Mwaka wa Tisa huu sijampiga wala kumnyooshea kidole Wakati kumtukana Binti Kimoso

Mwaka wa Tisa huu sijampiga wala kumnyooshea kidole Wakati kumtukana Binti Kimoso

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MWAKA WA TISA HUU SIJAMPIGA WALA KUMNYOOSHEA KIDOLE WALA KUMTUKANA BINTI KIMOSO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Miaka tisa siô mingi Sana làkini pia kwèñye mahusiano ya mapenzi hasa nyakati hizô siô miaka michache.

Katika miaka yote hiyo tumepitia mambo mbalimbali yaliyotujenga na yapo yaliyohatarisha penzi letu kuvunjika ukizingatia Sisi wote bàdo ni Vijana wadogo kama mjuavyo damu changa.

Lakini tupitapo katika njia ngumu au hekaheka tuliamua Upendo, Haki, Akili na kwèli (Utibeli) vitawele.

Kwèñye mahusiano yetu kama Vijana wadogo kîla mmoja wetu ana chanzo cha kuleta mgogoro.
Upande wàngu chanzo changu cha mgogoro kilikuwa ni HISIA, kama mjuavyo Sisi Wanaume tunatamaa. Hivyo kama walivyo Vijana Wengine wakiume kutamañi mabinti wengine na kuwatongoza au kutongozwa n wasichana au mashangazi ilikuwa changamoto kûbwa Sana làkini Mûngu alituongoza.

Sikutaka kumuumiza Mwanamke niliyempenda na aliyeonyesha kunipenda.
Ilifikia Wakati WA kulambishana viapo vya damu dadeki! Lakini nilishindwa kumficha kama mjuavyo Watibeli ni Wakweli.
Kiapo kilijikita kwèñye nadhiri ya kutoku-cheat Maisha yàngu yote. Mmmh!

Akaanza yeye kuapa, kisha zamu yàngu ikafika. Wakati anaapa Kwanza sikutegemea kama angeapa Kwa kiapo kile. Moyoni mwangu nikawa na mgogoro niape au nisiape.
Nikiapa nafsi yàngu Ipo wazi kuwa siwezi kuishi miaka yote bila ati ku-cheat. Hiyo ñîlijua haiwezeniki
Nisipoapa ataona simpendi. Dadeki.
Nifanye nini jàmani?
Kumbuka ni Vijana wadogo hata miaka 25 hawaijui huku Binti Kimoso Miaka 20 haijui.
Ulikuwa labda NI utoto lakini Kwa upande wàngu nilikuwa chuoni na nilishajiona NI mkubwa.

Niliapa au sikuapa? Hiyo NI Stori ya Siku ñyiñgine.

Binti Kimoso changamoto yake kûbwa ilitoka katika pande mbili, ishu ya kihisia na kiakili.
Kwa hîyo MIGOGORO àmbayo chanzo NI yeye Basi mingi Ipo kihisia Kwa kuhisi labda simpendi au kuhitaji kudekezwa, sîjui kubembelezwa na mûda wote niwe attention na yeye.
Changamoto za kiakili ni suala la usahaulifu wake wa mara Kwa mara.

Kuelewa chanzo cha migogoro ni hatua muhimu katika kutatua mizozo ndàni ya mahusiano na mapenzi. Yote haya tuliyafanya Kwa kuzungumza(mawasiliano)…

Mwanamke NI kama Mtoto. Binti Kimoso licha ya kuwa ni mpenzi wàngu lakinî kiumri NI mdogo kwangu Kwa zaidi ya Miaka mitano.
Mimi kwàke ni kaka, làkini pia ni Mwalimu wake. Hivyo anamambo mengi ya kujifunza kutoka kwangu na Mimi nilikuwa na machache ya kujifunza kutoka kwàke hasa mambo ya kihisia Kwa sababu Wanawake ni emotional entity.

