Mwajiri ametumia Mishahara yangu kukopea Mikopo LUKUKI

Mwajiri ametumia Mishahara yangu kukopea Mikopo LUKUKI

John L. Mihambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
526
Reaction score
177
Habari Magwiji wa Sheria, naomba kupatiwa muongozo wa kisheria ili niweze kumburuza aliyekuwa Mwajiri wangu MAHAKANI.
Huyu bwana alisimamisha mishahara yangu kwa muda mrefu kwa madai kwamba imerudishwa HAZINA kutona na utata wa utumishi wangu, baadaye nikaja kugundua mishahara hiyo inapokelewa na MTU NISIYEMFAHAMU huku akiwa amepatiwa MKOPO kutoka taasisi ya PLATINUM CREDIT LTD.
Nilipofuatilia kwa Mwajiri, akarudisha mshahara na makato ya mkopo wake wa kughushi, kisha akaendelea kulipa MTU NISIYEMFAHAMU hadi baadaye nilipombaini tena, huku kukiwa na MIKOPO MINGINE YA KUGHUSHI kutoka taasisi za LETSHEGO NA AFRICAN BANKING CORPORATION (BancABC).
Nahitaji kuwapeleka hawa WAHUNI MAHAKANI, ili wanilipe fidia kutokana na kadhia hii ya muda mrefu, naomba kupatiwa msaada wa kisheria.

0755 732 981 / 0784 324 102
 
Andika barua kwa mwajiri wako kuomba kulipwa stahiki yako yote, akishindwa mpeleke baraza la usuluhisi (CMA) ndani ya siku 30 baada ya kukaidi ombi lako.
kuhusu hayo makampuni ya mikopo unaweza kuwawajibisha kisheria pia, ukimuunganisha mwajiri wako kama mtuhumiwa. utatakiwa kuwasilisha hii kwa DPP kupitia Takukuru.
 
Aisee! Nchi hii inaliwa na wenye meno, suala lako limefikia wapi bwana Mihambo? Mwajiri anawezaje kukopa kwa kutumia majina yako? Akaunti ya benki ilitumika ipi? Ni nani aliingiza hilo deni kwenye mfumo wa mishahara ya watumishi (LAWSON)?
 
Back
Top Bottom