Mwakilishi wa TANESCO: Mchakato wa kuuza umeme nchi jirani unaendelea

Mwakilishi wa TANESCO: Mchakato wa kuuza umeme nchi jirani unaendelea

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) limesema mchakato wa kuuza umeme nje ya nchi umeanza kwa kujenzi wa njia za kusambaza umeme huo kuelekea Malawi, Uganda na Kenya

Mwakilishi wa Shirika hilo, Odilo Mutalemwa amesema hayo kwenye Maonesho ya Sita ya viwanda yanayofanyika visiwani Zanzibar

Mutalemwa amesema “Tunategemea tutakapokuwa na umeme mwingi zaidi tutauza nje ya nchi. Sasa hivi tunaendeleza miradi mbalimbali ya kutengeneza njia kubwa za umeme (Transmission Line)”

Hoja yangu:
Hivi haya maneno si kejeri kwa sisi ambao tunashindwa kufanya kazi za kutuletea kipato!

ITV nao wanahoji je mkakati wa kuuza umeme nchi za nje unakwenda sambamba na kuboresha huduma hiyo hapa nchini?
 
Nasikia kuna umeme wa ziada unaozalishwa kiwanda cha miwa TPC pale Moshi, TANESCO waliombwa waunganishe na mifumo yao kusaidia Taifa, lakini cha kushangaza nasikia huo umeme unauzwa Kenya kwa makubaliano na TANESCO na miundo mbinu iko wazi kabisa.
 
Yaani ukamuuzie chakula jirani wakati wewe mwenyewe unanjaa mpaka watoto wanalia ?
Mkuu unashangaa nini? Kumbuka wakati hule watanzania walifukuzwa msumbiji hawana vyakula na malazi lakini Jiwe na upuuz Wake badala ya kuwasaidia na kuwatetea aliwatukana na kuwaambia shauri zao na kuenda mbali kuambia serikali ya msumbiji iendelee kuwafukuza.

Mafuriko yakatokea msumbiji Jiwe kwa kimbelembele chake akatuma misaada ya chakula malazi nk kwa wamsumbiji kupitia profesa jalalani watu wakabaki kushangaa WTF!
 
Kumuelewa Magu inahitaji akili. Alikuwa serious kwenye vitendo na strategies.
Huo mradi aliusimamia kwa nguvu sambamba na bwawa la mwl Nyerere na miradi mingine. Ili miradi ikianza kuzalisha umeme kwa wingi basi tunauza moja kwa moja umeme wa ziada
 
Umeme wa REA ni taabu tupu!
 
Hahahahahaha... Tujikite tuendako, tupo na samia. Kwa jinsi ulivyoandika tulikuwa tushampata museveni wetu. [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
before we even think of exporting power to neighboring countries, we better think of power distribution infrastructures, which lead to erratic power supply
 
Nchi ya majinun hii. Hapa nchini tu hautoshelezi.

BTW, nchi gan inaweza kununua umeme unaokatika- katika kila baada ya sekunde?
 
Kigoma Leo hakutakuwa na umeme kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni
 
before we even think of exporting power to neighboring countries, we better think of power distribution infrastructures, which lead to erratic power supply
Viongozi wetu wanapenda sana sifa na kiki zisizo na uhalisia!
 
Back
Top Bottom