Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), Mwajuma Noty Mirambo, amesema kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha anaigawa Tanzania kwa Majimbo. Ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni za chama chake kwenye Soko la Mitumba Muheza, Tanga.