Mwaka Mpya Uwe Upya wa Utu Wetu!

Mwaka Mpya Uwe Upya wa Utu Wetu!

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,730
Reaction score
2,230
Naomba sana Mungu atupe neema ili katika mwaka huu mpya zisiwe mpya namba za tarehe, yaani Januari Mosi, 2021.

Bali tufanywe wapya, tuvae utu mpya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika roho zetu na kuufikia utakatifu wa kweli. Waefeso 4:22-24

Tuachane kabisa na matendo ya kimwili machafu na ya kifisadi. Tujiulize: bado tunasengenya, tunasema uongo, tunaiba, tunadhulumu, tunachukiana, hatusameheani, hatuna huruma, tunatukanana, tunadharau wengine, tunajikweza na kujitukuza, nk?!

Tutakuwa hatujaingia mwaka mpya, bali tunaishi utu wa zamani unaoharibika!
 
Back
Top Bottom