PreGE2025 Mwakajoka: Tuhuma za waliohama CHADEMA hazina Msingi, walishiriki mageuzi wakiwa ndani ya Chama

PreGE2025 Mwakajoka: Tuhuma za waliohama CHADEMA hazina Msingi, walishiriki mageuzi wakiwa ndani ya Chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Katika kipindi ambacho baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakitangaza kuhama na kujiunga na vyama vingine, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Frank Mwakajoka, ameeleza kuwa hatua hiyo inaonyesha kushindwa kwao kuvumilia misimamo ya chama. Amesema kuwa wanachama hao hawawezi kuipuuza kauli mbiu ya chama ya “NO REFORM NO ELECTION”.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama zilizopo Kanda ya Nyasa, Mwakajoka amesema kwamba tuhuma zinazoibuliwa na baadhi ya waliokihama chama hazina mashiko, kwani walishiriki hatua mbalimbali za mageuzi chini ya uongozi wa aliyekuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe. Ameongeza kuwa ni jambo la kushangaza kuona wanageuka na kuikosoa misimamo ambayo waliwahi kuisimamia.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pia, Mwakajoka amesisitiza umuhimu wa CHADEMA kujibu propaganda na taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya waliokihama chama. Anasema chama hakiwezi kunyamaza wakati ukweli unapotoshwa hadharani.

“Mwaka 2020 tulipoteza wanachama wanane katika uchaguzi mkuu. Je, ni busara kurudia mazingira hayo tena? Ndiyo maana CHADEMA tunasimamia msimamo wetu wa ‘Hakuna Mageuzi, Hakuna Uchaguzi.’ Tunataka Watanzania waelewe ukweli kwa sababu mengi yanayosemwa si ya kweli,” alisisitiza Mwakajoka.
 
Back
Top Bottom