Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Simon Mwakifwamba, ametoa onyo kali kwa wanachama wa CCM ambao watakuwa kikwazo cha ushindi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Amesema chama hakitasita kwenda nao jumla jumla wale watakaozuia kufanikisha malengo ya kushinda, kwani lengo kuu la CCM ni kushika mamlaka ya kuiongoza Tanzania katika nyanja zote za uongozi. "Hatuna mpango wa kugawana uongozi na mtu yeyote; labda itokee bahati mbaya tu," aliongeza Mwakifwamba.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa Kata ya Minazi Mirefu, Jimbo la Segerea, Ilala Mwakifwamba amewataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha kata hiyo inajiweka katika hali ya ushindi kwa kuondoa tofauti zao na kushikamana. Alihimiza mshikamano ndani ya chama ili kuhakikisha ushindi huo unapatikana.
"Wekeni kata katika mkao wa ushindi, na mkao wa ushindi ni kuondoa migogoro. Tusahau yaliyopita, mnakumbuka madhara ya kutawaliwa na upinzani kwa miaka mitano. Mlikuwa kama watoto yatima, wakati huo watu walikuwa wanavalia sare nje ya kikao," amesema Mwakifwamba, akisisitiza umuhimu wa kushirikiana ili kuzuia kurudi kwenye hali ya utumwa.
Pia aliwataka viongozi kufahamu kuwa sasa kuna kazi moja tu mbele yao – kuhakikisha kwamba wapinzani hawapati nafasi tena ya kutawala. Mwakifwamba amesisitiza kuwa mshikamano ndani ya CCM ni muhimu ili kufanikisha lengo la ushindi wa chama hicho katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, mwezi Novemba 27.
Pia, Soma:
+ Fadhili Maganya: CCM hatuna mpango wa kutoka madarakani, ushindi kwetu ni lazima