Chagga King
JF-Expert Member
- Jul 6, 2011
- 1,866
- 1,076
Mwaka 2007 sukari iliyokuwa inazalishwa ndani ya nchi ilikuwa inauzwa kati ya Tsh 800-900 kwa kilo, ambapo imported sukari kama Ilovo ilikuwa inauzwa 1000/- kwa kilo 1 ya pakti.
Nakubali kuwa kuna sababu nyingi zinazopelekea price fluctuations hasa sababu za kiuchumi, hizi tuziache maana athari zake ni kiasi, tuzungumzie hii ya sasa ambayo imepelekea bei ya sukari kupanda sana (bei zinatofautiana eneo 1 na lingine) lakini zaidi sababu hii imepelekea mpaka sukari kuadimika kabisa.
Gazeti la Mwananchi la tarehe 14 December 2023 (Mvua yapaisha bei ya sukari Kilimanjaro) liliripoti sababu za kupaa kwa bei ya sukari kuwa imetokana na mvua kubwa ambayo imepelekea uvunaji wa miwa kuwa mgumu.
Najua kuna mijadala kuhusu kupanda kwa bei ya sukari, lakini hapa nataka kujua uhalisia wa hii sababu, ikiwa kwa nchi si mara ya kwanza kuwa na mvua kubwa.
Miaka ya 2000 kulikuwa na kiwango kikubwa cha mvua kuliko ilivyo sasa, lakini hatukuwahi kusikia sukari imepanda bei kutokana na mvua kuwa kubwa, hivyo sababu hiyo kukosa uhalisia.
Kwa masilahi mapana ninawaomba wafanya biashara na wazalishaji kuwa wazalendo, maana hii njia wanayotumia ni kama mbinu ya kibiashara ili wao kupata faida kubwa, maana vitu ambavyo vyenye tija kama mafuta na sukari vimekuwa vikitumika ktk wao kujinufaisha kupita kiasi, hivyo waisaidie serikali kwa kupunguza bei ili wananchi waweze kumudu hizo gharama.
nawasilisha