OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Nawasalimu kwa jina la aliye juu wakulima wenzangu.
Nasimama hapa kutangaza rasmi kwamba 2023 nitafia shambani. Nimejiridha pasipo na shaka kwamba mali utaipata shambani.
Kwa hiyo 2022 nimeitumia vizuri kujiandaa na kutafuta mtaji. Nasema nitafia shambani nikijiamini kwa sababu ya maandalizi niliyofanya. Nimekuwa na zana zote muhimu za kilimo. Trekta 2 ndogo 2WD zipo tayari mguu sawa,moja ikiwa ya kulima vibarua ili mapato yake yanisaidie kuhudumia mashamba kwa ufanisi wa hali ya juu. Ile ya pili sasa itakuwa kwa ajili ya mashamba yangu tu. Tayari harrow na planter vimepatikana. Hakuna kupanda kienyeji. Ni kitaalamu tu.
Upande wa mashamba naona ni gharama sana kuyamiliki. Zimepatikana ekari 120 Singida changamoto shamba ni pori linahitaji kusafisha. Nimeziweka kiporo mwakani. Kwa hiyo mwaka huu nitakodi tu.
Kwa kuanzia nimekodi ekari 150 katika mikoa miwili tofauti. Ekari 100 zao moja ekari 50 zao lingine. Gharama za kukodi bado chini sana 40,000- 50,000. Tayari amepatikana bwana shamba ampaye nitaingia naye partnership ya mwaka mmoja kwa asilimia fulani ya mapato yote. Yeye kazi yake ni kusimamia tu kulingana na utaalamu wake. Mimi nitamuhudimia kila kitu.
Kingine nimechagua sana kutumia teknolojia. Ukiwa na hela kidogo mambo mengi yanarahisishwa na teknolojia. Kupalilia mashine zipo, kufukuza ndege mashine zipo, kupanda na kuweka mbolea zipo. Kupiga dawa nk.
Kinachobaki hapo ni kumuomba Mungu tu ashushe mvua nzuri kustawisha mazao. Mimi ni mzuri wa Risk Management, nimeona kulima mazao yanayistahili ukamu kama dengu, mtama na alizeti.
Kwa hiyo kwa upande wangu nimejitahidi na nitajitahidi sana tu, sehemu iliyobaki ni ya Baba wa Mbinguni. Wakati mvua inanyesha wewe unafurahi kupata maji ya kunywa, mimi nafurahi kuvuna maekari.
Huu ni uzi ni kwa ajili ya watu wanaoamini kufanikiwa wakimtanguliza Mungu huku wakifanya kazi. Sio wale wanamlilia Mungu bila kufanya kazi wakiamini kwenye miujiza ya bila kazi. Sio wale wakatisha tamaa kwao kila kitu kigumu.
Hatutajadili stori za kukatishana tamaa. Haimaanishi kwamba hakuna changamoto, basi tulete changamoto na mbinu za kutatua.
Kifupi 2023 tupunguze maneno meengi na ngonjera tufanye kazi.