Mwaka mmoja baada ya kuuawa kwa Jenerali Qasem Soleimani: Iran yaapa kulipiza kisasi, Marekani yajihami

Mwaka mmoja baada ya kuuawa kwa Jenerali Qasem Soleimani: Iran yaapa kulipiza kisasi, Marekani yajihami

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Umetimia mwaka mmoja tangu kuuawa kwa Kiongozi wa ngazi ya juu wa Jeshi la Iran, Brigedia Jenerali Qasem Soleimani, aliyeuawa kwa shambulio la ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani alfajiri ya Januari 3, 2020 mjini Baghdad nchini Iraq, akiwa na Abu Mahdi al-Muhandis, kiongozi wa kundi la Kata'ib Hezbollah, tawi la kundi la kijeshi la Hezbollah lenye mafungamano na Iran.

Qassem-Soleimani.jpg


Kama sehemu ya kumuenzi, kumekuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu iliyodumu kwa takriban wiki moja sasa katika maeneo kadhaa ya mji wa Tehran, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uturuki, Anadolu. Mikutano ya hadhara inafanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran, ikihudhuriwa na wanasiasa na viongozi wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran pamoja na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati.

Mmoja ya wazungumzaji katika tukio hilo ni Jaji Mkuu wa Iran ambaye pia alikuwa mgombea wa Urais, Ebrahim Raeesi. Raeesi amesema Marekani inangoja "kisasi cha nguvu kwa uhalifu iliotenda," akimuonya Rais wa Marekani anayemaliza muda wake, Donald Trump kuwa asijione kuwa na kinga na kuwa wote "waliotenda uhalifu huo hawatakuwa salama popote duniani."

Mrithi wa Jenerali Soleimani na kiongozi wa sasa wa Jeshi la Quds, Esmaeil Qaani amesema kuwa kifo cha Jenerali Soleimani kinaweza kulipizwa kisasi na watu "ndani ya Marekani."

Rais wa Iran, Hassan Rouhani, amesema siku ya Alhamisi kuwa kuuawa kwa Jenerali Soleimani ni "uhalifu usioweza kusamehewa" akiongeza kuwa kisasi kitaamuliwa kwa wakati sahihi.

Wakati hayo yakijiri, Marekani imesema kuwa inajiandaa kwa lolote litakalotokea, ikituma ndege mbili za kivita aina ya B-52 kutoka kambi ya kijeshi iliyopo jimbo la North Dakota katika juhudi za kuonesha uwepo wake wa kijeshi Mashariki ya Kati na kujaribu kuitishia Iran, kwa mujibu wa The Washington Post, huku Rais Trump akisema kuwa kuna "fununu" za kuwepo kwa mashambulizi zaidi dhidi ya Wamarekani nchini Iraq, akiionya Iran kuwa itawajibishwa kwa lolote litakalotokea.

Kufuatia kuuawa kwa Jenerali Soleimani mwaka jana, msuguano baina ya nchi zote mbili ulikaribia kiwango cha kuingia katika mgogoro wa kivita baada ya Iran kufyatua kombora lililowajeruhi zaidi ya wanajeshi 100 wa Marekani na kuharibu miundombinu katika kambi ya Marekani nchini Iraq siku tano baada ya kuuawa kwa Jenerali Soleimani. Hata hivyo, kumekuwa na ongezeko la msuguano katika siku za hivi karibuni baada ya ubalozi wa Marekani kushambuliwa kwa roketi mjini Baghdad na kundi la kijeshi la Iran, Ashab al-Kahf kukiri kuhusika.

Iran imeapa kutokata tamaa hadi pale haki itakapopatikana, ikisema kuwa Marekani imeingilia uhuru wa Iran na kuvunja sheria za Kimataifa kutokana na kuuawa kwa Jenerali Soleimani.
 
Iran mikwara mingi action sifuri

Akifanya action basi lazima iwe off target
 
Huyu Jamaa alikua Mwamba sana

Sema alipenda shoo shoooo

Akajiachia sanaaaaa


Akajisahau akidhan sasa Iraq ni Iran


ameisaidia Iran Kujitanua, Pengo lake halitakaa kamwe kuzibwa !!
 
Back
Top Bottom