Mwaka 2060 watu watakua na uwezo wa kusafiri toka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufikiria tu!!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Mwaka 2060 watu watakua na uwezo wa kusafiri toka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufikiria tu!!



Je utajisikiaje ikifika wakati unatoka Dar Kwenda Dodoma kwa kufumba na kufumbua macho tu kama ilivyokuwa kipindi Cha Nabii Suleiman 🤫....!!!!



Wanasayansi wako kwenye Utafiti wa kuleta Teknolojia mpya inaitwa Teleportation, tunaweza sema Ndoto ya baadaye ambapo Mtu ataweza kusafiri toka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufikiria tu.






Tumekua tukingaalia kwenye movie mbalimbali kama vile, vitabu vya dini, Matrix, star trik na movie zile sci - fi ya wagunduzi kuruka toka sehemu moja kwenda nyingine kupitia kufumba na kufumbua tu macho.




Watu walikua na uwezo wa kuingia chumba Fulani mahali na kutoweka kwa haraka hadi eneo la mbali limevutia sasa wanasayansi wanataka kuileta kwenye Maisha ya Uwalisia.



Lakini vipi ikiwa ndoto hiyo iko karibu kuliko tunavyofikiri? Kufikia 2060, maendeleo ya Teknolojia inaweza kuwa zaidi ya ndoto tu.



Shukrani kwa maendeleo ya Quantum pizikia (physics) Teknolojia hii itaweza kuwa mustakabali wa kuweza kusafirisha Mtu mahali popote duniani kwa sekunde kadhaa tu.



iwe kwa madhumuni ya kuabudu, kupatiwa matibabu, usafiri, kisayansi utaweza kupitia kufikiria tu utaweza kusonga Angani.

Credit to: #Bongotech255 #Nasa #astronomy



Je unafikiri itawezekana kuwasafirisha wanadamu kwenda sehemu nyingine kwa kufikiria tu 😳!!!!
 

Attachments

  • 4_20250309_014733_0003.png
    1.4 MB · Views: 1
Dunia ina mambo mengi sana yakufikirisha, hayo mambo unayoyasema mwaka 2060 yamekuwa yakifanyika toka enzi na enzi na mpaka sasa yanafanyaika kwa wanayoyaelewa hayo mambo.
 
Mwambie huyo mtu anayejaribu kuelezea jambo kama hili ajifunze kwanza kuandika maneno ya kiswahili (au lugha yoyote anayoitumia) kwa ufasaha kwa sababu kushindwa kuandika kunafanya wasomaji wachukulie kuwa ni kilaza asiyejua lolote. Nimekutana na neno ''unazani'' badala ya ''unadhani'' nikaacha kusoma.
 
Hii inafanyika na ipo Ila kinachofanyika ni kuiweka katika Physical touch
 
Sumbawanga na kule gamboshi hiyo sio teknolojia mpya!!
 
Chochote unachoweza kufikiri kipo,kilichobaki ni kukitoa katika wazo na kuwa kila halisi (tangible).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…