Mimi kama Mkubwa na mwanaume ndiye niliyekuwa na wajibu Wa kuhakikisha namfanya Awe Huru îli hata kama anashida ananikuwa muwazi.

Nilimpa Uhuru wa kujionyesha vile alivyo bila kunihofia. Mwanzoni alihisi huenda NI mtego nimemwekea lakini kadiri Siku zilivyokuwa zinaenda aligundua nilikuwa namaanisha Kwa sababu mii mwenyewe sikuwa MTU WA kuficha tàbia zangu.
Yàani kiufupi asingepata nafasi ya kunichunguza Kwa sababu kîla kitû kipo wazi.

Nilimfanya awe muwazi yàani awe Huru. Siku Moja tumeenda kuzurura maeneo Fulani Mafinga, Iringa. Tukiwa tumechoka, mûda WA kupata lunch ulikuwa mbele yetu.
Nikamwambia tukale chàkula akasema fresh.
Tumefika mgahawani nikamwuliza anataka Kula nini akasema çhochote.
Nikamwambia awe muwazi asifikirie kuhusu mfuko wàngu unakiasi gàni.

Bado akasita. Akasema wali maharage huku akinipimishia, nikamuuliza utaenjoi huku nikijua tangu Mimi MTU hasa Mrembo aenjoy wali maharage. NI kama alikuwa ananitega, na Mimi NI mtegua mitego.

Mhudumu kaja nikamwagiza Wali maharage, na kinywaji alichoagiza alafu Mimi nikaagiza zangu Kuku choma na ugali wàngu. Chàkula kikaletwa. Nikampa wali maharage yake nami Kuku na ugali wàngu.
Mizozo ukazuka😀 baàda ya kuona nimemkaushia tunapiga stori yeye Akila wali maharage yake nami nikiendelea na chàkula changu. Uvumilivu ukamshinda akataka tule wôte. Nikamkatie kifinyango kiduchu🤪 akataka kukataa làkini alipoona ninakirudisha akanipokonya😀😀.
Kisha akanipokonya na ule mnofu mkubwa.
Taikon NI mtu masikhara na drama. Nikazusha mzozo WA uongo na kwèli wakaja wahudumu kutusikiliza.

Wakanichamba weee😊 làkini Mimi nikabaki Nadai mnofu wàngu WA nyama.
Hao tukatoka nikijifanya nimenuna😉 Njiani tunarudi home ananiambia Leo nimemkomesha làkini naye amenikomesha. Nikajifanya bàdo ninahasira zangu kumbe drama. Nilitaka nizifanye hisia zake ziwe huru.
Baadaye Maisha yakaendelea,

Siku Moja tupo Mji mkongwe (Stone town) pale Zanzibar kwèñye Moja ya migahawa. Binti Kimoso hakujivunga na hicho ndîo kitû Watibeli wôte tunapenda. Nikamuuliza aagize, akaniangalia huku akitabasamu. Akaagiza mazagazaga, nami nikaagiza.
Tukala tukafurahi.

Nilimwambia siwezi mpeleka sehemu àmbayo sijaifanyia uchunguzi kuhusu gharama, na kama sijafanya uchunguzi Basi tangu mwanzo Kabla hatuanza vacation ninatoa bajeti ya Huko tuendako. Hii îli nisimweke kwèñye hofu na kutokuwa Huru kuagiza.
Lakini pia humpa nafasi ya kuamua kama hiyo safari twende au tusiende kwani Kwa bajeti iliyopo huenda hatutafurahia.

Uhuru usiwe upande mmoja. Yàani Mwanaume usimpe tuu mwenza wako Uhuru pekee huku wewe úkiwa haupo Huru Kwake.

