Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Rafiki yetu 2024 ndio anatuaga leo anakwenda zake,tulikuwa nae pamoja na changamoto za hapa pale lkn baadhi yetu hawakupata bahati ya kuwa hai mpaka leo na wengine masaa haya machache yaliyobakia huenda tukatoboa au tusitoboe hakika uhai ni miliki ya Allah
Mwishoni mwa 2023 nilihitimisha na uzi wa TUAZIMIE KUACHA KUACHA KUANGALIA FILAMU ZA NGONO
Azimia kuacha kuangalia video/picha za ngono 2023
Watu Wana malengo mengi Sana kila mwaka mpya ukianza na mengine ni Makubwa mno hata hayatekelezeki hata katika ndoto kwasababu hakuna ajuaye kesho yake, ingawa hii haitufanyi tusiache kuweka malengo. Ndugu zangu ili tufanikiwe basi tunahitaji Sana msaada wa Mwenyezi Mungu, kwani si akili zetu...
Hope baadhi yetu tulikula kiapo hicho na tukakomaa nacho hatuna budi kujipigia makofi hakika kongole kwetu sote tumeushinda huo uraibu na kuuponya ubongo wetu na kuwa mbali na tabia ya kupanda mnazi kwa mkono mmoja,maana porn mwenzake ni masterbation
Mwaka huu ambao tutaingia hivi punde inshallah tuazimie kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zetu,hakika tutaepuka magonjwa yasiyo ambukiza kama presha,kisukari na mengineyo ambayo yanapatikana kutokana na mtindo wetu wa maisha
Lakini tukijikita zaidi kwa kufanya mazoezi ya kutembea kama hatua 10,000 kama anavyosema Doktori Janabi naamini kabisa tutajenga afya zetu,kuna jogging na mazoezi mengine ya viungo mbali mbali
Kwasisi wazee ambao tupo kwenye miaka 40 hasa sisi wanaume itatusaidia pia kuepukana na matatizo ya tezi dume,wataalamu wanasema kufanya mazoezi kunasaidia sana kuepukana na matatizo haya
Pasina kusahau afya yetu ya uzazi,wanaume mazoezi kwetu ni muhimu kuimarisha mzungumko wa damu na matokeo yake tunapokuwa kwenye mambo yetu ya sita kwa sita tusizingue,amini nakwambia hakuna mwanaume mwenye matatizo ya nguvu za kiume ni kubadilisha mtindo wa maisha,acha pombe,kula vizur na piga tizi sana utakuwa vizur sana,mazoezi ya kegel usikose yanasaidia chuma kusimama imara na kwenda mbio ndefu
Kwa ujumla tujenge utamaduni wa kufanya mazoezi ni bora sana kwa afya zetu,usifikirie utaanza lini bali anza sasa,anza hata kwa hatua 3000 za kutembea au anza kwa kukimbia mita mia tu,hiyo itakupa hamasa ya kufanya zaidi na zaidi
Tambua mazoezi ni kwa ubora wa afya yako mwenyewe
Happy New Year
Ni hayo tu!