Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
- Thread starter
- #261
Ukitaka ujiajiri vizuri, wekeza kwenye kutengeneza na kuuza, na si kununua na kuuza (uchuuzi)Sawa, basi endelea kulalamika Mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukitaka ujiajiri vizuri, wekeza kwenye kutengeneza na kuuza, na si kununua na kuuza (uchuuzi)Sawa, basi endelea kulalamika Mkuu.
Wewe ni mzee wa miaka 60 tena kada wa CCM , Tabia yenu kubwa mnaendeleza mitazamo yenu ya miaka sabini katika Dunia ambayo imechukua uelekeo.mwingine , huwa hamtaki kukubali ukwelii mnasimamia msimamo wa miaka ile.Tatizo vijana ukweli hatutaki kuusikia.
Aliyeajiriwa anafanya kazi(anafungwa) kwa misingi na kanuni zilizoainishwa na mamlaka husika; hawezi kufanya ubunifu wake nje ya miongozo iliyowekwa.Nani kakwambia nimeajiriwa Mkuu? Au umejiamulia kuja na conclusion yako?.
Unakosea sana unaposema waliojiajiri ndio wagunduzi, huu ni ujinga wa hali ya juu Mkuu.
Mtu yoyote anayefanyakazi kwa bidii anayetaka maendeleo haijalishi ameajiriwa au kajiajiri anaweza kuwa mgunduzi.
Hivi unajua utofauti wa kuajiriwa sekta binafsi na serikalini ni ndogo sana na ambayo haiathiri ugunduzi wa mtu.
Tatizo sisi vijana wa kitanzania ni wavivu sana na walalamishi mno.
Inawezekana sisi wengine tunashindwa kutokana na mazingira tuliozaliwa au uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo, au labda tupo bado kwenye uendelevu wa 'evolution stage'Wengine wanafikiri kufanya biashara unahitaji akili ya shule kama degrees au uwe na mtaji mkubwa sana wa kuanzia biashara
Babu yangu hakusoma kabisa ila kwenye kurudisha chenji na kuendeleza mtaji alikuwa makini sana mpaka kumfundisha na mwanae (baba)
Leo biashara zinaendelezwa na wajukuu
Kuna mzee alikuwa anahojiwa biashara zao zilianza 1930s na 40s na sasa warithi wanakuja ila waendeleze View attachment 2877360
Wenye akili kubwa watakuwa wamekuelewaShida ya mbongo inakuwa hapa akisikia neno kujiajiri anafikiria ujasiriamali.
Wewe ni mwanasheria umefanya kazi ya kuajiriwa umekusanya pesa ya kutosha kwanini usiache ajira na kuanzisha Law firm yako, wewe Ni daktari ushajijengea jina watu wakakuamini kwanini usifungua kliniki yako na mdogo mdogo ikawa hospitali ukaajiri watu wengi , Wewe ni mhasibu na CPA yako kuliko kuendelea kuajiriwa kwanini usitoke kwenye comfrot zone na kuanzisha Auditing firm yako.
Kama raia tukiwa na mawazo haya nchi itapiga hatua, maana faida zake ni nyingi kwanza utaacha nafasi ya watu wengine kuajiriwa na wewe pia utaajiri , kuliko kusubiria kufa au kustaafu ili wengine wapate ajira.
Nchi ya Marekani yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 150 ni asilimia 18 tu ya idadi yote ya watu wameajiriwa serikalini na asilimia zote zilizobaki ni sekta binafsi na wengine kujiajiri.
Maana yake ni nini? , hata taifa kibwa kama Marekani halina uwezo wa kuajiri raia wake wote sasa Sembuse Tanzania ambayo ndio kwanza hata uchumi wa kati hatujafikia.
Ukishajiajiri na ukatoboa maana yake unaingiza biashara yako au Kampuni yako katika orodha ya sekta binafsi.
Wenzetu wamepiga hatua kwasasabu mitazamo yao ishabadilika muda mrefu lakini sisi ndio kwanza tunalumbana hapa kitu ambacho kipo wazi.
Yaani kuna wakati huwa nawaza na kujisemesha mwenyeweInawezekana sisi wengine tunashindwa kutokana na mazingira tuliozaliwa au uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo, au labda tupo bado kwenye uendelevu wa 'evolution stage'
Kwa sababu kujiajiri na kuajiri wengine ni mateso zaidi kuliko kuajiriwa hasa serikalini.kwa nini hatujiajiri huku mtaji ukiwa si tatizo?
Acha wakariri...hii ni Tz ambayo kila mtu ni mjuaji.Kujiajiri sio kwa kila mtu nyie.
Unahisi ni nini kichowafanya watu wasijiajiri?Acha wakariri...hii ni Tz ambayo kila mtu ni mjuaji.
Well..kwa sasa (nyakati hizi)Unahisi ni nini kichowafanya watu wasijiajiri?
Japo ni UKWELI MCHUNGU juu ya kula kwenu maisha wafanyakazi wa serikali ukilinganisha na kundi kubwa la vijana waliojiajiri.[emoji23][emoji2] Vijana mmekosa ajira mnaishia kujifariji kujiita wafanya biashara...
Nyie ni machinga tu mnao bangaiza maisha mpate pesa ya kula na kulipa kodi vyumba vya uani...
Watu wameajiriwa wanakula mishahara take home sio chini ya Million 1 na ana uhakika wa kupata Allowances kila wiki...
Wakati wew uliyekaa hapo umefungua kibanda cha kuuza juice urembo chupi na biscuits faida kwa mwezi haifiki Laki 1 [emoji23][emoji23]
VIJANA MSIDANGANYIKE HII TZ MTU ANAYEFAIDI MAISHA BILA STRESS NI MUAJIRIWA TENA WA SERIKALINI...
Anaenda kazin siku 5 kwa wiki, ana uhakika wa mshahara umeme uwake ukatike, jua au mvua inyeshe, hana hofu ya kufukuzwa kazi, anaenda likizo kila mwaka, akiumwa anapewa ruhusa bila kipingamizi, akifiwa hata na jirani haendi kazin...
Hivi hamjiulizi kwanini viongoz wengi wana ng'ang'ania madarakani..?[emoji23][emoji2]
Nasikia chadema wameandaa maandamano [emoji23][emoji2] watakao enda ni nyie vijana mnajiita wafanya biashara kwasabab hamna uhakika wa kula na kuishi kesho...
UKWELI MCHUNGU [emoji23][emoji2][emoji120]