Siku Moja Binti Kimoso nyakati hizohizo za mwanzoni tayari anauhuru na Mimi lakini alijua Mimi sipo Huru na yeye hasa kwèñye vipengele viwili.
Mosi, Pesa yake. Pili, Simu Yàngu.
Yeye alikuwa huru nîtumie Siku yake lakini Mimi sikuwa Huru aitumie Simu Yàngu
Huko messenger, inbobo na pm kulijaa madhambi.
Sikutaka aumie atakapoona meseji zangu jinsi ninavyochat na Wadada Wengine.

Siku Moja akaniambia twende sokoni. Sasa Mimi Muda huo sikuwa na Pesa. Nikawaza Huko sokoni tunaendaje na sina Pesa. Kama aliona niwazacho akaniambia yupo na Laki moja na arobaini.
Nilitaka nipinge kwenda yàani aende pekeake lakini nikasita ukizingatia sikuwa na sababu ya kumuacha aende pekeake.

Tunakaribia sokoni akatoa Ile Laki na arobaini akanipa. Akaniambia tukifika Mimi ndîo niwe nampa😆😂 Dadeki! Tukafika, chukue Huko, chukua kile. Mara ooh! Baby hii itafaa, mara ooh! Rangi hii NI nzuri, nikasema Hapa nimepatikana. Sasa akiniita vile mbele za Watu Mimi ñàona Jau😉. Naye alikuwa anajua akawa ananiita kimakusudi huku akitabasamu.
Kazi yàngu ilikuwa kuitika, kusema ndîo au hapana na kutoa Pesa Ambazo siô zangu ila weñye maduka walijua NI zangu😆 lakini sikuwa na Raha jàmani. Hela za Mwanamke kuzitumia unakuwa kama unakunywa Dawa bhana.

Tukatoka, tukiwa Njiani akaniambia, vile ninavyotaka yeye awe Kwa nini Mimi sipo Huru Kwake kutumia Pesa alizonazo. Mbona Mimi namsisitiza Pesa zangu NI zake lakini kwàke ñàona shida. Akasema wewe Mtibeli unatakiwa uishi maneno na sheria zako. Hapo Mimi mpole naangalia mbele natamani tufike.

Akazoea, Nami nikazoea. Hakuna Pesa yangu wala pesa yake.

Sasa Kanuni hiyo àmbayo niliitunga mwenyewe, kuna Wakati inaleta tafrani.
Siku Moja akaniambia anahitaji Pesa za matumizi yake binafsi.
Nikamuuliza kama shillingi ngapi, nikashangaa anaenda kuchukua peni na kidayari. Huyo upesiupesi Kwa furaha akidhani nitampa Pesa.
Akapiga piga Hapo huku akiniongelesha sasa Mimi siô kîla Muda ninaongea kuna Muda naandika au nacheza Game lakini yeye anataka Muda wôte tukiwa pàmoja ni- concentrate naye. Nisipofanya hivyo hujinunisha akitaka abembelezwe.

Akapiga hesabu Hapo akaniambia Kwa Mwezi nikimpa Laki Mbili Kwa mambo yake binafsi itakuwa shwangwa.
Nikamwambia Sawa. Akasema mbona sasa sijikiti kwèñye mazungumzo, nikanyanyuka nikaenda kuchukua Kadi za Benki zîpo Mbili. Nikamkabidhi.

Nikamwambia hizi Kadi za Benki NI zetu. Password NI .... Nikampa. Usiniombe Pesa. Nikamuuliza wewe Pesa YAKO unajiombaga? Akasema hapana. Si unatumia upendavyo akajibu ndîo. Basi ajisikie Huru.
Mabusu Kama yote😘 nikamwambia aniache niendelee na shughuli zangu

Akatoe Pesa aitakayo Kwa matumizi yake. Huyo akatoka, Mimi nikaendelea zangu na mambo yàngu. Nusu Sana huyo amerudi kanuna. AKajibwaga ati kavimbisha mashavu.
Nikamuuliza kulikoni. Akazirusha zile Kadi juu ya meza. Mimi nikaendelea kucheza Game.

