Mwaka mpya, fursa mpya. Tuchukue hatua kupata matokeo

Mwaka mpya, fursa mpya. Tuchukue hatua kupata matokeo

Joined
Jan 9, 2026
Posts
7
Reaction score
20
SALAMU ZENU??
Hii thread ni ndefu ila we isome tu uimalize kwa manufaa yako

📢📢.HAYA kwa zaidi ya miaka 17 niliyokuwepo Jamii forum nimejifunza mambo mengi sana, nimekutana na mawazo ya kila aina, watu wenye mitazamo na maoni ya kila aina, fursa za kila aina na ndipo nikagundua kumbe watu ni fursa na fursa ni watu, yaani tunajifunza mambo mengi kupitia watu na tunapenyeza fursa zetu kwa watu hao hao (CIRCLE GAME)

Sasa basi kwa utashi wangu na akili ya kawaida nimegundua watu wengi wanasumbuliwa na matatizo ya aina gani, kiuchumi, kijamii na kiafya ndipo nikaamua kurudi upya kwa ACCOUNT hii ya kutatua changamoto hizo ambazo nina uhakika wa solution zake.

Miaka inakwenda, umri wa vijana unazaidi kwenda lakini maisha yao bado ni yale yale, na wengine maisha yakizidi kuwa ya hovyo zaidi, wengine afya zao zikizidi kudhorota kwa kukosa suluhisho la matatizo yao.

What next? Nimekuja na suluhisho, mwaka huu wewe unayejiona hutaki kubaki ulipokuwa mwaka jana na unataka kuinuka Kwa namna fulani, huku huoni mwanga wa kuona mbele, nakuletea fursa mbalimbali.

Mwaka 2026 jifunze skills mpya haijalishi una experience na mambo kadhaa ambayo hayajakupa matokeo chanya, kubali kupoteza ulichokipoteza, kubali kuanza upya, nakuletea fursa mpya hasa wewe kijana unayejitafuta lakini huoni mbele
👉Fursa ya kujifunza ujasiriamali wa kisasa, kupitia uwekezaji wa Shamba eeeh shamba mnaogopa nini?, ufugaji wa mifugo inayorudisha faida kwa kipindi kifupi, jinsi ya kupambana na changamoto za magonjwa kwa mifugo, changamoto za mbegu bora, suluhisho kwa changamoto za hali ya hewa ktk uwekezaji wa shamba.

👉Fursa ya biashara mtandao/digital marketing, hasa kwa kizazi hiki cha Gen-Z ambacho internet ndio msingi wa kila jambo, kupitia internet unaweza kupata taarifa za masoko na biadhaa mbalimbali dunia nzima bila ya mtu kati, na kwa mtaji mdogo unaweza kuwa sehemu ya wafanya biashara wanaoingiza faida nzuri kama utaenenda sawa na mahitaji ya dunia.
✍️...Sasa kwa angle hii nataka niwape vijana fursa ya kujifunza kiundani nini maana ya mitandao ya kijamii, manufaa yake ni yapi?, na kwanini ushinde njaa wakati una smartphone, na bando unalomaliza kutizama pornograf na maudhui ya kipuuzi, kwanini usiitumie internet kukupa faida?.
✍️..Ktk internet kuna fursa nyingi makumi Kwa makumi, kuanzia kwa wenye elimu ya juu mpaka kwa wale wa standard 7 failure, muhimu ujue kusoma/kuandika na kingereza cha kuombea maji.

Mfano kwa wenye elimu ya kawaida standard 7- form4 hapa panawafaa 👉 contents creation
👉products advertisement
👉 AI training kwa sasa hii ndio iko moto,
👉tourism marketing orientation,
👉 QA& Websites/software testing,
👉 Opinions+feedback surveys.

Na kwa wenye elimu ya certificate, Diploma, Degree+, kuna fursa za
👉 web3 jobs hapa ndipo unazikuta fursa za cryptocurrency/digital assets trading& investment,
👉web3 technical writer,
👉researcher(trends analysis, market reports writing),
👉Digital fashion creator,
👉NFT project management,
👉Core blockchain development
👉Trading (fiat currency based+digital assets exchanging).

Nje ya web3 kuna 👇
👉Data scientist-data entries, software Eng, Software dev, Network administrator, Cybersecurity analysis, na wale wote ambao wako interested kwenye tech innovation dev's impacts na wana ujuzi wowote you're welcome, kuna fewer Camps zina hire watu wenye ujuzi wa aina hii chamsingi uwe makini, fursa ni nyingi hakuna kulala.

✍️...La mwisho kama nilivyoandika mwanzo nimekuja na suluhisho kwa matatizo mengi ya kiuchumi na kijamii, kama unajijua mapenzi yamekuwa yakikuhangaisha, humpati umtakaye either kwa udomo zege wako, uvivu wa kutongoza, aibu, kukosa pesa(sio sababu), kuna suluhisho lako, pia kwa wale jamaa/wanawake wenye ubize na mbanga za kutafuta pesa mpaka wanasahau kuna mahusiano lkn wanahitaji mtu tu wa kuhang nae kwa muda mfupi kujiliwaza, pia kuna suluhisho lenu, acha kupoteza muda kutafuta watu wasiokutaka njoo nikupe chaka,

✍️...Na kuna wale akina dada/kaka wanaochoshwa na tabia za kusimama njiani kusaka madanga/malaya ili watimize haja zao, pia kuna suluhisho lao, sijawasahau wazee wa mishangazi/mibaba pia nina suluhisho lenu.

🚨.Naposema suluhisho namaanisha Connection ya wewe na huyo umtakaye,

✍️...Mwaka 2025 ulikuwa na mambo mengi lakin 2026 utakuwa mwaka wa mchaka mchaka full kukimbizana na fursa vijijini, mijini mpaka nje za nchi, muhimu pesa iingie mfukoni, hakutokuwa na msalia mtume tutapita na fursa zote, sitoishia hapa, Account hii pia itakuwa ikitoa mawazo magumu yenye MATOKEO CHANYA kwa wenye maswali waliyoshindwa kujibiwa kwa muda.

📢.. Nimerudi kivingine, kuanzia sasa nitakuwa namwaga THREADS kila siku Mpaka kufika April-May kuwe na watu waliopata mwanga, marufuku kulia kisa mahusiano, marufuku kulia kisa hujapata kazi, huna mtaji sijui hujui usome nini, mambo yameiva kaa tayari.

🚨🚨Note...kwa wale wote wenye michongo tafadhali msikae nayo kimya mkala pekee, tuelezane na kugawiana fursa tumechoka kupewa ushauri tunataka tugawane fursa kila mtu akale pesa zake, ushauri hauleti pesa zaidi ya kusisimua moyo na faraja ya muda, 2026 toa mchongo ushauri peleka ZAHANATI.

Soon naleta mboga, ugali mnao tayari
 
Back
Top Bottom