JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakizungumza na waandishi leo juni kwa nyakati tofauti Juni 24, 2025 wamesema tangu Mwaka 2016 maalbino wanauawa kama Wanyama lakini Sheria kali za kuwalinda wanyama kama Tambo na wengine zimeundwa lakini hakuna sheria mahususi ya kumlinda albino hivyo wametaka mwasaada wa dharula wa sheria ya kuwalinda maalbino kupitishwa bungeni.
Sarah Katanga Muwakilishi wa walemavu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA amesema "Tunamuomba Rais Samia Suluhu atoke hadharani atamke kutaka kuwepo kwa mswaada wa dharula wa kuwalinda maalbino,ameongeza kuwa kumekuwa na sheria kali za kuwalinda wanyama,sheria za madawa ya kulevya lakini hakuna sheria maalum dhidi ya ulinzi wa ma albino"Amesema Sarah Katanga.