D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,399
- 3,666
Wakuu inshort namshukuru Muumba japokuwa mwaka 2019 umeniishia nikiwa vizuri kiuchumi na vibaya kiafya.
Malengo yangu ya savings bado sijafunga hesabu mpaka tarehe 28 ya mwezi huu wa kwanza japokuwa zaidi ya asilimia 89 ya kiwango nilichopanga kusave kwa mwaka 2019 kimetimia.
Kikubwa mwaka 2019 umenifundi mambo mengi
•Ndugu sio mtu wa kumtumainia na kumuwekea nguvu kubwa maishani(wazazi wanatosha)
•Hakuna rafiki wa kudumu na hata rafiki unayemtegemea sana anaweza kukugeuka
•kutofanya mambo kwa mihemko(huu mwaka nimelizwa pesa ndefu sana kwa sababu ya mihemko na kuongozwa na tamaa
•Pesa ipo nyingi tu kikubwa ni mbinu na ubunifu wa namna ya kuipata.
•Asilimia kubwa ya watanzania hatuna akili kama alivyosema mzee mkapa
nimethibitisha(vijana wengi ambao hatujatimiza miaka 30 tunawaza sana mapenzi na vitu vya kijinga amabavyo haviwezi kutusaidia miaka ya mbeleni)
•usihangaike kuwaza watu wanawaza nini Juu yako,just grind it huwezi kumtosheleza kila mtu maishani,muda wako ni wa thamani sana kuwaza ujinga wapotezee.
Naandika haya nimesimama kuna biashara nimeenda kuifuatilia lakini mhusika ananambia nije kesho tena hapo unaona jinsi gani watanzania sio watu wa kutafuta pesa kwa juhudi yaani kuniandalia mzigo mpaka kesho? Duh! Bado tuna safari ndefu
Samahani kama haieleweki au haina mpangilio nimeandika harakaharaka bila kukaa chini kujipa muda wa kutosha(kwa sababu nimepata mood ya kuandika acha. Niandike)
Ila wakuu 2020 hakuna msamaha kwa umasikini tukaze