Mwaka 2015 ilikuwa ni aibu kuvaa nguo za kijani wakati 2020 ni ufahari mkubwa

Mwaka 2015 ilikuwa ni aibu kuvaa nguo za kijani wakati 2020 ni ufahari mkubwa

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
CCM ilikuwa imefikishwa pabaya kiasi cha mtu aliyekuwa anavaa shati au kitenge cha kijani alirushiwa mawe. Leo hii tunaona maelfu ya wananchi wakiona fahari kubwa kuvaa jezi za kijani na wanajitokeza kwa wingi ili wapate nafasi ya kupeperusha bendera za Chama Kubwa.
 
Hata leo hii huwezi kumkuta Mtanzania mwenye akili timamu akivaa hizo nguo na kutembea hadharani! Zaidi tunawaona nyinyi wachumia tumbo na wanafiki mlio amua kupambania maisha yenu kupitia hiyo ccm.
 
Wewe siasa huijui, mwaka ambao CCM waliona aibu kuvaa kijani ni 2010. Pia baadaye mwaka huu CCM itakuwa na mpasuko wa aina yake! Endelea kuwa mpenzi mtazamaji.
 
Wewe siasa huijui, mwaka ambao CCM waliona aibu kuvaa kijani ni 2010. Pia baadaye mwaka huu CCM itakuwa na mpasuko wa aina yake! Endelea kuwa mpenzi mtazamaji.
Mpasuko utaanzia wapi kwa chama kama hiki ambacho hakina makundi?
 
Kama una akili timamu huwezi kuvaa nguo ya kijani ufanane na majani ya miti.
 
Dah ila kweli ivumayo sana hupasuka, yaani kitaa hamna tena chochote kinachoashiria uhai wa Chadema. Sio gwanda, scarf wala bendera nyuma ya bodaboda. Hakuna anaejihusisha na chadema tena hadi bodaboda wamewatenga makamanda.
Chadema ilizaliwa, ikalelewa na walezi wasanii ikadumaa sasa inaelekea kufa. Poleni ndugu, jamaa na marafiki.
 
Unataka watu waozee jera?
Nani anaipenda jera...mama wa kambo sio mama wa kweli ila inakudi umuheshimu na kumuita mama
 
Mkuu maisha yanaenda kasi ukiwa na kwenye mtandao wa kusifu na kuabudi inabidi tuu uvae.
 
CCM ilikuwa imefikishwa pabaya kiasi cha mtu aliyekuwa anavaa shati au kitenge cha kijani alirushiwa mawe.
Leo hii tunaona maelfu ya wananchi wakiona fahari kubwa kuvaa jezi za kijani na wanajitokeza kwa wingi ili wapate nafasi ya kupeperusha bendera za Chama Kubwa.

Kwa sababu ya matumizi ya mabavu ndio maana unadhani ccm sasa imeimarika. Kwa sasa matumizi mabaya ya madaraka ya urais ndio yameipa ccm uimara fake, lakini ki uhalisia bado ccm ni ile ile.
 
Kumbe na nyie mnajua kuwa 2015 mlimwibia Lowassa na Maalim, eh?

Back
Top Bottom