Mwakinyo ashinda pambano lake dhidi ya Tinampay

Pambano la Mayweather vs Pacquiao halifanani kabisa na pambano la Mwakinyo na Tinampay

Defence ya Mawyweather ni ngumu sana kupenya kuliko ya Mwakinyo ,angalia hata highlights.
Nakubaliana na wewe ila jua viwango tofauti hata floyd alianza hivi baadae akazidi kuongeza umakini....
 
Aibu nimeona Mimi..haihitaji rocket science kutambua Kama Mwakinyo kapigwa..huku kubebana ndio kunatugharimu Kama taifa..
Tatizo la wabongo ujuaji mwingi. Kwa ambaye hajui ngumi ataona Mwakinyo ameshindwa. Ila kwa anayejua ngumi ataona Mwakinyo yupo vizuri.

Litizame pambano la Andy Ruiz Jr. Vs Anthony Joshua halafu utajua kwa nini Joshua alipigwa.

Joshua ni mrefu Andy ni mfupi. Tafsiri yake mikono ya Joshua ni mirefu ya Andy ni mifupi. Joshua upigaji wake ulikuwa Andy akirusha naye anarusha! Lakini Andy alijua akipigana na Joshua kwa style hiyo atapigwa. Kwa sababu mikono yake ni mifupi na ya Joshua ni mirefu, mpaka amfikie Joshua kwa mtindo wa piga nikupige atakuwa ameshakula vitasa vingi sana.

Andy alichokifanya ni kutompa nafasi Joshua. Akawa anapiga ngumi cherehani. Alicho' feli Joshua akawa anapigana na Andy inside fighting. Hii ni hatari ukiwa na opponent wa namna hii. Kingine Joshua alifeli kwenye guard kwa sababu upiganaji wake ulikuwa piga nikupige.

Mwakinyo alichokutana nacho ndicho hicho hicho. Yeye aligundua mapema kwamba mpinzani wake hampi nafasi. Kwa maana anarusha ngumi nyingi kwa wakati mmoja. Kwa vile upiganaji ni wa point inabidi umtafute huyo mpinzani wako.

Advantage aliyoitumia ni kulalia kamba! Hii ni advantage kwenye ring. Kwa sababu opponent wa Mwakinyo inside fighting anakumliza. Mosi, hata kama ukiweka guard lakini guard inaambatana na uvumilivu, kuna ngumi zitaumiza hiyo guard yako. Pili, ngumi utakazorushiwa lazima nzito zitakuwemo!

Ukipigwa kikombe kizito hata kama umeweka guard kitakurudisha nyuma. Lakini ukumbuke unapigana na mpinzani anayerusha ngumi nyingi sana kama cherehani. So ukiyumba unapoteza balance ya kwenye miguu. Ni hatari kwa sababu utaangushwa!

Cha kufanya lalia kamba zinakupa support halafu unamuhama kwa kishtukiza, then unamtia bomba! Bomba! Mpaka anakuja kukaa sawa tayari wewe una point zako huku ukimzungusha kwenye ring kwa maana unamtafuta.

Ngumi ni technique.
 
Sisi tulioanza kufuatilia ndondi enzi za kina George Lister Sabuni, Koba Kimanga, Joseph Marwa, Rashid Matumla, Mbwana Matumla, Maneno Oswald "mtambo wa gongo", Hassan Matumla, Haji Matumla, Mzonge, Michael Yombayomba ni dhahiri huyu bwana mdogo anatudanganya
 
Wengi humu hawajui ngumi mkuu ndio maana wanaingiza siasa na wengi wao ni ukawa hawapendi kuona tz inapata ushindi maana sifa zitaenda kwa serikali, mimi ni mpinzani lkn sipingi kila kitu.
Na huu ndio ujuha wa watanzania mkuu,kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu
 
Sisi tulioanza kufuatilia ndondi enzi za kina George Lister Sabuni, Koba Kimanga, Joseph Marwa, Rashid Matumla, Mbwana Matumla, Maneno Oswald "mtambo wa gongo", Hassan Matumla, Haji Matumla, Mzonge, Michael Yombayomba ni dhahiri huyu bwana mdogo anatudanganya
Nani kakwambia kuwa kutajataja majina ya boxers ndio utatuaminisha kuwa unaujua vema huu mchezo????!!!

