RAHA KAMILI
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 203
- 83
Bondia Hassan Mwakinyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na kampuni kubwa zaidi ya kubashiri nchini ya SportPesa.SportPesa imesaini mkataba huo na kuutangaza leo ingawa ni kiasi gani imefanywa kuwa siri.Mkataba huo kati ya Mwakinyo na SportPesa umesainiwa mbele ya waandishi wa habari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Baada ya kusaini mkataba huo, Dk Mwakyembe aliwapongeza SportPesa kuamua kuingia kwenye ngumi na kumuamini Mwamkinyo.Naye Akizungumzia kuingia kwa mkataba huo Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas, alisema wao kama kampuni wanajisikia faraja kudhamini suala la ngumi kwani imekuwa desturi yao kuhakikisha wanadhamini mambo ya michezo kwa lengo la kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao.
Kudhamini vipaji kama hivi ni jambo la kawaida sasa kwetu kwani tulianza kudhamini kwenye masuala ya mpira na leo hii tunaingia rasmi kwenye ngumi, lengo likiwa ni kuhakikisha tunaimalisha michezo yote hapa nchini,” alisema., kwingine pia kuna michezo mingine. Hapa tulianza na soka na baada ya mafanikio, sasa tunaingia kwenye ngumi na tumeanza na Mwakinyo lakini tusisitize, mkataba wetu utabaki kuwa siri,