kiba nchi haikuwa imetulia pia, ilikuwa katika mgogoro wa kidini na kama sijakosea palikuwa na mauaji na majeruhi kwa wenzetu maalbino,
jambo ambalo mi silioni kuwa dogo hata kama limetokea watu wachache.
Kuhusu NECTA kutoa matokeo yaliyokuwa CSV-fomatted yaliyokuwa zipped na
yenye "13 MB" japo ni mfano tu unaowakilisha grief yako juu ya mifumo yetu nitasema kidogo
(Nafanya makusudi kutosema sana maana bado tuko msibani)!
Tanzania ni nchi changa na haina wataalam katika sekta nyingi hii inasababisha hata mambo madogo tu kama uliyoyatamani yasifanyike kwa kuwa
wakubwa wamezungukwa na watu wasiowaza hayo unayoyawish na wao hawayawazi kabisa. Kwamba rekodi kadhaa kama "pattern ya nani wa kwanza kwa kila somo kwa nchi nzima" haina sababu ya mwananchi wa kawaida kuijua, ni nani huyu anayejali haya? Wana majibu,
"Aende Wizarani, kwani kanyimwa?" Waziri wa Viwanda na Biashara wakati huo Juma Ngasongwa aliwahi kusema "Tatizo lenu mnataka kila mkataba wa Serikali uwe wazi, haiwezekani!"
Ukweli ni kuwa vitu vingi bado sana katika nchi hii. Elimu, michezo, teknolojia etc, Sijui kama kuna ulazima wa akili za mtabiri Nostradamus au Mwanafalsafa Nietzsche kujua kuwa tuko chini. Hata kama sifuri na DIV FOUR zisingekuwa hivi kwani hao wanaofaulu nao uwezo wao ukoje? Bado sana. Akina
Nyani Ngabu kila leo wanahoji hao wa
"Special Schools" ni special kiasi gani.
Hivi ni lini tunaweza kuwa na watu wanaofanya majaribio yenye magnitude kama ya akina Robert Millikan, DeBroglie, Heinselberg, Einstein, Max Plank, Niels Bohr etc (Nimewataja watu ambao najua wako katika anga zako)? Kwamba tuna watu wanatoa maelezo yenye ushawishi juu ya Black Hole.....Relativity.... na labda juu ya next gen cpus na hybrids za cpu na gpu, na huenda tukashindana na Intel kwa kufanya reverse engineering ya processors zao au tukaja na brand new technology ya pc cpus zenye teraflops kadhaa..... ni lini....??? Kuna kazi.
Anyway, thread ni juu ya Diamond, tusi-hijack. Bendera nusu mlingoti, itakaporudi juu Absalom Kibanda kashambuliwa. Tanzania.
Aroo Mama Rhobi rete kama turivyo.
For your reference:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wa-nao-ni-wasomi-wa-udsm-wanasaka-degree.html