Acha kujidanganya
 
Kwa mara ya kwanza kushuhudia ndondi live ilikuwa ni mwaka 2009 katika tamasha la mtikisiko mpambano ulikuwa kati ya CHUPAKI CHIPINDU(R.I.P) wa Makambako vs RASHID MATUMLA.
Mashabiki wa kuanzia MAKAMBAKO,MAFINGA NA IRINGA wote tulikuwa kwa CHUPAKI.CHUPAKI akawa anarusha ngumi nyingi na tukamuona kama anashambulia sana na tukajua ndo mshindi wetu,la hasha kumbe zile ngumi za jamaa zilikuwa hazina maana yoyote kama za TANMPAY jana,lakini MATUMLA alikuwa anajikinga sana na kurusha ngumi chache za maana ambazo zilikuwa zinamkuta CHUPAKI na ndipo alipompiga bao.Na kama jana kwa MWAKINYO nililiona hilo na ule ushindi ni halali kabisa kwani pamoja na MWAKINYO kushambuliwa sana na tungumi twingi,tule hatukuwa na maana yoyote kwani tulikuwa hatuendi maeneo muhimu lakini MWAKINYO alimpa jamaa ngumi za haja yule jamaa maeneo muhimu.
Halafu hata TANMPAY rekodi yake bado mbaya tu L16 kati ya 51,kiasilimia MWAKINYO ana rekodi nzuri.
viva MWAKINYO,ulistahili ushindi.
 
Nani kakwambia kuwa kutajataja majina ya boxers ndio utatuaminisha kuwa unaujua vema huu mchezo????!!!

Acha kujidanganya
Endeleeni kushangilia Si ameshinda? Acha namm nitaje mabondia wa kweli siyo wa maigizo igizo ulingoni
 
Follow this link,maybe pia ikiunganishwa na uzi ni vizuri....hii link inafundisha jinsi Ya ku-win points kwenye boxing match

Tatizo la wabongo ujuaji mwingi. Kwa ambaye hajui ngumi ataona Mwakinyo ameshindwa. Ila kwa anayejua ngumi ataona Mwakinyo yupo vizuri.

Litizame pambano la Andy Ruiz Jr. Vs Anthony Joshua halafu utajua kwa nini Joshua alipigwa.

Joshua ni mrefu Andy ni mfupi. Tafsiri yake mikono ya Joshua ni mirefu ya Andy ni mifupi. Joshua upigaji wake ulikuwa Andy akirusha naye anarusha! Lakini Andy alijua akipigana na Joshua kwa style hiyo atapigwa. Kwa sababu mikono yake ni mifupi na ya Joshua ni mirefu, mpaka amfikie Joshua kwa mtindo wa piga nikupige atakuwa ameshakula vitasa vingi sana.

Andy alichokifanya ni kutompa nafasi Joshua. Akawa anapiga ngumi cherehani. Alicho' feli Joshua akawa anapigana na Andy inside fighting. Hii ni hatari ukiwa na opponent wa namna hii. Kingine Joshua alifeli kwenye guard kwa sababu upiganaji wake ulikuwa piga nikupige.

Mwakinyo alichokutana nacho ndicho hicho hicho. Yeye aligundua mapema kwamba mpinzani wake hampi nafasi. Kwa maana anarusha ngumi nyingi kwa wakati mmoja. Kwa vile upiganaji ni wa point inabidi umtafute huyo mpinzani wako.

Advantage aliyoitumia ni kulalia kamba! Hii ni advantage kwenye ring. Kwa sababu opponent wa Mwakinyo inside fighting anakumliza. Mosi, hata kama ukiweka guard lakini guard inaambatana na uvumilivu, kuna ngumi zitaumiza hiyo guard yako. Pili, ngumi utakazorushiwa lazima nzito zitakuwemo!

Ukipigwa kikombe kizito hata kama umeweka guard kitakurudisha nyuma. Lakini ukumbuke unapigana na mpinzani anayerusha ngumi nyingi sana kama cherehani. So ukiyumba unapoteza balance ya kwenye miguu. Ni hatari kwa sababu utaangushwa!

Cha kufanya lalia kamba zinakupa support halafu unamuhama kwa kishtukiza, then unamtia bomba! Bomba! Mpaka anakuja kukaa sawa tayari wewe una point zako huku ukimzungusha kwenye ring kwa maana unamtafuta.

Ngumi ni technique.
Mkuu uko sahihi kwanza kunaajabu gani kwa kubebwa mwakinyo juzi tu hapa tumeona libya ikipewa peneti hewa na kama huyo mfilipino yuko vizur kwa nini asimalize mchezo mapema
 
Wewe hujui boxing, usibishe.
Wewe ndiyo unajua sana na ni lecturer wa sheria za ngumi, mtatetea sana ila bahati nzuri mchezo ulichezwa hadharani na nilikuwepo Uhuru na leo nimeirudia clip ya azam TV kwahiyo Mwakinyo amesaidika na unyumbani siyo ushindi wake.
 
Ni ngumi za namna gani ambazo zinatoa score kwenye boxing?
 
Back
Top Bottom