Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala yangu ya Salaam za Mwaka Mpya, Imechapishwa kwenye gazeti la Nipashe la Leo.
Jana ndio tumeuanza mwaka mpya wa 2022, hivyo nianze kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya wasomaji wangu na Watanzania wenzangu, “Happy New Year”.
Wakati tukitakiana heri ya mwaka mpya, sio vibaya tukiutafakari kidogo mwaka uliopita wa 2021 kwa sisi Tanzania tumepitia wapi, tumekumbana na nini, tumejifunza nini hivyo mwaka huu wa 2022, tunatakiwa kufanya nini.
Kwa kuanzia, mwaka 2021 ulikuwa ni mwaka wa majanga, tumeuanza mwaka huku tukikabiliwa na janga la Corona, ambalo sio tuu tumewapoteza wapendwa wetu wengi, bali pia miongoni mwao, pia tumewapoteza viongozi wetu na sio tuu kupoteza nguvu kazi ya taifa, bali kuathiri shughuli mbalimbali za maendeleo na zinazotupatia kipato, sekta ya utalii ikiwa ni moja ya wahanga wakuu wa athari hizi za janga la Corona.
Mwaka 2021, tarehe 17 Machi, tulimpoteza kiongozi wetu mkuu wa taifa letu, rais John Pombe Magufuli, ukiondoa msiba wa kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, msiba wa JPM, ndio msiba mkubwa wa kwanza kwa taifa letu kwa mkuu wa nchi yetu kufariki dunia, akiwa madarakani.
Japo tulitangaziwa sababu ya kifo chake, ni ugonjwa wa moyo, lakini kiukweli kabisa, mazingira ya usiri wa kuugua kwake, toka alipoonekana mara mwisho Februari 22, na kufuatiwa na minongono ya kuna kiongozi anaumwa, ila inafanywa siri, mara tukasikia hivi, mara vile, lakini hatimaye Machi 17, 2021, ndipo Makamo wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akalitangazia taifa habari za msiba huu mzito, na kiukweli ni habari za kushtua sana.
Japo yaliyopita sii ndwele na muda umepita, ila haijalishi ni muda gani utapita, lakini Watanzania, bado wana haki ya kuambiwa ukweli kupitia kifungu cha “the right to information”, kwenye katiba yetu, ni nini haswa kilichopelekea usiri ule?!.
Kama ilivyo kila lenye mwanzo, pia lina mwisho, vivyo hivyo kwa binaadamu wote, tangu ile siku anazaliwa, inajulikana wazi, kuna siku itafika na atakufa, kila mtu atakufa, siku yake ikifika ni imefika, atakufa tuu, hata mimi nitakufa, wewe utakufa na sote tutakufa, hivyo kifo kipo, tatizo na mshtuko sio kwa nini fulani amekufa, bali mazingira ya kifo ndio kitu kinachostua, mtu mlikuwa nae, mzima, hamkupewa taarifa zozote za kuugua chochote, halafu akawa haonekani, hamkuelezwa chochote, kuja kulezwa tuu kuwa JPM amekufa, hata ungekuwa nani ni lazima ushituke.
Kwa vile kuzaliwa, uhai ni kifo ni vitu vilivyoko kwenye mamlaka ya juu kuliko uwezo wetu, hatuwezi kuuliza sababu, bali tunaweza kujadili yatokanayo. Hivyo kifo cha JPM ni moja ya janga kubwa sana lililolikumba taifa letu mwaka 2021 kuhalisha kuuita mwaka 2021 ulikuwa ni mwaka wa majanga kwa Tanzania.
Kwa vile mpangaji ni Mungu, ndiye aliyetuletea JPM na kumfanya kuwa rais wetu, na ni Mungu aliyemchukua JPM, na sasa rais wetu ni Mama Samia, hivyo hayo ni mabadiliko yaliyofanywa na Mungu mwenyewe kwa Tanzania, ina maana aliyamua kufanya mabadiliko ya uongozi Tanzania ni Mungu, hii inamaana Mama Samia, sasa ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania ya sasa.
Japo kifo cha JPM ni majanga, ila pia kimeleta mabadiliko ya kumuingiza Samia, sio kila majanga, ni majanga majanga, majanga mengine ni “blessing in disguise” kuna baadhi ya misimamo ya rais Magufuli kuhusiana na baadhi ya issues, ukiwemo msimamo wake kuhusu ugonjwa wa Corona, hivyo Mungu akaamua kumuita kwake ili kuleta mabadiliko, na kweli Samia amebadili msimamo, hivyo sasa ni jukumu letu sisi Watanzania katika umoja wetu, kwenda na mabadiliko chanya yoyote, hivyo mwaka huu wa 2022, uwe ni mwaka wa mabadiliko, Watanzania tubadilike.
Happy New Year.
Paskali