Yàani Kadi zote Mbili zina elfu tisini tuu?😂😂😂😂 Nikaangua kicheko. Kisha nikamwambia NI Kadi zetu kipenzi. Kwa Sasa humu ndàni tuna elfu tisini. Na inatakiwa iende mpaka tarehe Fulani ndîo kuna hela nitapata. Akapiga hesabu zilikuwa kama bàdo wiki Mbili. Dadeki!
Ndàni kwenyewe kulikuwa HAKUNA chàkula.

Akanuna lakini baada ya lisaa limoja akakaa Sawa. Tukapanga ishu ya bajeti za kiuchumi Sasa. Na jinsi hela ndàni zitakavyotumika Kulingana na mipango yetu.

Uwazi WA bajeti katika uchumi ndàni ya mahusiano NI muhimu Sana Baina ya Mke na Mume. Hii itawasaidia katika kutimiza mipango yenu hata kama mnakipato kidogo namna gàni. Pia inapunguza kugombana Baina ya Mke na Mume

Zingatia, Moja ya chanzo cha migogoro katika mahusiano mengi NI kufichana vipato. Hii hupelekea Mke kuona Mumewe huenda anahonga nje kumbe hakuna kitu kama hicho.
Lakini vipato vyote vya Mke na Mume lazima vitumike ndàni ya familia. Kusiwe na kipato cha Mke na kipato cha Mume. Hii NI Kwa wale waliokwenye Ndoa weñye mpàngo kuishi mpaka Kifo kiwatenganishe.

Bajeti ya kusaidia Wazazi au ndugu jamaa na marafiki íwe bayana. Ninyi NI familia Moja. Lazima mpànge kuwa Pesa yetu hii itaenda Kwa Wazazi, hii Kwa ndugu, jamaa n marafiki na hii NI sadaka Kwa wahitaji.
Mwanamke kuwa na chake au Mume Kuwa na chake husababisha upendeleo. Na ukishapendelea unaondoa kitu kinaitwa Haki ndàni ya familia, ukishaondoa Haki automatic migogoro itaanza.

Miaka mitatu imepita, sitaki kumpa Binti Kimoso password ya Simu WALA ya mitandao ya kijamii.
Ila Simu yake alinipa kitambo, na password zake za mitandao ya kijamii ninayo. Ingawaje sikumwomba.

Wanaoendesha vuguvugu la mapinduzi wakitaka kunipindua 😉 nilikuwa nasoma makombora yao. Wengine ni Watu ninaofahamiana nao. Wengine washkaji.
Hakuna kitu kizuri kama kujua Watu wanaokulamba kisogo.

Ukikutana Unazungumza nao kama hakuna kinachoendelea. Hiyo kwangu siô tatizo.

Sasa Muda wôte nilikuwa najua Kabisa Binti Kimoso ananivizia aipate password yàngu baàda ya kuona sina mpàngo wa kumpatia.
Wanasema ukiishi na jasusi na wéwe utapata ABC za ujasusi.
Sasa Siku Moja usiku nimelala nashangaa naamshwa. Kulikoni! Binti Kimoso ananipa Simu. Sikuipokea ikaiangalia Moja Kwa Moja nikaona ameshaingia kwèñye akaunti zangu za mitandao ya kijamii. Moyo Paaaaaaaaaaap! Nusura nikufe. Aiseeh siô Kwa presha Ile.

Nikatoka nikaenda Uani Kwanza bila kusema çhochote. Nikarudi nikaangalia Saa ilikuwa Sana kumi Kasoro za usiku.
Nikamwambia nimechoka Acha nilale alafu atanionyesha hicho alichoniamshia.

Nikalala nikamwacha Binti wawatu analîa. Asûbuhi hii Hapa. Mimi nilikuwa nimeshapanga chakufanya.
Nilipoamka yeye tayari alikuwa ameshaandaa breakfast.
Hapo nimetatizika Sana. Nikampa Pesa akaniletee mayai. Akatoka. Mimi huyo kwèñye Simu, select all kisha Delete maana ali-nscreenshot chat zangu zote tayari tunajuana Kwa kiasi Fulani na anajua Mimi NI MTU WA aina gàni.

