Mwaka mpya niliulia Cello ya Police

Mwaka mpya niliulia Cello ya Police

Wadau wasalaam.Toka nizaliwe sijawahi kulala Police ila tarehe 2 nililala. wadau pale nilivua viatu na nikakaguliwa nikawakuta jamaa wawili wakituhumiwa kuiba ndizi na kuku.
Wadau pale sakafuni palikua na baridi la kufa mtu na sio poa.
Ndugu zangu fanya yote ila pale sio poa yani.
Tarehe 3 nilipata dhamana nikatoka ila mpaka sasa kisaikolojia sipo sawa wadau.
Kosa ni mambo ya kusherehekea kupita kiasi na kuleta chaos kitaa.
Wadau Police sio poa

Ni kweli aiseee ,polisi kwa watu walionyooka na kuingia kwa bahati mbaya hapafai...huko panafaa waliopinda tangia mtaani.
 
Bado sijakuelewa mkuu
.
Ulifanya nini?
Alilewa kupitia kiasi akasheherekea kwa vurugu.
Kama sakafu ilikuwa baridi ndivyo inavyotakiwa kuwa.
Siye bila sababu Ile sehemu inaitwa "The Cooler",mahali ambapo hasira Kali zinapungua.
Au furaha zilizopitiliza.
 
Mwanetu we unaonekana mdebwedo (mchelemchele) kwa sana yaani kulala siku 1 police post ndo una stress sasa ungeenda staki shari au segerea si ungeliwa kiboga bila woga wewe halafu ungeludi mweupe peeeeeeh
 
Unasherehekea mpaka unaleta fujo! Uzuri siku za sikukuu doria za POLISI huongezwa.
Siku nyingine jifunze, fujo za baani na ugomvi wa hovyo havifai.
 
Back
Top Bottom