TADPOLE
JF-Expert Member
- Nov 18, 2015
- 2,914
- 9,472
Twaha anatakiwa ajengwe kwanza afike level za Mwakinyo hili tulinde thamani zao wote wawili kama wawakilishi wa nchi..yaani siku likiwekwa pambano lao wote wawe na thamani kama vile enzi zile Muhammad Ali na Joe Frazier au Tyson na Evender au hata Mayweather na Pacquiao kuwapambanisha sasahivi ni kuionea thamani na brand ya Mwakinyo aliyoijenga kwa tabu sana..Halafu huu mchezo wa kupigania sijui Magari,mara viroba vya ufuta ni kushusha thamani ya mchezo husika ipo siku mtu atakuja na gunia lake la uwele kutoka Mpwapwa halafu awatake mabondia wetu wapambane kama majogoo vile..All in all Twaha kiduku ni bondia mzuri na Mwakinyo pia ni bondia mzuri