ZINJANTHROPAZ
JF-Expert Member
- Aug 6, 2023
- 287
- 470
Mimi si mpenzi wa kuongea au kuandika mambo bila hata kufanya utafiti kidogo.
Ukweli ni kwamba mwaka huu, CCM imepoteza mvuto kwa kiwango kikubwa, na sijawahi kushuhudia hali kama hii hapo kabla. Angalia hata umaarufu wa matukio haya mawili: uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM pale Dodoma na uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA pale Mlimani City.
Tofauti ni kubwa, na ukiondoa wasanii wa vichekesho na Bongo Fleva ambao walikuwa wakipost mambo yao na kuonekana wako pale, hakuna kingine kilichovutia sana.
Hata hapa JF, threads nyingi zimekuwa zikihusu uchaguzi wa CHADEMA, na mpaka sasa mshindi kapatikana, lakini mijadala bado inaendelea kwa moto. Kiukweli, tangu nikiwa mtoto, sijawahi kuona kitu kama hiki.
Hongera sana Tundu Antipas Lissu, na pia hongera sana Freeman Mbowe kwa kutekeleza katiba ipasavyo.
Nitoe rai kwa CCM: wajifunze kutoka kwa wenzao.