Nikiri wazi, hiyo ndîo Siku ya Kwanza Kwa Binti Kimoso kunipiga bao., kunizidi Akili. Kwanza aliipata Wapi password yàngu, hiyo siô kesi
Kumbe yote nafanya ya kufuta zile pîcha za chating yeye alikuwa hatua mbele yàngu. 😆
Namaliza kufuta nashangaa mlango unagongwa, si niliufunga bhana ili akirudi asinipate Kwa urahisi nikiendelea kufanya mafekeche yangu.
Zikafutika lakini akawa anagonga nikichelewa kufungua mlango nitamkasirisha. Nikaenda kufungua. Nikijifanya nîlikuwa bafuni napiga Mswaki, muda huo ninamswaki mdomoni weñye Dawa😆 haya mahusiano haya.

Akaingia Mimi nikiwa naangalia mikononi mwake kuona kama amebeba mayai, hakuwa amebeba. Nikajua alikuwa amerudi chapu ili anikûte. Nikajiona mjanja.
Akaondoka tenà, nikafuta meseji ya kwèñye mitandao ya kijamii. Aliporudi tukanywa chai huku nikisubiri Muda WA Jalada/Kesi kusikilizwa. Nishafuta ushahidi Hana uthibitisho

Kesi ikaanza, oooh! Kumbe hutaki nishike Simu yako Kwa sababu unajua unamadudu YAKO.
Madudu gàni, embu acha hizô nikawa najisemesha huku nikimbembeleza

Akachukua Simu akasema anhaa umefuta! Nilijua tuu utafuta.
Nikamwambia nimefuta nini. Hujui enhee!
Nikamwambia aache mambo hayo Mimi ninampenda, na sina uchafu wowote🙄 akasema najua huku hukufika.

Sasa kumbe kuna App ñyiñgine aliipakua àmbayo ukifuta video au pîcha zinaenda kuhifadhiwa kwèñye hiyo App.
Akazifungua, dadeki! Nikabaki ninacheka Sana. Kwa mara ya Kwanza Binti Kimoso kanichezea faulu, Dadeki. Kanizidi ujanja.

Nikaanza kumsifia alichokifanya kimenikosha Sana. Nikamwambia sikutegemea mpenzi wàngu unaakili namna hii. Wewe NI jike la Simba.
Akatabasamu, nilijua tuu ungefuta hata Ile kunituma mayai asûbuhi asûbuhi nilijua NI tricky tuu.

Lakini nikamuelewesha Kwa nini sikutaka aone. Sikutaka aumie. Hatà hivyo chats nyingi zilikuwa za Miaka miwili Nyuma. Chache zilikuwa za hivi karibuni.

Tangu Siku hiyo nikatoka katika jela ya kuficha Simu akawa anatumia yangu akitaka.
Kûna Muda unakuwa na mchecheto WA kutongoza, lakini utafanyaje Sasa.

Kuishi na mwenza kunahiajj
1. Upendo WA kwèli,
2. Muda Kwa ajili ya kûèlewana na kîla mmoja apunguze Yale yanayomkera mwenzake.
3. Kufurahia na kusapotiana hobby za MWINGINE.
4. Uwazi na Uhuru wa mazuri na Mabaya Yenu.

Nimechoka kuandika, tutaendelea Siku ñyiñgine naamini wale wakujifunza wamejifunza, wakuburudika mmeburudika, wakudharau mmedharau.
Yote Kwa yôte ñawatakia jioni Njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Robert hariel Mtibeli much respect bro, kwa vijana Kataa ndoa kama hamjachota chochotee....... Itaishia na kusema anyway.
 
Back
Top Bottom