BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Bandari ya Fujairah na DP World ambaye ni mmoja wa waendeshaji wakuu wa bandari duniani, walikubaliana na kusitisha Mkataba wa Uendeshaji uliosainiwa mwaka 2005 kwa lengo la kujenga, kuendesha na kuhamisha (BOT) kupanua na kuendeleza Kituo cha Kontena cha Fujairah bandarini kwa ajili ya kubeba na kusafirisha makontena.
Pande zote mbili zilikufikia makubaliano hayo baada ya kukamilisha uhamishaji wa shughuli kutoka DP World kwenda kwa mamlaka ya Bandari ya Fujairah.
DP World iliripoti kupata faida ya Tsh. Trilioni 2.678 iliyotokana na umiliki wa hisa zake, ikiwa ni ongezeko la asilimia 27.6.
Ikumbukwe, Fujairah ni kati ya Falme zilizopo ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).