Mwakasege na Martha Mwaipaja wamshitaki Mbarikiwa na hivyo account yake YouTube hatarini kufutwa

Mwakasege na Martha Mwaipaja wamshitaki Mbarikiwa na hivyo account yake YouTube hatarini kufutwa

Ikifutwa mnishtuwe niende kudislike kwenye alaunti zao uko YouTube
 
Anaandika mwakipesile mbarikiwa

Christopher & diana mwakasege pamoja na martha mwaipaya wamemshitaki mbarikiwa youtube na account ya mbarikiwa hatarini kufutwa (huo ujumbe ulio katika picha hapo chini umetoka youtube na umeeleza hayo).

Hawa na wafuasi wao ndio moja ya wahubiri wanaosema kuwa kuchukua hatua za kulalamika pindi unapoonewa au unapoumizwa ni kupigana vita kimwili au unatakiwa umwachie mungu apigane mwenyewe.

Swali ni je,

1. Utamwachia mungu apigane mwenyewe kwa wale ambao ukiwalalamikia watakuua au kukutia ndani au kwa mambo yote?

2. Kwa nini wao wanapoona kuonewa na mbarikiwa hawamwachii mungu apigane mwenyewe??

3. Kwa nini wafuasi wao hawamwachii mungu acomment ila wana comment wenyewe?

Hii ni ajabu kweli kweli. Mbarikiwa akilalamika kuuawa kwa mtoto wake anapigana mwilini ila nyie kulalamika kuwa mbarikiwa anawatukana ni kupigana kiroho. Mkimsikia mbarikiwa analalamikia jambo au kukosoa jambo, ni anafanya vita mwilini, amepotea nk. Ila nyie mkilalamika au kukosoa kwa comment au kwa wenye mitandao mko rohoni au mnapigana rohoni na hamkosei.

Sijaona ajabu kwa sababu iliandikwa kuwa; nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu (luka 21:16-17). Nafahamu fika kwamba dunia yote imekuwa adui wa ninachofanya. Hata kama kuna anayeniunga mkono nje ya watoto wangu ni kwa siri na kwa namna isiyo na nguvu ya kubeba jambo sawa na maumivi yangu. Mimi nafahamu kuwa ni mwanadamu/ mhubiri niliye na haki ya kuongea, kukosoa, kupinga, kukaripia nk. Siamini kwamba ni mtu ambaye ninatakiwa kupingwa tu au kuonewa tu au kutukanwa tu nk. Yaani wengine kuua mwanangu ni kiroho mimi kulalamika ni kimwili. Wengine kunitukana kwa comment na mahubiri ni kiroho ila mimi nikifafanua ni kimwili.

Najua sina mahakama ninayoweza kushitaki. Na mungu wangu ameamua kunyamaza. Mke wangu na watoto wangu tuko katika msiba usiokoma. Tufanye kuwa mimi ni mwanadamu niliyekosea kila kitu duniani ila sijutii. Na ninaamini kuwa sina uwezo wa kufurahisha kila mtu. Na sina mpango wa kuongea kila kitu kwa namna wanavyotaka wote. Zaidi ya hayo najua kuwa hata mnaotukana sana au ku comment kwa namna udhaniyo kuwa ni sahihi si kwamba wewe ndio unafurahisha kila mtu.

Mimi nimefanya niliyotakiwa kuyafanya. Kwamba ni ya kimwili au kiroho hivyo ndivyo nilivyotakiwa kufanya. Najua ni hasara kiasi gani nilipata channel ya kwanza (iliyokuwa na jina mbarikiwa mwakipesile) ilipofutwa na subscribers 65k. Kisha nikaanza moja kwa hii ya kikosi kazi cha injili ambayo sasa ina subscribers 55.6k. Na najua ni hasara kiasi gani nitapata akaunti hii ikifutwa. Na kwamba kwa kigezo hicho kilichowekwa sina uwezo wa kukivuka. Kwani ikiwa mungu analalamikiwa, mimi ni nani nisilalamikiwe? Nafahamu fika kwamba hii ndiyo moja ya akaunti inayofuatiliwa zaidi na watu. Na kwamba tatizo si hilo tu la akina mwakasege.

Nafahamu fika kuwa hapa nimefungwa miguu na mikono na kutupwa katika shimo lefu asimoweza kuniona, kunisikia au kunitoa mtu. Aibu ni yangu, matusi ni yangu, kuhangaishwa polisi, mahakamani na magereza ni kwangu na hatimaye kuuliwa kwa mwanangu na kuuawa mimi na mke wangu ni kwangu.

Mlio salama na mtakaobaki wote ndio watakatifu, wenye hekima nk. Asanteni dunia kwa malipo mliyonilipa. Ila naamini mtakuja kunikumbuka.

View attachment 2763775
Una uhakika na ulichokiandika au ndo story za kusikia?
Huyo mtu alishamuona ,ajikite kwenye kueneza injili aachane na majina ya watu lkn hasikii,akaona sifa!
Mwal.hanaga muda, hajawahi na Huwa hamjibu mtu!
Hivi unapata wapi muda wa kusimama madhabahuni na kuanza kuongelea watu?
Kwamba huoni Cha kuhubiri au?
Ifike mahali madhabahu zitumike Kwa vitu sahihi sio mambo ya kijinga!
Ushauri chubguza kitu,upate uhakika kabla hujakileta kwenye public!

Huyo mtu mwenyewe chenga na ameshatukana watumishi wengi wanamuangalia tu!
Aisee
 
Hana shida mwakasege wa watu siijui hii story yao ila itakua kakosewa
Yaani baba wa watu hanaga muda na mtu
Hata asemwe,atukanwe hutakaa unisikie anajibu popote au kuongea!
Ndo kinachowapa shida

Halafu mpk abiudi wa misholi katukanwa humo!
Tena alikuwa anajidifia kabisa huyo mwakipesile
 
Mbarikiwa ungejipa muda kidogo Na mambo ya Mitandao Komaa tu na Mungu wako
Eeh ss huko jela yamkini atapata muda,
This is too much
Cha ajabu watt wake wa kiroho na mkewe wanaendelea na hayo mambo kwenye hiyo acc🤔
 
Back
Top Bottom