Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 2,833
- 8,777
Mimi sio mchambuzi wa soka,sio mtabiri wala sio mganga,Bali ni mtu ninaependa kuangalia mambo kwa kina.
Sababu zinazonifanya nione kabisa kua, safari hii na mwaka huu wa 2025,ni mwaka wa Simba kutwaa kombe la shirikisho ni hizi:
Ni kweli Simba bado inajenga timu,hili wala hakina ubishi.
Lakini amini nawaambia Simba inakomaa na kuimarika Kila siku kutokana na kucheza mechi ngumu za ndani na za nje.
Timu za ndani hua zinaipania sana Simba,lakini kupaniwa huko ndio hua Kunaiimarisha sana Simba.
Hali hiyo hupelekea Simba kuona kua Kila mechi kwake ni Fainali.
Simba imekua kama ina bahati mbaya inapopangiwa timu za nje, hujikuta imepangwa na timu ngumu,ingawa huishia kusema Iko tayari kucheza na timu yoyote,tofauti na Yanga ambao husherehekea Kwa vile hupangwa na timu dhaifu.
Hivyo Simba imejiwekea spirit ya kucheza na timu yoyote hapa Afrika.Na hii ndio Siri Yao ya ushindi.
Simba itacheza fainali na RS Berkane.
RS Berkane imekua ikizifunga magoli mengi timu pinzani katika michuano hii,na hili ndio kosa kubwa la Berkane.
Kwa sababu,Simba imeshajua kabisa nguvu ya Berkane ni kuzifunga magoli mengi timu pinzani,,kwa hiyo Simba itachukua tahadhari na kujipanga kukabiliana na Hali hiyo.
Ni ukweli usiopingika kua, Simba hua haiogopi timu yoyote ya haba Afrika kwa sababu Simba imeshacheza na timu nyingi kubwa na gumu sana zaidi ya hiyo Berkane,hivyo Simba haiiogopi zaidi ya kuiheshimu.
Simba Hadi kuingia fainali imezitoa timu nyingi sana,licha ya kua bado inajenga timu.
Kwa kuzitoa timu zote hizi,imeimarika,imekomaa na imeiva.
Licha ya kwamba, Kuna watu wanaiona Simba hii ya 2025, kama Simba yenye wachezaji wasio na kile wanachokiita wao low Quality, lakini ukweli ni kwamba, namba hazidanganyi.
Simba hii hii wanayoiona Haina wachezaji wenye ubora ndio imeingia Fainali.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza utaanza kuchezwa Morocco,na mchezo wa pili utachezwa Dar es salaam.
Pamoja na Tabia za soka kua,timu inaweza kufungwa kwao lakini mara nyingi, Simba hua inauwezo wa kufanya vizuri sana nyumbani.
Sioni kwa Nini Simba izembee mara ya pili kwa kuruhusu kupoteza mchezo nyumbani siku ya fainali kwa mara ya pili.
Simba hii sio ya kufungwa goli nne na RS Berkane huko Morocco,
Lakini pia Simba hii Ina uwezo wa kushinda nyumbani.
Baada ya Yanga kucheza fainali katika michuano hii hii na kuanza kuwadharau,kuwacheka na kuwa tania Simba Kwa kuishia robo,ambao kwa hakika Simba ni role model wa Yanga na waalimu wao.,nayo hii ndio sababu nyingine iliyowahamasisha Simba kujibu mapigo.
Uhakika uliopo Kwa Simba ni kwamba,watapata medali,lkn ili kuwanyamazisha yanga,Simba watafanya juu chini kuhakikisha wanapata taji kubwa zaidi ya medali ambalo yanga hawajapata.
Hivyo Simba watafanya Kila wawezalo kutwaa kombe.
Bahati Kwa Simba ni kwamba mechi ya kwanza itapigwa Morocco na mechi ya marudiano itapigwa Dar es salaam.
Kombe litaletwa hapa kwa ajili ya kuja kukabidhiwa kwa mshindi wa mechi zote mbili.
Kitendo Cha kombe kutolewa hadharini siku ya fainali, nayo ni chachu nyingine ya Simba kupambana ili kulibakiza hapa nyumbani.
Mwaka 1993 kombe lililetwa hapa pia lakini Simba ilifungwa goli mbili bila na Stella Abidjan ya Ivory coast baada ya Simba kutoka bilabila huko Ivory coast.
Kwa Historia hiyo yenye maumivu, sioni Simba Kukubali Tena kurushusu maumivu kujirudia.
Mbali na hivyo, Bali pia itakua ni muda sahihi wa kuionesha Yanga kua Simba daima imeitangulia Yanga katika maendelea ya soka la kimataifa, na kuionesha Yanga kua, Simba siku zote Iko mbele ya Yanga,kwa kulitwaa kombe hili.
Mara nyingi timu yoyote ikiingia hatua ya fainali,na hususani mchezo wa mwisho au wa marudiano kufanyika nyumbani,mechi hizo huchukua sura za Kitaifa.
Serikali huiona Club ikiwa na hadhi ya timu ya"Taifa"
Kwa muktadha huo serikali haitaiacha Simba peke yake.
Wanasimba wenzangu Simba na RS Berkane zinalingana nguvu lakini pia:
Nyota zinaiangazia Simba,
Namba zinaipa Simba,
Wakati unaibeba Simba,
Geographia inaibeba Simba
Simba Ina wachezaji wenye ubora na ndio maana wameingia fainali.
Ndugu zangu Naiona Simba ikibakiza kombe Tanzania.
Ingawa natambua kabisa kua, hakuna fainali rahisi.
Naona Mungu safari hii Yuko upande wetu.
Simba itatwaa kombe la shirikisho 2025.