Mwaka 2023 nitafia shambani, eeh Mungu nisaidie!

Tunakushukuru sana kwa kutushirikisha hili, tunakuombea kwa Mungu ufanikiwe ktk utendaji huu, juhudi zako ndio mafanikio yako, mtumainie Mungu nae hata kuacha utange tange ktk hiyo ardhi. Barikiwa sana.
 
Hongera sana kwa maamuzi na utekelezaji.

Pamoja na kuchagua mazao yanayostahamili ukame, nakusihi sana tena sana kwa moyo wote, -kwa uzoefu na hasara niliyowahi kuipata katika safari ya kilimo-, tafuta mashamba yenye vyanzo vya maji, au laa vuna maji ya mvua kwenye mabwawa ya kutengeneza/kuchimba.

Kilimo cha kutegemea mvua tu bila kuhifadhi maji ni sawa na kubeti.

Tunza maji hata ekari moja kila shamba (at least nusu eka kila shamba) umwagilie kuanzia mvua zitakapokata hadi maji yako yatakapomalizika utanishukuru kwa matokeo ya kilimo chako.

NB: ukifanikiwa kuchimba maji usiruhusu wafugaji watumie maji yako yatakauka haraka sana.
 
Kila la kheri GT..

Usisahau kuleta mrejesho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mkuu

Moja ya lengo langu 2023 ni kutafuta mtaji wa kueleweka, 2024 nitafia shambani
 
Kama mali zinapatikana shambani waarabu wasingekuja iba twiga

Kama mali zainapatikana shambani wazungu wasingeijia madini

Kama mali zinapatikana shambani wahindi koko wasinge miliki maduka

Kama mali zinapatikana shambani wangetoa mikopo ya wakulima ila wanatoa ya wafanyabiashara wadogo wadogo

Kama mali inapatikana shambani kusingekua na njaa nchini, kila mtu angelima

Nakushauri Kilimo cha mvua hutapata mali shambani utapata presha.
 
Huku kanda ya kati kilimo cha alizet msimu ujao kitakufa, bei ya mafuta imeporomoka vibaya SIRIKALI imeruhusu mabwanyenye kuingiza mafuta mbadala kutoka nje ya nchi.
Mama ameshindwa kulinda viwanda vidogo vidogo vya ndani, sad!!!.
Kununua Lita kwa 8500 ili tukulinde wewe ni ubati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…