Mwaka 2020 tutafute pesa

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Wakuu inshort namshukuru Muumba japokuwa mwaka 2019 umeniishia nikiwa vizuri kiuchumi na vibaya kiafya.

Malengo yangu ya savings bado sijafunga hesabu mpaka tarehe 28 ya mwezi huu wa kwanza japokuwa zaidi ya asilimia 89 ya kiwango nilichopanga kusave kwa mwaka 2019 kimetimia.

Kikubwa mwaka 2019 umenifundi mambo mengi

•Ndugu sio mtu wa kumtumainia na kumuwekea nguvu kubwa maishani(wazazi wanatosha)

•Hakuna rafiki wa kudumu na hata rafiki unayemtegemea sana anaweza kukugeuka

•kutofanya mambo kwa mihemko(huu mwaka nimelizwa pesa ndefu sana kwa sababu ya mihemko na kuongozwa na tamaa

•Pesa ipo nyingi tu kikubwa ni mbinu na ubunifu wa namna ya kuipata.

•Asilimia kubwa ya watanzania hatuna akili kama alivyosema mzee mkapa
nimethibitisha(vijana wengi ambao hatujatimiza miaka 30 tunawaza sana mapenzi na vitu vya kijinga amabavyo haviwezi kutusaidia miaka ya mbeleni)

•usihangaike kuwaza watu wanawaza nini Juu yako,just grind it huwezi kumtosheleza kila mtu maishani,muda wako ni wa thamani sana kuwaza ujinga wapotezee.

Naandika haya nimesimama kuna biashara nimeenda kuifuatilia lakini mhusika ananambia nije kesho tena hapo unaona jinsi gani watanzania sio watu wa kutafuta pesa kwa juhudi yaani kuniandalia mzigo mpaka kesho? Duh! Bado tuna safari ndefu

Samahani kama haieleweki au haina mpangilio nimeandika harakaharaka bila kukaa chini kujipa muda wa kutosha(kwa sababu nimepata mood ya kuandika acha. Niandike)
Ila wakuu 2020 hakuna msamaha kwa umasikini tukaze
 
Hela sio ngumu,kikubwa ni kubuni mbinu ambayo itakuingizia pesa.
Watu wanakula
Watu wanavaa
Watu wanakunywa
Then hakuna anayepata hivyo vitu bure so why hela iwe ngumu?
Ishi beyond your means yaani kikubwa kilichobadilika kwa sasa na kinafanya watu waone maisha magumu ni kuwa hakuna MTU anayejali sana kuhusu mwingine mpaka serikali nayo imeanza kuwa hvyo,
Cha kufanya fight kivyako its you are life no one care about you wala hakuna MTU atakayetoka from nowhere kuja kukusaidia kuboresha maisha yako.
Pambana kadri ya uwezo wako usiache hata mia mbili ikatishe mbele yako tumia akili kuipata.
Kama una wazo au idea usisubiri kesho time is now anza hata kwa kidogo ulichonacho usione aibu kwa watu au mademu mtaani kwenu watakufikiriaje ipo siku watakuelewa pia utakachopata usisahau kusave.
Pia jtahidi uwe angalau na chanzo zaidi ya kimoja cha kipato pesa utakayopata isikaae tu benk au Mpesa izungushe kuzalisha zaidi
Vp wale wenye kauli za kasema hela ngumu sikuhizi unawachukuliaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Metakeflin umeongea point nying sana daah mpaka kuziachia bila screenshots nimeshindwa.

Saf great thinker.

Sent from my U2 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika kitu kizuri sana hsa hapo ulopoandika usiache mia mbili ikikatiza mbele yako!😍😍!….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…