Uchaguzi 2020 Mwaka 2015 wapinzani waliipinga CCM sio mgombea. Mwaka 2020, upepo umebadilika

Uchaguzi 2020 Mwaka 2015 wapinzani waliipinga CCM sio mgombea. Mwaka 2020, upepo umebadilika

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2020
Posts
275
Reaction score
802
Neema ya Magufuli ya kupendwa na Wananchi na Wapinzani imeishia 2015. Magufuli alibebwa na sifa ya utendaji kazi na kuwa waziri asiye kuwa na makuu siku zote. Kwa kweli alipendwa na kila kada.

Sasa wengi ni mashahidi ingawa amefanya mambo mengi mazuri kipindi cha 2015/2020, wananchi wengi wamejuta. Hawana hamu na Magufuli tena. Karibia kila mtanzania wa kawaida ameguswa, orodha ni kubwa.

Hivi sasa, wananchi wanaomba Mungu afanye miujiza huyu jamaa apumzike apishe wengine. Wananchi wanataka ustawi wao na jamii zao. Wanahitaji furaha, wanahitaji Uhuru, wamechoka kufokewa na kudharilishwa.

Ee Mungu, Sikia kilio chetu watoto wako tunaangamia!
 
Mtabweka Sana lakini Magufuli is there to stay yeye anatekeleza maagizo ya ilani ya CCM hafanyi yake anaungwa mkono na chama ndio maana alipitishwa na mkutano mkuu wa chama kwa asilimia Mia Moja tofauti na Lisu ambaye hata kamati kuu hakupita kwa asilimia Mia alikataliwa

Kukubalika ndani ya chama Huwezi linganisha Magufuli na Lisu

Lisu alipigiwa chini na wajumbe wengine hawezi tembea kifua mbele Kama Magufuli kwenye kukubalika ndani ya chama
 
Mtabweka Sana lakini Magufuli is there to stay yeye anatekeleza maagizo ya ilani ya CCM hafanyi yake anaungwa mkono na chama ndio maana alipitishwa na mkutano mkuu wa chama kwa asilimia Mia Moja tofauti na Lisu ambaye hata kamati kuu hakupita kwa asilimia Mia alikataliwa...
Kwa nini mliprint fomu moja. Mngeruhusu wanaccm wengine wachukue fomu, ndo mngejua maana ya wajumbe
 
Huo ndio ukweli halisi ndio mana ata kwenye kauli mbiu ilikuwa ni chagua magufuli bt now ata hilo jina hawataki hta kulisikia, mzee baba umeharibu vibayaaaaaa.

Hamna jipya zaidi ya maendeleo ya vitu... Mtaani vyuma vimekaza, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii wanalia na TCRA, wanasiasa Cha Moto wamekiona, wafanyabiasaha wanalia na TRA, mahakama imekuwa mkusanya mapato, mfanyakazi hajui lolote.

Ni mengi kwa kweli.
 
Hamna jipya zaidi ya maendeleo ya vitu... Mtaani vyuma vimekaza, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii wanalia na tcra, wanasiasa Cha Moto wamekiona, wafanyabiasaha wanalia na Tra, mahakama imekuwa mkusanya mapato, mfanyakazi hajui lolote...
Ni mengi kwa kweli...
Structures hazijawahi kuleta maendeleo. Maendeleo yanahitaji watu, uongozi bora, na ardhi.
 
Back
Top Bottom