Mwaka 2024 usiache mtu mwingine aendeshe maisha yako

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Maisha yetu wakati mwingine hukabiliwa na mikwamo mingi sana inayotokana na kuwaachia watu wengine kuendesha maisha yetu.

Mwaka 2024 uwe ni mwaka wa kukataa watu wengine kuendesha maisha yetu.

Kama unataka kumuomba Mungu juu ya Maisha yako, omba mwenyewe Achana na kubebeshwa vitu na unaowaamini kuwa Wana nguvu ya kukuombea.

Kama mahusiano yako yanasumbua, wewe ndiyo wa kuamua kubaki ama kutoka bila ya kujali wengine wataonaje.

Pamoja na vigezo vya kijamii, mwaka 2024 wewe mwenyewe weka vigezo vyako utakavyotumia kupima mafanikio yako.

Acha kutegemea wengine kuendesha maisha yako!!
 
Shida Kuna wengine Maisha yao ni sawa na complementary goods yaani uhitaji wa bidhaa moja unategemeana na nyingine.

Mfano gari na petrol kwahyo hata iweje lazima watakubali tu kuendeshwa maana hakuna jinsi kinyume na hapo Maisha yao yatakuwa magumu.

Machawa ujumbe utawaudhi huo maana bila kuendeshwa hawali [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Machawa hawajauona huu ujumbe😁😁😁
 
Ongeza sauti
 
Kweli kabisa mkuu! Naona wale waliokuwa wanajiita watumishi wa Mungu kumbe matapeli wakihaha mitaani kwa njaa kwasababu watu wamewashtukia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…