Mwadui 0-1 Simba | Uwanja wa Kambarage | Vodacom Premier League

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL' kuvurumishwa leo Jumapili ya Aprili 18, 2021 ambapo Mwadui FC anakwaruzana na Mabingwa wa Nchi, Mnyama Mkali Simba SC kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Mchezo huu utarajiwa kuwa kali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 kwa kila timu ikihitaji alama tatu muhimu kuweza kufikia sehemu ya juu kwenye VPL

Wachimba Almasi wakiwa na hali mbaya kwenye msimamo wa Ligi, wataweza kumzuia Mnyama Mkali? Au Mnyama Mkali ataendeleza desturi yake ya kuandika alama tatu muhimu ili kutetea ubingwa wake?

Kumbuka mtanange huu wa VPL ni kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


=========

Timu zipo uwanjani zikifanyiwa ukaguzi, salamu pamoja na kupiga picha za kumbukumbu.

Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, mashabiki ni wengi wamejitokeza hasa wa Simba

Naaaam mpira umeanza ni vita vya VPL, kuwania alama tatu muhimu

01' Chama upande wa kushoto, anakwendaa anapiga shutiiiiii loooooo golikipa anatema shuti lile na unaokolewa na mabeki

Ilikuwa hatari sana lango la Mwadui FC na nafasi bomba kwa Simba SC

Mchezaji wa Mwadui anapiga shutiiiiii linapaa nje ya lango la Simba SC

10' Hakuna timu imeona lango huku Simba wakimiliki zaidi mpira dhidi ya Mwadui FC

15' Mpira unachezwa zaidi eneo la Mwadui FC. Hii ni ishara mashambulizi ni makali kwao, lakini hakuna bao

Mwadui FC 0-0 Simba SC

25' Wanakwenda Mwadui FC, shambulizi kwa Simba, lakini golikipa Manula anaokoa hatari na kuweka salama lango.

34' mpira unapigwa mbele kule kwake Chamaaa, anapiga shutiiiiii linatoka nje na kuwa Goal Kick

40' Mwadui FC wameweza kudhibiti hatari zote za Simba SC kwa kipindi hiki cha kwanza pamoja na Simba kumiliki zaidi mpira

Mwadui FC 0-0 Simba SC

44' Anapigaaaa kulee mpira unagonga mlingoti na kumkuta Beki wa Mwadui FC na kuokoa, ilikuwa hatari sana lango la Mwadui FC

45+2'
Kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Kambarage, ni VPL

Inapigwaa kwenye lango la Simba shutii wanakosa Mwadui FC

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo hakuna timu imeweza kusalimia lango la mwenzake si Mwadui FC wala Simba SC

HT: VPL, Mwadui FC 0-0 Simba SC


Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Kambarage.

Mabadiliko upande wa Simba SC Ametoka Chikwende na Mkude na wameingia Bocco na Morrison

Mabadiliko upande wa Mwadui FC, Ametoka Richard na Ameingia Aziz.

Uhuru wa Mwadui FC anaonyeshwa Kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Bernard Morrison

48' Nafasi kwa Simba anakwendaa Bocco, anapiga krosiiiiiiii loooooo unatoka nje Mpira

51' Mpira wa uliopigwa na Morrison Washambuliaji Bocco na Kagere wanashidwa wanakosa utulivu wa kuweka wavuni mpira.

64' Kiango wa Mwadui anaonyeshwa Kadi ya Njano baada kumchezea faulo Chama

66' Inapigwa Kona na Morrisoooon kwake Onyango anaruka juu na kupiga kichwa mpira unamkuta Boccooo

Goooooooooooooaal Gooooal

John Bocco anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa kichwa

Mwadui FC 0-1 Simba SC


Anakwendaa Kagere go go go go go laaaaa anaokoa Difenda yule wa Mwadui FC, ilikuwa nafasi kwa Simba SC kuandika bao.

70' Bernard Morrison anaonyesha Kadi ya Njano

Haya Mwadui FC wameamka wanashambulia kujaribu kusawazisha lakini ngome ya Simba chini ya Wawa na Onyango wapo imara

80' Simba anaongoza moja bila, wakati huo huo Mzamir ameingia na Ametoka Bwalya upande wa Simba SC

90+4' kuelekea kumalizika kwa mchezo wa leo wa VPL'

Ni free kick kuelekea Mwadui FC, Bernard anapigaaaaa, lakini mpira unatoka nje ya lango.

Wawa kwake Onyango wanapiga pembeni kuleee kwake Hussein wanagonga gonga mpira ni wakati wa Biriani

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Mwadui FC, bao la John Bocco dakika ya 66'.

FT; VPL' Mwadui FC 0-1 Simba SC


........... Ghazwat
 
Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Kambarage

Naaaam mpira umeanza ni vita vya VPL

Mwadui FC 0-0 Simba SC
 
01' Chama upande kushoto anapiga shutiiiiii loooooo, golikipa anatema shuti lile

Ilikuwa hatari sana lango la mwadui FC
 
Kuwa makini na simu yako isiibiwe,kuna jamaa wanasifika kwa wizi wa simu.Waliwaikuwapokea wageni airport,mwisho wa siku wale wageni hawakuona simu zao.
Hata kombe la VPL wanaweza kuliiba,hao jamaa ni nouma sana.
😂😂😂😂🤣🤣🤣Aisee wana hasira sana ila tunawavumilia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…